Wembe uliomnyoa Wassira watumika kwa Lowassa

Mwanakijiji,

Lowasa akikataa inabidi kumpaka sana hapa JF na kwenye magazeti kwamba kaogopa kuongea na Watanzania wanaoishi nje, kisa wana uelewo kwahiyo hawezi kuwadanganya nk.

Hivi vita inabidi kupigana kwa njia zote.

Ningefurahi kuona CCM inavunjika ili akina Lowasa wabaki na Chukua Chako Mapema na waadilifu wengine wachukue CCM ya Mwalimu.
Leo hii unamtetea lowassa
 
Mwanakijiji,

Hujui madhara ambayo taifa litapata kama Lowasa ataachiwa kuchukua urais mwaka 2015. Inatakiwa kummaliza mapema kwa faida ya nchi yetu.

Ndio maana wengine tunapiga ngoma ndogo ndogo kuhakikisha vita na Lowasa inafanikiwa.
watanzania walikuelewa
 
heshima yenu wakuu.

jana ilikuwa siku ya kuanza ziara ya lowasa hapa Mbeya itakayochukua siku nane kikazi. pia ni siku ya huzuni kwake maana kama WAANDISHI huandika habari za kila mkoa vizuri, basi hamna mkoa ambao uliwahi tia fora kama huu mkoa wa Wanyakyusa, Wasafa, Wamalila, Wanyiha ambao ni wenyeji.

kabla ya ndege yake kutua katika ardhi hii, watu walisikika wakidai kuwa hawangeenda kumpokea maana serikali yake haifai.

mida ya saa 6 mchana, ndege yake iliwasiri katika Uwanja ule mbovu wa Somora Machehe; ukiwa na wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wenye uniform, scout, watu wenye jezi za kijani, na watu wenye vitambi. idadi ilikuwa ndogo sana kulingana na uwiano wa watu wa Mbeya. watu wengine walikuwa kandokando mwa barabara huku wakijaribu kujenga hoja za hapa na pale. hata mimi nilikuwepo.

mida ya saa 10 ndipo hotuba ya Lowasa ilipoanza kwa maswali kutoka kwa wananchi.

viongozi waliojaribu kujibu maswali huku wakiwa wanazomewa ni Chenge, mkuu wa mkoa, Meya wa jiji, Naibu waziri wa elimu nk, huku Lowasa akilazimika kutoa ufafanuzi kwa kiongozi.

Baadaye, Lowasa alianza hotuba iliyojaa utetezi wa Karamagi kuwa mkataba aliousahini ni bora kuliko mkataba wowote ule Tz na kwamba hauna tatizo lolote kisheria.

Akadai kuwa cement imepanda bei kwa sababu Afrika Kusini wananunua kwa wingi ili kujengea viwanja vya mpira wa kombe la Dunia, n.k

Pale uwanjani, Lowasa hakuzomewa sana kwa sabau zifuatazo.

1. kama mnavyojua, Lowasa ni msanii. alinza kwa kuuliza maswali ili apate cha kuongelea. mimi nilidhani hotuba inabidi ianze ili watu waulize pale ambapo hawakuelewa.

2.alikuwa anakatakata hoja. mfano, pale anaposema "karamagi hakufanya kosa:.......ghafla anasema .Mbeya oye....na kuingiza hoja nyingine kabla watu hawajatulia.

3.Tofauti na Wasira, uwanja huu ulikuwa umesheheni watu wengi, ingawa hawakukaribia wa Zitto. ila pia niliona magari aina ya Kenta pale uwanjani, idadi inazidi 10, na nikafikiri kuwa labda kwa sababu Mkutano ni wa kimkoa, yawezekana magari hayo yalisomba watu toka wilaya tofauti, ili waonekane wengi. pia ulijaa wanafunzi.

4. sababu, wengi waliokuwa karibu na jukwaa walikuwa na jezi za kijani, na ndio waliokuwa wanauliza maswali, basi inawezekana maswali yaliandaliwa ili kuondoa sumu iliobaki kipindi cha wasira, na hivyo maswali yenyewe hayakuwa na msisimko, waliouliza maswali ni sanasana wanafunzi wa sekondari.

