Kuna habari za chini ya kapeti kwamba mwanadada Wema Sepetu amemwaga prince charming wake Idris.
Habari kutoka ghorofa ya pili nyumbani kwa Idris zinasema Wema hapokei simu za jamaa huku mnyange huyo akienda mbele zaidi na kufuta picha za jamaa huyo kwenye IG yake.
Idris na yeye anaingia kwenye orodha ya jamaa walioingia kwa Wema na kuonja utamu na kisha kupitiliza.
Tulipompigia simu Wema alikataa kuzungumzia suala hilo lakini pia alipoulizwa kipi atakimiss kutoka kwa Idris kama wataachana alisema
"Kwa kweli miguu ya Idris inaniacha nimepondeka kama nyanya kwa kweli naipenda sana hasa jinsi ilivyojikunja kwa chini,kwa kweli sijawahi kuwa na mtu mwenye miguu kama ya Idris"
Pia tulipotaka kujua kama amemalizana na Tanesco alikata simu na haikupatikana tena, mwandishi wetu anafuatilia suala hili kwa ukaribu ili kuwajuza nini kinaendela hasa ukizingatia tayari tumeishapandikiza vinasa sauti kwenye nyumba za maceleb hawa.
Wema Sepetu amefuta picha zote za Idriss kwenye akaunti yake ya Instagram, hii inaweza kua ni kiashiria kingine cha kuachana kwa wapenzi hawa.