Wema Sepetu na Ommy Dimpoz kwa mara nyingine tena waonekana kwenye picha hizi tata

kipax96

Member
Dec 2, 2013
6
3
LICHA ya tetesi kuzagaa kuwa amerudiana na mpenzi wake, Idris Sultan, mtoto mzuri Bongo Muvi, Wema Sepetu kwa mara nyingine ametengeneza habari, amedaiwa bado anaendeleza uhusiano wa siri na staa wa Bongo Fleva, Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’,

Hiyo imedhihirika hivi karibuni baada ya kuvuja kwa picha mpya za wawili hao wakiwa chumbani katika mapozi ya kimahaba huku Picha moja wapo ilimuonesha Dimpoz akiwa amemwekea miguu Wema mgongoni huku nyingine akiwa ameegesha mkono kwenye kalio kitendo ambacho kinaleta tafsiri ya mtu na mtu wake.

Dimpoz amekuwa akiendelea ‘kujiweka’ kwa siri jambo ambalo watu wengi hawalitambui.
“Mbona kitambo tu, Dimpoz amejiweka kwake kiulaini, sema wenyewe wanafanya mambo hayo kwa siri. Si mnajua Dimpoz si mtu wa kutangazatangaza mambo yake na ndiyo maana hadi Nay wa Mitego (Emmanuel Elibariki) akafikia hatua ya kumhisi vibaya hadi kumuimba kwenye wimbo wake,”kilisema chanzo

MAZINGIRA YA TUKIO

Chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, picha hizo walipiga wenyewe chumbani, nyumbani kwa Dimpoz, Kinondoni jijini Dar hivyo zilibaki katika simu ya Dimpoz ndipo chanzo hicho kilipozikwapua na kuzituma kwa paparazi wetu.

“Bwana nakupa lakini msinitaje huko, nyie kamilisheni mambo yenu lakini habari ndiyo hiyo; Dimpoz na Wema ni kapo ya kimyakimya maana wenyewe hawataki kuanika mambo yao,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata ubuyu huo, Reporter wetu‘alimvutia waya’ Wema ili kumsikia anazungumziaje picha hizo na uhusiano huo unaodaiwa ni wa siri, simu yake iliita bila kupokelewa lakini baadaye rafiki yake mmoja alisema huenda hakupokea kwa kuwa siku hiyo alikuwa safarini kuelekea Dodoma.“Jana (Jumatano) aliniaga ana safari yaDodoma so (hivyo) nafikiri yupo njiani nawenzake na pengine kelele za wasanii ndani ya gari si unajua tena na kaenda na wasanii wenzake wengi tu,” alisema rafiki huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.

DIMPOZ HUYU HAPA

Baada ya kumkosa Wema, Repoter wetu alimtafuta Dimpoz ambaye alikiri kuwa picha hizo zilikwapuliwa kutoka kwenye simu yake lakini akadai hawana uhusiano wa kimapenzi.“Hizo picha nazijua, nakumbuka tulipiga hapahapa Dar. Ilikuwa ni hotelini na si nyumbani kama huyo mtu alivyowaambia lakini kitu cha msingi unachopaswa kujua,Wema ni mshikaji wangu wa karibu na hakuna kitu kingine zaidi ya ushikaji.

Kuna mtu itakuwa kanifanyia umafia kwenye simu lakini nitadili naye lazima nitamjua tu,” alisema Dimpoz.

KUMBUKUMBU

Wema na Dimpoz walidaiwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, Februari, mwaka jana walipokuwa wakirekodi video ya Ommy, Wanjera nchini Afrika Kusini.Picha zao ‘tata’ wakiwa chumbani zilizagaa kwenye mitandao ya kijamii na kuripotiwa katika vyombo vya habari.Baada ya hapo, Wema aliripotiwa kutembeana wanaume tofauti akiwemo Idris Sultan,mshindi wa Shindano la Big Brother Africa.

wema1.png


wema2.png


wema3.png
 
Namsikitikia wema jina lake halimsaidii. Kila siku linatumika vibaya. Hata makampuni yanashindwa kumtumia. Hajajua jina lake ndo lingempa hadhi ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio. Kashindwa kucheza karata kwa muda muafaka. Amebaki anaishi kwa kuigiza. Kila anachokiongea ama kukifanya kinaonekana ni uongo. Umri haudanganyi. Natamani azinduke sasa.
 
Namsikitikia wema jina lake halimsaidii. Kila siku linatumika vibaya. Hata makampuni yanashindwa kumtumia. Hajajua jina lake ndo lingempa hadhi ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio. Kashindwa kucheza karata kwa muda muafaka. Amebaki anaishi kwa kuigiza. Kila anachokiongea ama kukifanya kinaonekana ni uongo. Umri haudanganyi. Natamani azinduke sasa.
Hajawahi kabisa kujua kulitumia jina lake
Kwisha habari yake, kabaki kutafuta kik kupitia aunt ommy kaishiwa huyu
 
Hivi ni kwanini huyu binti anapenda sana kuongozana na vijana Wa kiume wenye uwalakini??
 
Punguza mahaba, mie namjua hata nikiona kivuli tu najua nichake
duu haha haha ndio dawa ila dimpoz inawezekana alivyosema ney kweli anatafuta kick za kuonekana na wanawake halafu chanzo ni yeye
walikua wanapiga stori tu inawezekana kama alivyosema
 
Back
Top Bottom