5.labda kwa sababu Mwandosya, ambaye Mkoani hapa anaonekana kama sio mwanamtandao alikuwepo, na alikuwa hakuvaa Uniform za sisiem basi watu waliridhika kumwona. maana watu wa hapa wako tayari kumwaga damu ilimradi tu waone haki ikitendeka. mfano ni kile ninachosadikika kwa Akukweti, baada ya kuwaambia kuwa vibanda vyao vya mwanjelwa vilistahili kuungua sababu vilikuwa vinatia kinyaa mipanga ya serikali. siku hiyohiyo anapanda ndege hakuvuka hata km. 1; na pia woga wa kikwete kuja huku Mbeya, maana hata yeye walishamwambia akikanyaga hapa atakiona.

Baada ya mkutano;

wakati wageni wanaondoka, watu walisubiri uwanjani na kuanza kumshangilia Mwandosya. na wachache tu kuzomea lowasa na mkuu wa mkoa. ieleweke kuwa mkuu wa mkoa ni Mwakipesile, ambaye ni mzaliwa wa mkoa huu, na kipenzi cha muungwana au Kingwendu kama ajulikanavyo huku.

lakini Mwakipesile hapendwi kabisa, na aliwekwa huku ili kuondoa mbegu zote za wasio wanamtandao, akiwemo Mwandosya. pia anadistribute unequally, lasrimali za mkoa kwa sehemu zenye upinzani na zisizo na upinzani. sehemu zenye upinzani ni pamoja na Tukuyu, Kyela na Mbeya Mjini, wakati zenye unafuu ni mwambao wa Mbozi nk.

Mwanjelwa ndipo watu walipojipanga mstari kumzomea. ilikuwa hatari. ilibidi nipaki usafiri wangi mbali maana nilidhani kuna watu watasombwa na FFU, au kama wakati wa Lurdism, vijana wanaweza kuanza kuponda mawe na kuharibu kila kitu chenye thamani wakidhania kila mwenye gari ni miongoni mwa wale wale mafisadi.

Walianza kudai. hoo.hooo.., *******, shenzi, haya ndiyo maisha bora? viwanja vya kujenga vinapanda bei, sement inapanda bei, mnatuvunjia vibanda vyetu, alafu eti maisha bora, . tunamtaka kikwete aje hapa, kwa nini anaogopa. hu........nenda bwana hatukutaki......

walikuwa na miti, mawe, fimbo . utadhani kuna mtu alikuwa anawaratibu . kama kweli vyombo vya habari huwa vinaripoti, basi Tz nzima haijawahi tokea. niliogopa, nikamhurumia lowasa, nikasema laiti hasingeingia siasa.

unajua, mwanzoni wakati wanaanza kumzomea, lowasa hakujua, alitoa mkono kwenya dirisha kuwapungia, ndipo ghafla akaurudisha na kuangalia chini baada ya kuona mambo sio kawaida.

Maoni ya watu; nilijaribu kuuliza kwa nini hawakwenda kumzomea palepele uwanjani,

wakasema kuwa kulikuwepo na mpango wa askari kuwapiga na kuwakamata kama kisasi kwa Wasira iwapo zomeazomea ingetokea hapo uwanjani. pia walisema wanamtaka rais, kwa nini hataki kuja huku Mbeya. anaona Mbeya ni mbali kuliko marekani na ufaransa? eti tangu apate urais hajawahi kuja mbeya, kila kitu alichokiandaa Mkapa hakijakamilika kama vile Uwanja wa Ndege wa Songe ambao ni wa kimataifa, anachokifanya ni kugawagawa mkoa tu.

wanasema walibeba mawe na miti ili FFu wakitaka kuwashambulia basi vita ianze.

Ikumbukwe pia kuwa wakati wa ziara ya wasira, ilibidi akatishe ziara ya kutembelea Tukuyu na Kyella baada ya zomea zomea aliyoipata Mbeya mjini. sasa sijui na Lowasa ataikatisha au la. maana alipokuwa akisema .'Mbeya hoyeeee' walikuwa wanaitikia wachache. ila akisema 'SISIEM oyeeeeee' minung'uniko kutoka kwa watu inasema 'hapo ndipo anapoharibu kabisa'

Mh..... siasa za Mbeya we ziache zilivyo. unaweza andika siku nzima.

mimi ninatarajia kuanza safari ya kurudi Dar. wakati wowote, ila kitakachotokea wakati bado nipo nitawakujulisheni
Mtoa mada kama ni mwalimu basi tutarajie wanafunzi wake wengi kupata division Zero.
 
Back
Top Bottom