Wengi watinga kwa mkemia kujua uhalali baba wa mtoto

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1576126286212.png

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Kanda ya Kati, imesema asilimia 90 ya sampuli za kupima vinasaba (DNA) ilizozipokea, zililenga kuangalia uhalali wa baba wa mtoto.

Meneja wa kanda hiyo, Musa Kuzumila, aliyasema hayo jana alipozungumzia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka miwili na nusu tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo katika ziara ya timu ya maofisa habari wa wizara na taasisi zake mkoani Dodoma.

Alisema kati ya sampuli mbalimbali 5,106 zilizokusanywa kwa kipindi hicho, 36 zililenga kuangalia uhalali huo, akieleza kuwa majibu ya sampuli hizo husaidia kumaliza kesi au migogoro kwa wakati.

“Hapa sina takwimu sahihi za kina baba wangapi wamesingiziwa watoto ambao si wao, tumekusanya sampuli 36 za DNA, asilimia 90 kati ya hizo ni za kusaka uhalali wa baba wa mtoto.

“Huwa tunapeleka kuchunguza kwenye maabara zetu zilizopo Dar es Salaam na Mwanza, tumekusanya na kufanya uchunguzi sampuli 5,106 hadi Desemba hii.

"Tunapofanya uchunguzi wa namna hii, DNA inahusika moja kwa moja na kutoa ushahidi mahakamani na kusaidia kesi kutatuliwa kwa wakati,” alisema.

Alibainisha kuwa asilimia kubwa ya sampuli zilizokusanywa, zilikuwa za dawa ya kulevya hususan bangi. Alisema sampuli za dawa hizo wamekuwa wakizipokea kwa kiasi kikubwa.


Chanzo: IPP Media
 
Wanaume wamechoka kuibiwa mbegu!

Na inapogundulika mtoto ni wake, ndoa huwa tamu. Ila ikigundulika si wake tu, ndoa hakuna tena na vilio na simanzi hutawala.
Matukio mengi hayaripotiwi tu!

Mungu atusaidie sana aisee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaume wamechoka kuibiwa mbegu!

Na inapogundulika mtoto ni wake, ndoa huwa tamu. Ila ikigundulika si wake tu, ndoa hakuna tena na vilio na simanzi hutawala.
Matukio mengi hayaripotiwi tu!

Mungu atusaidie sana aisee!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kama hicho.

Kitendo tu cha mpaka mtu amekwenda kuhakikisha maana yake ni kwamba kuna "a seed of doubt" na baada ya hapo kamwe ndoa haiwezi kuwa tamu tena kama mwanzoni

Sana sana utamu utakua kwa mtoto wake kwakua atakua na uhakika asilimia 99 ni wake. Ila si kwa mke
 
Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Kanda ya Kati, imesema asilimia 90 ya sampuli za kupima vinasaba (DNA) ilizozipokea, zililenga kuangalia uhalali wa baba wa mtoto.


Kwanini kanda ya kati tu?
Nani analengwa?
 
Back
Top Bottom