DOKEZO Wengi wanaoshadidia sakata la wachina ni watu wa kawaida na sio wafanyabiashara. Tuache ushabiki na tuchukue hatua hizi stahiki

DOKEZO Wengi wanaoshadidia sakata la wachina ni watu wa kawaida na sio wafanyabiashara. Tuache ushabiki na tuchukue hatua hizi stahiki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Al-habiib

Senior Member
Joined
Jun 21, 2023
Posts
132
Reaction score
192
Habari wakuu,

Nimekuwa nikifuatilia mijadala mitandaoni, hasa kwenye Facebook, X na hapa JF, kuhusu sakata la Wachina kwenye biashara za rejareja.

Inaonekana wale ambao hawafanyi biashara au wanaoendesha biashara zisizotegemea uagizaji wa bidhaa kutoka nje ndio wanaoshabikia Wachina kuruhusiwa kuuza rejareja, eti kwa sababu bei zao ziko chini.

Sababu za Bei ya Mchina Kuwa Chini​

  1. Wachina Wameshika Soko la Afrika
    Wachina ndio wazalishaji wakuu wa bidhaa nyingi tunazoagiza barani Afrika. Wanamiliki viwanda na ndio wasambazaji wakuu wa bidhaa tunazouza. Lakini wanapokuja kuuza rejareja, wanavuruga mfumo wa biashara ambao umekuwepo kwa muda mrefu.
    • Mfumo wa biashara kawaida huwa na mlolongo huu:
      Manufacturer → Supplier → Distributor → Wholesaler → Retailer
    • Mchina, akiwa Manufacturer au Supplier, anavunja mfumo huu kwa kuuza moja kwa moja kwa mlaji wa mwisho (Retail). Hii inaondoa nafasi ya distributor na wholesaler, hivyo faida ambayo ilipaswa kwenda kwao inabaki kwake, na hii inampa uwezo wa kuuza kwa bei ya chini zaidi.
Mfano: Fikiria Mo Dewji au Bakhresa wangeamua kuuza bidhaa zao wenyewe moja kwa moja kwa wateja badala ya kupitia wasambazaji na wauzaji wa jumla. Unadhani nani atakuwa na bei rahisi?

Hali hii inaua ajira nyingi kwa sababu maduka ya wenyeji yanashindwa kushindana. Mwisho wa siku, biashara za wazawa zinakufa, na uchumi unashikwa na wageni.

  1. Wachina Wana Mkakati Maalum
    Si Wachina wote wana viwanda au ni wasambazaji wakubwa. Wengi wao ni wafanyabiashara wa kawaida wenye mtaji, lakini wanafaidika na mitandao ya viwanda vyao vya nyumbani. Wanapata bidhaa kwa bei ya chini sana na wanauza kwa bei ya chini hapa kwetu ili kuteka soko.
    • Kwa nini wanauza bidhaa kwa faida ndogo sana hata kama wamesafirisha kwa muda mrefu?
    • Kwa nini wanauza chini ya bei ya soko huku wakijua wameingia gharama za usafirishaji na ushuru?

Hili si jambo la kawaida katika biashara. Hii ni mbinu ya predatory pricing, ambapo wanapunguza bei kupita kiasi ili kushinda ushindani, kisha baadaye, wakiwa wametawala soko, wanapandisha bei na kudhibiti uchumi.

  1. Wahindi Vs Wachina
    Wengine wanajitetea kuwa hata Wahindi wamekuwa kwenye biashara kwa muda mrefu. Lakini kuna tofauti kubwa:
    • Wahindi wanafuata mfumo wa biashara wa kawaida.
    • Wahindi hawapunguzi bei kupindukia hadi washindani waanguke.
    • Mfano: Tanga Anjari, Toptang Tomato, Seifi Plastics, Jambo Houseware—hawa wote hawavunji mfumo wa biashara, na mara nyingi hata wanauza kwa bei ya juu zaidi kwa sababu wanawaheshimu wasambazaji wao.
  2. Kodi na Gharama za Biashara
    Mfanyabiashara wa kawaida anapoagiza bidhaa kutoka China, anapitia gharama nyingi—ushuru bandarini, VAT, na muda wa usafirishaji. Lakini mchina mwenyewe anapouza bidhaa hizo hapa, bado anaweza kuuza kwa bei ya chini zaidi ya mwenyeji. Inawezekanaje?
Bandari ya Dar es Salaam na Zanzibar zina viwango tofauti vya ushuru, ndiyo maana bidhaa Zanzibar ni rahisi zaidi. Hata hivyo, bado haielezeki kwa nini Wachina wanashinda wazawa kwa bei, hata wakiwa wamepitia mlolongo wa kodi sawa.

