GE2025 Wenje: Chama kinachosusia uchaguzi ni cha fujo, nimepata wokovu CCM

GE2025 Wenje: Chama kinachosusia uchaguzi ni cha fujo, nimepata wokovu CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Wenje tangu ahamie CCM amecharuka zaidi :Alien: :Alien::Alien:

Vituko vinaendelea huko Wenje anasema amepata wokovu CCM leo hii anaiponda CHADEMA eti ni hawana mipango wanashinda Mtandaoni kazi yao nge nge nge nge nge

Uchawa ni mbaya yaani kama vile siyo Wenje wa enzi zile

-----------
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Nyamagana kupitia CHADEMA, Ezekiah Wenje amesema amepata “wokovu mpya” baada ya kuachana na kile alichokiita “chama cha matusi, malalamiko na makasiriko” na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Wenje alitoa kauli hiyo leo, Oktoba 18, 2025, katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika mkoani Katavi, ambapo amesema umati mkubwa wa wananchi ulioshiriki ni ushahidi wa nguvu ya chama hicho tawala

Wenje amesema vyama vinavyoshinda mitandaoni havina mipango wala mikakati ya maendeleo, na badala yake vimekuwa vikijikita katika matusi na malalamiko. Ameongeza kuwa taifa linapaswa kutofautiana katika sera za maendeleo, lakini linapokuja suala la ulinzi, usalama na amani, hakuna mjadala

Akiendelea, Wenje ametaja kuwa baadhi ya viongozi wa upinzani wamekuwa wakitumia kigezo cha tume ya uchaguzi kulalamikia matokeo wanaposhindwa, jambo aliloliita ujinga


 
Mwambieni akimaliza kubwabwaja hapo akafagie kaburi la kaka yake alieuwawa akijaribu kumtetea yeye dhidi ya hao aliojiunga nao
 
149116.jpg
 
Selemani Bungara amesema uamuzi wa CHADEMA kususia huu uchafuzi ulikuwa ni sahihi na amesema hatopiga kura 29octoba.
 
Back
Top Bottom