Weka 5M uvune faida ya 5M baada ya miezi 5

Vangigula

JF-Expert Member
Aug 13, 2015
814
2,543
Hii ni baada ya kufuatilia trend ya masoko kwa zaidi ya miaka minne mfululizo.

Ni hivi, kuna bonde moja liko kati ya wilaya za Mpwapwa na Kilosa, linaitwa Lumuma. Pale kwa sasa wameanza kuvuna kitunguu maji, na bei kwa gunia kwa sasa ni elfu hamsini (50,000) za kitanzania.

Kama ukinunua magunia 100, utawekeza 5M + maximum ya laki 2 kwa ajili ya storage. Then u nasubiri kwa miezi mitano, mpaka December, ambapo bei kwa gunia moja huwa imeshakaribia, au kufikia shilling laki moja.

(Kwa mwaka jana December 25, gunia lilishafikia 120,000/= kule kule shambani ). Ukivumilia mpaka gunia lifike 110,000/= utakuwa ume offset kiasi kidogo cha vitunguu kitakachopotea wakati umekitunza (kumbuka kitunguu hupoteza maji na kunywea kidogo kidogo kadiri unavyoendelea kukihifadhi ), na utakuwa na uhakika wa 5M kama faida.

Unaweza kununua zaidi ya 100 bags ambalo litakupa faida zaidi. Kwa uhakika wa bei, tembelea masoko yote wanayouza kitunguu, na uwaulize bei zake huwaje kuanzia December mpaka April.
Kizuri, kula na ndugu.
 
Mkuu ni red Bombay ndio kinaweza kukaa muda mrefu zaidi bila kuharibika pia kinapendwa sana sokoni
Nilidhani labda "Red Bombay" vina maji sana hivyo vinaharibika haraka, pengine "Khaki" ndio durable, shida yake Khaki ni vidogovidogo sana sababu ni vikavu vikavu hivi hivyo hadi ujaze gunia basi shughuli yake nzito. Huu ni mtazamo wangu tu
 
Nilidhani labda "Red Bombay" vina maji sana hivyo vinaharibika haraka, pengine "Khaki" ndio durable, shida yake Khaki ni vidogovidogo sana sababu ni vikavu vikavu hivi hivyo hadi ujaze gunia basi shughuli yake nzito. Huu ni mtazamo wangu tu

Ohoo! Unaweza kuwa sawa mkuu ngoja wajuzi wengine waje Ila kuna muuza mbegu mmoja aliniambia red Bombay ndio vina kaa muda mrefu pengine aliniingiza Chaka
 
Ohoo! Unaweza kuwa sawa mkuu ngoja wajuzi wengine waje Ila kuna muuza mbegu mmoja aliniambia red Bombay ndio vina kaa muda mrefu pengine aliniingiza Chaka
Inawezekana nawe uko sawa Mkuu,
Ila nimewaza ile Red Bombay naoijua ilivyo na maji mengi, sema kwenye kufanya vizuri sokoni ni kweli sababu hivi vinakuaga vikubwa vikubwa sababu vimejaa jaa (maji??)
 
Aina zote za Vitunguu zinafaa kwa storage Mkuu??
Ni fursa kweli, but let us be realistic Mkuu
Nimesema almost aina zote zinazolimwa TZ. Fanya utafiti wako binafsi ujiridhishe mkuu
 
Mimi nimeingia shambani mwenyewe with less capital navuna december
1469551725715.jpg
 
Ni
Biashara kama hizi hazitatabiriki mkuu[/QUOTENi
Biashara kama hizi hazitatabiriki mkuu
Ni kweli kabisa, hakuna biashara utakayotabiri kwa 100% certainty. Ila wanaoweza kuchukua calculated risks mara nyingi ndio hutusua. Besides, nimetoa na majina ya sehemu ili wanaoweza wakajifanyie uchunguzi zaidi, na wakishajiridhisha wafanye maamuzi. Karibu
 
Back
Top Bottom