Wema ni akiba

Wema ni akiba

Mimi bana niliwahi kukopa benk. Sasa yule aliyesimamia mkopo wangu alikuwa mshikaji sana tulielewana sana sasa cku moja niko karibu kumalizia mkopo jamaa akaja na bonge la shida na ckuwa vizur aisee. Ilibid nikakope nimpe ile hela. Nafikir kuna hela ilipelea kule ndan na kilikuwa kinuke. Sasa bana ile hela hakuweza kunilipa hata nusu mi coz ni mshikaji ikabid niwe mpole. Bas maisha yakaendelea akaja kuacha kaz akajiendeleza nikaja kumkuta sehem niliyokuwa nimebanwa kupita maelezo. Halafu yeye ndie alikuwa bos wa pale daa. Aisee nilijifunza. Jamaa kumbe alikuja kurud akapata kaz nzur akanitafuta sana hakunipata ndio hivyo Mungu akatukutanisha. Mpaka leo ni family friend wangu.
 
Kwa sababu hatujui kesho tutakutana na nani basi fanya wema kwa yeyote bila kujali cheo chake, rangi, kabila na hata dini.

Imepita kama mwezi hivi Siku Moja niko maeneo flani natembea nikaiona simu aina ya sumsung pembezoni mwa njia ikiashiria kuwa imedondoshwa, simu ile ilikuwa mpya kabisa na nzuri hasaaa.

Nikaiokota nikaendelea na safari zangu ikapita kama nusu saa ikapigwa nikapokea, akaongea kaka mmoja kwa unyenyekevu sana akinisihi kwamba yeye ndiye aliyedondosha simu akiwa kwa boda boda hivyo ananiomba sana nimrudishie na atanipa kiasi flani cha pesa.

Basi moyo ukaanza kubishana nizime nitoe laini nitokomee au nimpe tu, dah shetani mbaya, roho wa Mungu akaniambia mpe, mabishano yakawa makali kati ya roho ya shetani na ile ya Mungu, mwisho wa siku nikaamua nisikilize la Mungu la kumpa simu mwenye simu.

Nikamwelekeza nilipo akaja nikampatia na kunipatia kiasi cha ela, dah nikakataa nikamwambia hana sababu ya kunilipa chochote kwani ile simu ni haki yake na mali yake, akanilazimisha sana nikagoma,.
Yule kaka hakuamini kama kuna binadamu anaweza okota sumsung akarudisha na akapewa hela akaikataa.

Basi juzi nikawa naenda mahali na nilikuwa nje ya muda so ili kuwahi ilinibidi nichukue boda, nikaongea na boda boda wa kwanza akasema huko nakoenda ni mbali na barabara ni mbaya na ni usiku so akanitajia bei kubwa sana, dah nikamshindwa akaja mwingine naye,hivyo hivyo

Wakati nawaza nifanyeje akaja yule niliyeokotaga simu yake kumbe kilikuwa ndo kijiwe chake na alishaniona na akanikumbuka akaja a kaniambia dada wewe si ndo uliokotaga simu yangu nikamwambia ndo mimi ujakosea, akasema twende dadangu, nikapanda akanipeleka bure akanisubiri akanirudisha hadi nyumbani bure kabisaaaa.

Jamani nilifurahi sana si kwa sababu nimepelekwa bure bali kwa sababu Mungu aliamua kunidhihirishia kuwa wema hauozi, nilifundishwa kwa matendo.

Nawewe msomaji wangu ebu tenda wema kuna siku tu Mungu atakulipa tena unaweza usijue wakati ukilipwa.

Epuka kutendea mtu mambo ya hiyani kuna machozi ya watu ambayo huwa hatari yanapodondoka.

Jioni. Njema
Ahsante kwa ushuhuda but kumbuka siyo kila kitu au mtu na kila mahali na muda unatakiwa kutenda wema. Kama huamini jaribu kumtendea wema shetani kisha uje hapa kutushuhudia!
 
Kwanini ulijiuliza mara mbilimbili kutenda wema? siku nyingine usifanye hivyo dada yangu, Allah akutengenezee mambo yako.
Sikuzote roho hushindana na mwili biblia inasema, mwili ulikuwa unaitamani sana mana mi binafsi sina Samsung nina tecno y3 ilovunjika kiooo teh teh, lakini roho huwa ina utakatifu kuliko mwili unaowaka tamaa

Dats y kulikuwa na huo mvutano
Ni wa kawaida kwa binadamu wote

Asante
 
Mimi bana niliwahi kukopa benk. Sasa yule aliyesimamia mkopo wangu alikuwa mshikaji sana tulielewana sana sasa cku moja niko karibu kumalizia mkopo jamaa akaja na bonge la shida na ckuwa vizur aisee. Ilibid nikakope nimpe ile hela. Nafikir kuna hela ilipelea kule ndan na kilikuwa kinuke. Sasa bana ile hela hakuweza kunilipa hata nusu mi coz ni mshikaji ikabid niwe mpole. Bas maisha yakaendelea akaja kuacha kaz akajiendeleza nikaja kumkuta sehem niliyokuwa nimebanwa kupita maelezo. Halafu yeye ndie alikuwa bos wa pale daa. Aisee nilijifunza. Jamaa kumbe alikuja kurud akapata kaz nzur akanitafuta sana hakunipata ndio hivyo Mungu akatukutanisha. Mpaka leo ni family friend wangu.
Waoooooo nzuri mnooooo
 
Ahsante kwa ushuhuda but kumbuka siyo kila kitu au mtu na kila mahali na muda unatakiwa kutenda wema. Kama huamini jaribu kumtendea wema shetani kisha uje hapa kutushuhudia!
Haha naelewa hili ndo mana tumepewa akili, ni. Ili mahala pa kuitumia tuitumie

Asante kukumbuka
 
Back
Top Bottom