Tukumbushane kwanza. Trump alianza kupaa kisiasa mwaka 2011 alipong'ang'ania kwamba Obama si mzaliwa wa Marekani na kwa hivyo hastahili kuwa raisi. Alitoka hadharani akidai Obama aoneshe vyeti vyake. Hakuna raisi yeyote aliyepata kudaiwa cheti cha kuzaliwa baada ya jamaa wa usalama kufanya kazi yao. In fact, mpinzani wake wa 2008 labda ndiyo angeweza kudaiwa hastahili maana alizaliwa Panama. Nilikuwa Marekani wakati Obama alipotoa cheti chake hadharani. Wakati huo Trump alikuwa safarini, alipotua tu airport waandishi wakamletea copy ya cheti cha Obama. I kid you not, alikataa kukiangalia pale na kusema "it doesn't matter." Bado aliendelea kudai kwamba Obama na familia yake walifoji vyeti vyake mpaka 2016.
Dear mwanza uzi, this story is extremely important if you want to understand Trump's rise. Wale wazungu wabaguzi wote na wengine wakiwa nyuma kwenye vivuli vya dini walimwona Trump kwamba ni shujaa ambaye ni pekee anaweza ku-confirm their beliefs. Watu wananukuu mpaka misahafu kuhalalisha uovu. Suala ni kwamba wanaona kwamba nchi hiyo ni ya wazungu, na watu wengine wote wanaonekana kuwanyang'anya. Wamewasahau hata watu wa asili waliowaua kwa mamilioni. Na Obama alikuwa kama ishara ya kunyang'anywa mamlaka yao. Ukiweza kusema sio mzaliwa wa Marekani, you in effect delegitimize him and everything he has done.
Siku hizi kuna fake news outlets nyingi sana duniani. Na muanza uzi huu umepata kutekwa na upuuzi unaotolewa huko. Kwa mfano, ati Obama aliwatuma watu wafanye vurugu. Sijui kama unaelewa harakati za watu huko Marekani ambapo watu weusi au people of color have to struggle to get their rights. Wanalaumiwa kwa maandamano tena kwa kutumiwa riot polisi wakati vijana wa kizungu hufanya vurugu mbaya kuliko hizo kwa sababu kama timu yao kufungwa. Lakini hutasikia vyombo vya habari vikisema lolote.
Usiambukizwe chuki zisizokuhusu kwa sababu ya fake news. Trump anapovuruga bima ya afya au sera za Obama si kwa kuwasaidia wananchi wake. Trump anapong'ang'ania atavunja makubaliano na Iran si kwa kutafuta amani hata kidogo. Anapomwaga uwongo kila siku si kwa maslahi ya Wamarekani walio wengi. Anapodai New York Times ni fake news, unamtaraji hatakwenda kwao tena kwa interview. Something is terribly wrong.
Umemsikia mara nyingi akidai kwamba Waislamu ndiyo adui mkuu wa usalama huko Marekani. Niambie kama umepata kusikia mauaji mangapi ya halaiki huko Marekani. Angalia tu, mwingine kaua karibu watu 60 majuzi tu. La, si Waislamu hiyo ni kile wenyewe wanaita dangling red meat. Wauaji wakuu huko ni wazungu wanaume.
Tafadhali soma orodha ya uwongo unaomwagika kutoka mdomoni mwa Trump hapa.
President Trump’s Lies, the Definitive List
Nina mashaka sana na mwanzilishi wa uzi huu na wote wanaomuunga mkono Trump hapa Tanzania kama kweli wenyewe wanafuatilia vizuri na kuelewa kinachosemwa na Trump. Nasema hivyo kwa sababu kama ni kujieleza hata wafuasi wake wa karibu kabisa hawawezi kumtetea kwamba anaeleza kitu kwa ufasaha wowote. Mawazo yake ni ya kujichanganya. Sentensi zake hazina mtiririko. Msamiati wake mdogo kama vile hajasoma: tremendous ni kila kitu kwake. Na kama ndivyo basi, anayemtetea kwamba anasema vizuri atakuwa hajui Kiingereza. Prove me wrong. Pia niseme hapa duniani nchi pekee ambapo kuna watu wengi wanaomsapoti Trump ni Tanzania na Urusi (its a deliberate hyperbole I am making). I wonder why Tanzania.
