Wengi wavurunda mitihani NBAA ................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wengi wavurunda mitihani NBAA ...................

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 2, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,266
  Trophy Points: 280
  Wengi wavurunda mitihani NBAA Saturday, 01 January 2011 12:01

  [​IMG]Mhasibu House Head Office of NBAA

  Nora Damian
  WATIHANIWA 739 wa mitihani ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), wamefaulu mitihani hiyo.

  Watihaniwa hao ni miongoni mwa watihaniwa 3,323 waliokuwa wamefanya mitihani hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Pius Maneno alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 22.2.

  Alisema watihaniwa 1,021 watarudia masomo waliyoshindwa na na wengine 1,563 wamefeli.

  Alisema mitihani hiyo ilifanyika katika Novemba 2 na 5 mwaka jana na kwamba mitihani mingine itafanyika kati ya Mei 3 na 6 mwaka huu.

  Pia alisema watahiniwa 175 wamefaulu mtihani wa Shahada ya Juu ya Uhasibu (CPA).

  Alisema kwa sasa watahiniwa waliofaulu mitihani hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 35 iliyopita, wamefikia 3,422.
  Hata hivyo alisema mwanafunzi mmoja amefutiwa matokeo yake ya mtihani baada ya kukutwa na vifaa visivyoruhusiwa katika chumba cha mtihani.

  Mkurugenzi huyo alisema kutokana na kosa hilo mwanafunzi huyo ataruhusiwa kufanya mitihani ya bodi hiyo kwa muda wa miaka miwili.

  "Wale ambao hawajafuzu wasikate tamaa na badala yake, waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili waweze kufanya vizuri katika mitihani ijayo,"alisema Maneno.
  Alisema katika ngazi ya uandishi na utunzaji wa hesabu, watahiniwa 33 kati ya 134, wamefaulu na wengine 46 watarudia somo moja au mawili wakati watahiniwa 55 hawakufaulu.

  Alisema idadi hiyo inafanya jumla ya watahiniwa waliofuzu katika ngazi ya uandishi na utunzaji hesabu kuwa 3,254 tangu bodi hiyo ilipoanza kutahini mitihani ya cheti mwaka 1991.

  Matokeo ya mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 2,602 walifeli mitihani ya bodi hiyo.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zilaumiwe shule za kata?
   
Loading...