Weka Neno kweye Hii Stori ya mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Weka Neno kweye Hii Stori ya mapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by paty, Mar 18, 2012.

 1. paty

  paty JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  kuna kijana ana mpenzi, wamekuwa pamoja kwa muda wa miaka 2 katika uhusiano usio rasmi kwa maana kuwa hakuna aliyejitambulisha nyumbani kwa mwenzie, kijana alipo pata kazi akaona umefika wakati wa kufanya mambo officially , akaone ni bora washirikishe wazazi wake juu ya mpenzi wake ili watoe baraka zako.

  filamu ikaanza

  kijana kamfuata baba kumueleza juu ya mwanamke wake, kijana alimweleza mzee wake kwa utulivu na baba alionyesha yupo makini na habari zile zilimfulaisha sana, baba mtu alizipokea kwa furaha habari hizi za kheri, ila baba akauliza je , mwanangu mwanamke unayetaka kumwoa unamjua vizuri??? je anaitwa nani? anakaa wapi? unaijua familia yake??

  kijana akaanza kuainisha wasifu kamili wa mpenzi wake ndipo baba ghafla akabadilika, kabla kijana hajamaliza kutoa wasifu baba akashika kichwa akasema "My God" , kwa mshangao kijana kauliza kuna nini?

  baba akamwambia mwanangu KUNA SIRI KUBWA sikuwa kukwambia,wala sijawai mwambia mama yako kwani naogoppa kuvunja Ndoa,
  Huyo binti mpenzi wako ni mtoto wangu kama wewe , nilizaa nje, na ilikuwa siri kwa maana kuwa mama yako sitaki ajua kwa sababu sitaki adai Talaka.

  UAMUZI WA BABA; ni kuwa huwezi muoa dada yako wa damu, nyote ni watoto wangu ila mama tofauti

  More confusions

  uamuzi wa baba na ukweli wa mambo ulikuwa mgumu sana kwa kijana, ghafla akabidilika mawazo muda wote na chakula hakiliki, mama kwa kuwa ni mtu wa karibu na watoto alikugundua mapema kuwa kijana wake yupo kwenye msongo mzito wa mawazo,
  kwa sauti ya upole na ushawishi mkuu, mama akamuuliza kijana wake " mwanangu tatizo nini" , kijana akasita kusema ukweli kwa kuofia KUVUNJA NDOA YA WAZAZI WAKE.

  siku zikapita kijana hajasema, mama akaendelea kushawishi na kuuliza mtoto wake kapatwa na nini

  Kijana anaamua kumwambia mama tatizo lililomsibu

  baada ya kukaa na dukuduku moyoni kijana alishindwa kuvumilia , akaona mama ni mtu pekee wa kumshirikisha huzuni ya moyo wake,
  kijana aliamua kumshirikisha mama yake kwa sharti kuwa chochote atakacho sikia awe mpole na asichukue uamuzi mbaya, Mama mtu akakubali, Kijana akafunguka juu hali halisi , akalia kwa kukosa mke ambaye kimsingi ni dada yake.

  Sikia ya MAMA nayo

  Baada ya kumsikiliza mwanae mama akamshika shavuni kijana wake na kumfuta machozi kisha aka mwambia " Kijana wangu, una weza kumwoa huyo mwanamkke unaempenda , wala usiumie moyo sana, "

  kijana akashangaa sana , je itawezekanaje yeye kumwoa dada yake??

  Siri nyingine

  mama akamwambia mwanangu kuna siri kubwa ambayo hakuna mtu anaijua, nliificha siri hii kulinda ndoa yangu na baba ako, ila leo naona bora nikushirikishe,
  wewe na huyo msichana wako sio ndugu wala hamjashare baba.
  huyu si baba yako, nlipata mimbba yako nje ya ndoa, nikaficha siri ilikurinda ndoa, Hivyo huyu si baba yako bali ni baba yake wa huyo demu wako.


  Kijana aliposikia ivyo tena mambo ndo yakawa magumu zaidi , kwanza kuupokea ukweli kuwa si baba yake na pili je ataanzaje kumwoa huyo dada ake, kwani baba bado hajajua ukweli kuwa libambikwa mimba, na baba akijua atachukuliaje?????

  WAKUUU WEKENI NENO
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  dah, mchina wangu kashindwa kusoma.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  huyo mama 'mapepe'
   
 4. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  old cr*p!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. G

  GENDAEKA Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba thao na mama thao!!
   
 6. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  Ni nyimbo ya peter tosh inaitwa pride and shame
   
 7. paty

  paty JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,259
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  yes......... a boy from trench town

  but it is very nice, rate and share, that is love rasta
   
Loading...