Weekend Story: YANGA! (Naipenda yanga shabiki wa damu)

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11

Wazima nyieee, sio kwamba jpili nili wachomesha mahindi makusudii ni kwamba kama gundu tu, ki laptop chaliiiiii! Mungu si athumani nimepata kipalm top ndo tutaenda nacho mdogo mdogo.

Story ya leo ni ngumuuu, kama kawaidaaa, sirudiii, si copy, nakuja kivingine kabisaaaa! Hii ya leo ya maisha yetu yale ya watu wa chiniii. (Mshaanza oohh Lara wa kishuaa, mbona story zote Masakiii, mngejuaa jirani yenu tandale ya migo migo kwa popo bawa pale unaingia kulia, sasa leo hakuna Masaki, Mikocheni wala Mbezi beach! Na utamu ule ule. ) Mashabiki wa Simba, nayo Simba imooo, tuseme 50 Yanga, 50 Simbaa. Hahahaaaa!

STAY TUNED SAA 4 KAMILI.

YANGA! NAIPENDA YANGA MSHABIKI WA DAMU!


OCTOBER 20, 1990
Huyu Khalidi yuko wapi jamaniiiii, mme muona wapi khalidi? Mke wake kajifunguaaa, haonekani hapa, na tulikwa nae hapa sasa hivi. Sasa itakuwaje, tunashindwa hata kusherekea maana baba mtu hajatia suna, mambo ya kheri, tumepata mwali, tumepata mingombeee! Aiiiiiiiiiiiiii! Mungu mkubwaaa! Hongera sanaaa, Ashukuriwe Mungu maana nkewe aliitwa ngumbaa, mtaa mzimaaa.

Hmajamuona Halidi hukoooo? Sisi twataka afanye hio suna tutoke hapa atii, yeye haonekani sijui kenda wapi. Mjue nini wazee wenzangu Halidi mwanangu namjua fikaaa, atakuwa jirani na hapa asikiza mpiraa, si leo wanacheza Simba na Yanga? Ngoja nikamvizie nitamfumaa tu huko njeee. Issa na wewe ufanye hima sio wafika huko wafanya kuusikiza huo mpira na wewe wakaa kitako kabisaa. Mzazi kachoka huyuuuu.

Issa akawa katoka nje akakuta kuna Mkulima redio wamejaa watu wanasikizaaaa, alivokaribia akasikiaaaa. "Yanga wanashambulia goli la Simba pale, Thomas kipese anampasia mpiraaaa Sanifu Lazaro paleeee, matata sanaaa huyu Sanifu Lazaro, anapiga chenga ya kwanza, anapiga chenga ya pili anamtoka Mohamed mlinzi wa Simba huyu,, anamkaribia kipa paleeeeee, Goaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaal! Yanga wanapata bao la 3 ndungu wasikilizaji hamuwezi kuaminiiii, dakika ya 89, Yanga wanapata bao la nyongezaa, bao la 3, Yanga 3, Simba moja lilifungwa na Edward Chumilaaa hapo dakika 58, akizawazisha goli la kwanza la hawa Dar Young Africans mnamo dakika ya 33 la Makumbi Juma huyuuu ndo alianza kuzifumania nyavu za watani wa jadi. Mpira unaanza tena pale kati, Refa anasema mda umekwisha anatoa dakika 3 za niongeza, bado Yanga 3, Simba 1. Wanacheza pale, anapiga kushoto kuleee kumtafuta winga wa Simbaaa, anakosa anaudaka Yanga pale, wanapasiana Yanga kupoteza mda tu, maana ushindi mnono wa 3 kwa 1! Refa anapuliza kipenga pale Mpira umekwishaaaaaaaaaaaa! Yanga 3 Simba 1. Eeeeeeeeeeeeeeeeeh! Woooooooooh! Kwako studio! Hii ni redio Tanzania ikikutangazia moja kwa moja toka uwanja wa Karume ..........."

Sheikh Issa tumeshindaaaa, watoto wa Jangwaniii juuuuuuuuu, eeeeeeh! Balaaaaa hiliii! Nina raha ajabu. Wakashangilia kitambo tu, ghafla Issa akakumbuka aliagizwa. Halidi mkeo kajifungua unaitwa kule! Eeeeeeh! wasemaje Issa? Mkeo kajifungua salama mtoto wa kike, unaitwa ukatie suna tuondokee. Eeeeeeeeeeeeeh! Nina raha juu ya rahaaa! Nishajua nitampa jina gani. Utampa jina gani Halidi mwanangu vijana mna tabu sanaa na majina yenu ya kileo. Nitamwita Yanga sheikh Issa! Hhahahaaaaaaa! Halidi una fujo sanaa, Yanga sio jina la mtoto wa kike, atakosa wachumba wa Simba usimzibie mtoto Riziki.

Mtoto wa kike hana timu, mwanamke timu ya mumewe ndo timu yake, dini yenyewe yasema hivooo. Hahahahaaa! Wakacheka na Halidi. Kufika kule watu wakasema bila shaka wote mlikuwa mwasikiliza mpiraaa? Fanyeni kumpakia huyu mzazi kwenye baiskeli akapumzikee. Halidi umemuona mwanao? Mzuriii, kafanana na mama yake. Halidi akambeba mtoto, Aaah Yanga mwanangu! Mama ake Khalidi akasikia. Majina ya ajabu ajabu kwa mjukuu wangu sitakiiii, mpira wenu huko huko, sitaki kabisaaa, msinipime Imani, huyu mtoto ataitwa Khadija kama mimi bibi yake, na mke wa kwanza wa Mtume. Halidi akasema sawa mama, ila nyumbani ataitwa Yanga. Watu wakachekaaaa! Bi Khadija akamkata jichoo, eti mzaa chema mtoto aitwe Yanga? wakamuuliza mke wa Halidi. Mke wa Halidi akajikaza kusema ataitwa Evelyne, jina la mama yangu. Ukimya ukapitaaaaa, maustaadh wakaangaliana, na kupeana ishara mbona jina la Kikafiri tenaaa. Waka kaa kimya wote.