Umetumia nguvu nyingi kuonyesha Trump ni mbaguzi kwa sababu ya kupinga cheti cha Obama. Trump na Obama wana bifu za binafsi. Ukiniuliza nitakuambia Trump alishafikiria kugombea urais huko nyuma lakini alifanya kweli 2016 baada ya dhihaka za Obama kwa Trump
Mimi nimekupa mifano miwili hai. Trump kamchagua Ben Carson uwaziri ili awasaidie watu weusi na hakuficha hicho kitu. Pili Trump keshapeleka polisi wapya mia moja Chicago na wanaweza kuongezwa hadi elfu na ikibidi Trump kaahidi kupeleka jeshi kukomesha mauaji ya watu weusi ya wenyewe kwa wenyewe Chicago.
Baltimore watu weusi walifanya fujo za kupigana na Polisi sikusema wametumwa na Obama nimehoji kwanini hakuna aliyesema wametumwa na Obama wakati wazungu wa Charlottesville analaumiwa Trump kawatuma wafanye fujo.
Mkataba na Iran ni bomu. Huwezi kuwaamini Iran. Alichofanya Obama ni sawa na kufanya urafiki na toto gomvi shule ili kuepuka kupigana nalo.
Trump hajasema waislamu ni maadui wa Marekani hata siku moja. Trump ana hoteli na Dubai na kapiga picha na matajiri wa kiarabu. Trump anapinga radical Islam. Waislamu wenye siasa kali. Hata mimi nawapinga. Na ndio moja ya sababu nilimpigia kura Trump. Kwanza hakuna kitu kinachoitwa waislamu wenye siasa kali. Wale ni wapotoshaji na wavurugaji wa dini kwa manufaa yao ya kidunia. Hasa kwenye suala la kumiliki nchi na mafuta.
Hata mtu aue watu milioni mbili kama hatahusisha dini yake na mauaji hayo, dini yake haitalaumiwa. Hawa wapumbavu wanauwa watoto wadogo, wazee na watu wasio na hatia. Hakuna kisasi cha kuuwa raia wasio na hatia katika uislamu. Wanalipua ndege, misikiti, makanisa, viwanja vya mipira na airport. Wanalipua matreni, wanatuma watoto wadogo wajilipue mabomu. Wanakamata watu kwa utaifa wao na kuwachinja kama kuku. Na wanafanya yote hayo kwa jina la Mungu. Shenzi type, acha Mungu hat shetani hawezi kuleta dini ya kishenzi hivyo.
Hiyo taarifa ya uongo wa Trump umeihakiki vipi. Waambie na wao waorodheshe uongo wao waliomsingizia Trump.
Eti Trump hawezi kujieleza. Kwenye kampeni ya chama chake walikuwa 16 kawashinda wote na akakishinda kile kibibi kiongo Hillary.
Ulisikia hotuba ya Trump alipowafuata waarabu kwao akawapa vidonge vyao. Yaani ilinikumbusha Nyerere alivyokuwa akienda Zanzibar kukomesha vurugu za wapemba.
Umesikia hotuba yake ya UN. Hata wapinzani wake wa fake news walishika kichwa.
Trump hakopeshi anasema vitu kama vilivyo. Ni uwezo wake mkubwa wa kujieleza ndio uliomfanya ashinde uchaguzi.
Aliahidii kujenga ukuta kuzuia wahamiaji haramu.
Aliahidi kurudisha viwanda vya Marekani nyumbani na kuviondoa Mexico na Asia.
Aliahidi kuvunja Obamacare na kuleta bima bora kwa wamarekani. Obamcare ilikuwa na mapungufu mengi ikiwemo kuwapandishia malipo ya bima wasiotumia bima hiyo nikiwemo mimi.
Aliahidi kuwashinda ISIS
Aliahidi kufuta mikataba mibovu ya kibiashara.
Aliahidi kusafisha na kuleta mabadiliko serikalini.
Aliahidi kuwapunguzia kodi wafanyabiashara wadogo.
Aliahidi kazi nyingi kwa wamarekani zikiwemo za kwenye migodi.
Aliahidi kukomesha wakimbizi hasa wa kutoka nchi zenye vita na Marekani. Ni akili gani kuvunjia watu miji yao halafu kuwachukua nchini kwako kama wakimbizi. Unafikiri wanakuja kwa heri?
Aliahiadi haki na usawa kwa wamarekani wote. Akasema binadamu wote wana damu ya rangi moja.
Alitoa ahadi nyingi na akizifanikisha atakuwa rais bora kuliko marais wote waliopita Marekani. Ndio sababu wanampiga vita. Na wanampiga vita kwa sababu hakubembeleza mtu. Na kwenye kampeni alitukana tukana wapinzanj wake na vyombo vya habari. Hawa CNN keshawafukuza sana kwenye mikutano yake.
Huyo ndio Trump. Una hoja au shauri?