Wengine wanaweza sisi tunashindwa nini?

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
4,253
5,737
Tanzania imebarikiwa kuwa na mali nyingi za asili ikiwemo maziwa makuu mawili ya Victoria na Tanganyika. Jografia ya mikoa ya Mwanza na Kigoma imetunukuwa kuwa na maziwa haya mawili ambayo ni maarufu na ni kivutio kwa yeyote anayebahatika kuitembelea.
Kuna baadhi ya nchi hazina rasilimali kama zetu ila zile walizobahatika kupata wameziongezea thamani kwa kujenga miundombinu imara na hivyo kuyafanya mazingira wanayoishi kuwa rafiki na kwa kweli nyumbani kwa hapa duniani.
Ukifika Mwanza pamoja na uzuri wake wa asili,utashuhudia ujenzi wa hovyo usiofuata mipango miji,Kwa Kigoma ndio kabisa,ujenzi wa kijijini umehamishiwa mijini licha ya kuwepo wataalamu wa mipango miji na uwepo wa kile chuo maarufu cha ardhi UCLAS! Hivi hatuna kweli watalaam wanaoweza hata kuiga vile wengine wamefanya?...Kwanini Mwanza au Kigoma zisifanane na picha hii? ....
photo.jpg
photo.jpg
 
Unafananisha mbingu na ardhi ???cc bado Sana'a ndio maana hata wakenya wanasema mlima Kilimanjaro upoo kwao
 
Ukiwa na upeo mkubwa wa kufikiri wewe peke yako.... hamna la maana litawezekana kwa level ya taifa. ..

Lazima elimu iende kwa watu wote ili kupiga hatua na kuwa na maendeleo ya kitaifa.

ELIMU ELIMU ELIMU
 
Back
Top Bottom