Wengi hushindwa kufanikiwa sababu hawataki kupoteza ili wapate

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
156
169
MAFANIKIO- ni hali ya kukamilisha lengo au dhumuni ambalo ulikua unatamani kulifikia siku moja. Kila binadamu ana malengo na mipango yake tofauti lakini wote wanafanya yote hayo kwa ajili ya mafanikio, huwezi kutana na mtu akuambie anawaza jinsi ya kuwa maskini huyo atakuwa anaiwaza dunia yake peke yake.

Lakini ili tufanikiwe inatupaswa tujue kwamba
Mafanikio ni mipango
Mafanikio ni Hatua na
Mafanikio ni kupoteza ili upate

Huwezi fanikiwa bila kuwa na mipango thabiti na inayoonekana, huwezi fanikiwa bila kuchukua hatua ambazo muda mwingine zitakufanya ujute kwa muda lakini ucheke maisha yako yote.

Wengi hushindwa kufanikiwa sababu hawataki kupoteza ili wapate. Binadamu anataka kupata tu bila kupoteza hii ni ngumu kwa mwanadamu yeyote yule angalia matajiri wote au watu wote maarufu waliofanikiwa ukiwauliza kuhusu hatua walizofata kufanikiwa utajua walipoteza mambo mengi sana na makubwa kuliko hata yako wewe unayoogopa kupoteza kwa muda mfupi na upate kwa muda mrefu na si muda mrefu bali maisha yako yote.

Katika hatua za kwenda kwenye mafanikio ndani ya mwaka huu 2017 kama kweli umedhamiria kufanya unachotaka ili ifanikiwe basi jiandae kupoteza vitu vingi, ikibidi hata marafiki zako wa karibu sana ambao wanakukubali wewe lakini hawaamini unachofanya kitakupa mafanikio wanaona unapoteza muda, Ila jiandae pia kuwapokea tena endapo utafanikiwa.

By Jay Speed
 
Tupo pamoja vijana tunaohitaji mafanikio

Umaskini tuupinge kwetu
 
Back
Top Bottom