Natania
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 262
- 217
Ni Lazima niseme ukweli kuwa CHADEMA imeyumba mno na kama jitihada za makusudi hazijafanyika basi hiki chama kinakufa rasmi.
Haya Madudu ya akina Mbowe yanayoendelea kuanikwa na kutolewa utetezi usioeleweka yananifanya mimi niliyekuwa naichukia CCM nianze kutafakari upya kwani kwa sasa SIONI TOFAUTI YA CCM na CHADEMA (na huenda CHADEMA wanaweza kuwa hatari zaidi).
Nimefuatilia kiasi kauli za wabunge wa CHADEMA [ambao ndiyo wanafahamika sana] wakiongea kuhusu swala la Kitila, ZZK, Mwigamba -kwa kweli nimesikitika sana. Nimesikitika kwa kuwa mwanzoni niliwaona wabunge hawa kuwa vichwa ila kwa sasa nawaona viumbe hatari sana.
Ukiachilia mbali mbunge Lema ambaye yeye amekuwa haeleweki vema kwenye baadhi ya kauli zake kwa muda mrefu sasa, Mnyika, Mch. Msigwa na Lissu kwa kweli wameharibu CV zao vibaya mno kwa utumbo waliouongea kuhusiana na mgogoro unaofukuta Chadema. Sikuamini mtu kama Mnyika, Msigwa na Lissu wanaweza ku-support udikteta wa akina Slaa na Mbowe (na wengine wote) wa kuwaona wahaini watu ambao wanamawazo mbadala wa namna ya kumpata kiongozi wa chama. Mnyika ndo niliyekuwa namwamini sana lakini naye kajitosa kwenye siasa za ki-imla hata sijui kwa sababu gani.
Naomba nichukue fursa hii kuwapongeza wabunge na wanachama mahsusi wa Chadema ambao at least wameonyesha akili kwa kukaa kimya.
Ndiyo, pamoja na kwamba kukaa kimya wakati madudu yanaendelea ni unafiki, lakini ni heri ukae kimya uonekane una-akili kuliko kuongea ku-support madudu. Pongezi hizi ziende kwa Mbunge Joshua Nassari, Mbunge Halima Mdee, Wakili Mabere Marando, Prof. Safari na wengine wote ambao wamesahaulika wakati wa kutoa maoni haya.
UPDATES
Wakili Mabare Marando na Prof Safari nimewatoa rasmi kwenye list ya kupongezwa baada ya kusoma gazeti la Mtanzania wakisema wanaunga mkono maamuzi ya kamati kuu ya Chadema kwa maamuzi yaliyofanyika dhidi ya wale wanaoitwa wahaini. Vituko havitaisha Tanzania!