Suluhisho​

Tunahitaji kulinda biashara za wazawa kwa kuhakikisha:
  • Wachina hawauzi bidhaa rejareja moja kwa moja kwa mlaji wa mwisho.
  • Bei zao zinafuata viwango vya soko na haziwezi kupunguzwa kupita kiasi ili kuua ushindani.
  • Mfumo wa biashara unaheshimiwa—wafanyabiashara wa ndani wanapaswa kuwa na nafasi ya kusambaza na kuuza bidhaa.
 
Hata raia wa kawaida wasio wafanya biashara wanapaswa kulipigia kelele hili, mwisho wa siku impact yake itarudi kwa mtu wa kawaida sana maana itaua mzunguko wa hela Kwa wachina kuhodhi kila kitu na Watanzania kubaki wanunuzi wasio na hela zaidi ya kutegemea mishahara midogo mwisho wa mwezi.

Biashara za Watanzania zikifa NI Watanzania wote wanaoathirika sio wachina.. Serikali ianze kupambana na hizi Cartel za wachina, wahindi na waarabu kabla Hali haijaanza kuharibika.
 
Top ten za Matajiri Tanzania ni Wahindi na Waarabu, sio muda mrefu watakuwa wachina baadala ya weusi Watanzania wazawa.

Hizi jamii zinaoperate in cartel mode sio free mode ya watu wote kudominate wao huwa wanatengeneza kajikikundi chao kwa maslahi ya community zao, mfumo wa kizamani sana.
 
Watu wa kawaida ni wanadamu,.. watu wasio wa kawaida ni majitu wala watu/madalali

Sisi wenyewe ni wafanya biashara eti usituchukulie poa.
Miaka ya 2009 kuna biashara nilikua nafanya nikawa napata wateja hadi wananizidi japo ile bidhaa nilikua napata faida nusu kwa nusu... Miaka michache mbeleni watu wengine wakaleta biashara kama Ile yangu tena wakaiboresha alafu wakauza kwa punguzo la 30%! Kilichotokea nilianza kunyenyekea wateja lakini hawakunielewa kitu kilichopelekea nirudi shamba kubuni biashara nyingine
 
Watu wa kawaida ni wanadamu,.. watu wasio wa kawaida ni majitu wala watu

Sisi wenyewe ni wafanya biashara eti usituchukulie poa.
Miaka ya 2009 kuna biashara nilikua nafanya nikawa napata wateja hadi wananizidi japo ile bidhaa nilikua napata faida nusu kwa nusu... Miaka michache mbeleni watu wengine wakaleta biashara kama Ile yangu tena wakaiboresha alafu wakauza kwa punguzo la 70%! Kilichotokea nilianza kunyenyekea wateja lakini hawakunielewa kitu kilichopelekea nirudi shamba kubuni biashara nyingine
Wizi tu
 
Tukiacha uvivu, wizi wa kijinga, bei za kuangaliana usoni, ujanja wa kijinga, tutawaweza.
Ama sivyo tutabakia tulalamika na kupiga mayowe yasiyo na mshiko..
Igeni wachina wanachikifanya na siyo kukaa kwenye vibanda vya betting, chini ya miti, baa, vibarazani nk nk
 
Uo ni ukweli.. kwa mtu asie na maono ya mbali anae waza kununua chupi ya kichina ataona unaongea pumba, but jamaa hawafai hata kidogo mm niliwahi kufanya kazi kwao.
 
Kwa hiyo hapo tunalinda viwanda au tunalinda madalali, Cartel, wakwepa kodi ambao hutaka faida maradufu?

Uchumi upi huo tunao uogopa mchina asiushike, huu ulio shikwa na Waarabu na Wahindi?

Waacheni waje Ili wauze kulingana na bei halisi ya soko Ili mwananchi wa kawaida apunguze maumivu ambaye ndie final Consumer.

Jifunzeni, na muadapt mazingira mapya, la sivyo.................
 
Kwa hiyo hapo tunalinda viwanda au tunalinda madalali, Cartel, wakwepa kodi ambao hutaka faida maradufu?

Uchumi upi huo tunao uogopa mchina asiushike, huu ulio shikwa na Waarabu na Wahindi?

Waacheni waje Ili wauze kulingana na bei halisi ya soko Ili mwananchi wa kawaida apunguze maumivu ambaye ndie final Consumer.

Jifunzeni, na muadapt mazingira mapya, la sivyo.................
Yetu macho, msije mkaanza kulia Lia baadae
 
Back
Top Bottom