Akajikusanya sheikh Issa, unajua Rhoda sasa wewe na Khalid kijana wetu ni wazazi, inatakiwa mfunge ndoa, japo wadogo kiumri ila mshaamua kuzaaa, wenyewe mmependana, mkaamua kuzaa, sisi tumekuja kujua mimba tu, tutakuoa kwenu vizuri tu kama dini yetu dini ya Mtume, dini ya Kiislamu inavoagizaa, tutachoma ubani, tutalipa mahari zotee, na tutapata idhini ya wazee wako, ingekuwa tushafanya hivo ila sema tu ulikuwa mjamzito na dini hairuhusu kufanya ndoa na mjamzito sababu Mtume kakataza kumwaga mbegu juu ya mbegu nyingineee, hata huyu mtoto ni wa zinaa, sababu mtoto wa kike wala Halidi hatoweza kutoa idhini ya kumuozesha, ama kumrithisha mali ila wewe mama yake atakurithi, na wewe utamrithi mtoto wako.

Ni makosa yashafanyika, kama wazee wa Halidi tumekwazikaa, tumesononekaa ila mwisho tumerudi kwenye dini inatutaka kusameheana, na kupendana, tupo tayari kurekebisha mambo, ndoa ya wazinifu ina juzuhuu, utaslimu mama, tutakuozesha kwa halidi, kama mlivopendana, ila tunaomba mama ufanye uugwana kama tulivofanya sisi wazee wako, tumekupokea vizurii, maadamu utaishi kwetu basi huyu mtoto umpe jina la mama yake Halidi, Khadija, itatupendeza mnoo, sawa mama yangu? Rhoda akaitikia sawa, manake atafanyaje.

OCTOBER 30!
Ngongoooo, ngongoooo, ngooooo! Wenyewe mpoooo? Tupo Bi Khadija pita ndaniii. Hata sikai mtu mzima mwenzangu njoo tutete kidogoo. Nakusikiza mtu mzima mwenzangu. Mwenzanguuu mwali wangu yule mkwe wa Halidi hakai vizuriii, hatembei vizuri siku ya 10 leo. Sasa sijui nifanyaje? Manake mimi hapa Magomeni nasifika kwa kukanda maji ya uzazi ila pale nimenawaaa. Au sijui huruma imenizdiii, nampozea maji sanaa, mdogoooo, miaka 16, nikimuangalia naingiwa imani, nikifikiria katoka kwao mama yake mwalimu wana jiwezaa kaja maisha ya huku naona anajikazaaa tu sasa nyuzi zishaanza kutoa wadudu sijui nifanyaje.? Mtoto wa watu yule najutaaa. Sikia bi Khadija kuanzia kesho nakuja kumkanda mimi mwenyeweee, sicheki na kimaa, hizo nyuzi pengine macho ya watu pia sio mazuri, fanya twende Yombo kwa yule Ustaadh atuandikie makombe tuje tumnyweshee na kumuogeshea, mambo yatakaa vizurii, utaniambiaa, Ustaadh hakosei yule. Sawa basi kesho uje umkande wewe, Halidi kajua kweli kumuharibia maisha binti wa watu form 1 yupo maskini, shule basi tenaaa.

Kesho yake yule bibi akaja, bi Khadija anajikosha kosha, Roda mwanangu naumwa mgongo kweli, leo atakukanda Bi Zaina hapa, jikaze mwali wangu ndo ukubwa huo. Roda akaitikia tu kwa unyonge sawa mama. Bi Khadija akabana mlangoni asikilizie mtiti huko! Akasikia Haaaaaaaaaaa! Whaaaaaaaaaaa! Nakufaaaaaaaaaaaa! Mama yangu wewe. Ananiuaaaaaa! Bi Khadija akadakia nije bi Zainaaa? Akasikia Usijeeeeeeeeeeeee! Sitaki kuona mtu huku kazi ishakushinda hiii. Basi kaka pale mlangoni anaranda randa hakuna anachokifanya. Zikaanza Mama Nakufaaaaaaaaa! Halidi ndukiiii mpaka bafuni! Vipi jamani, mke wangu inakuaje hukooo! Bi Zaina akamwambia mwana ukomeeeeeee, tena ukomaeee nitakususia mkeo aozeee. Halidi akawa mpole, basi taratibu Bi Zaina, mke wangu bado mdhaifuuuu! Tokaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Angekuwa mazaifuuu angeukatikia mpaka mkazaaa. Alivo ukalia tu kashakua mkubwaaa, tokaa tena usinitibue nikakupa maneno ya kadhiaaaa. Halidi akaondoka anageuka nyuma nyuma. Kelele zikaendelea.

Wakatoka Roda anayumba yumba, anajisotaaa! Akasikia tembea vizuriiiii, sitaki ujisoteee, kwanini unajiendekezaa? Ukijisontaa nakuongezea maji ya moto kesho, Ukikaa upande maji tu ya moto. Unavonipa moyo unapona ndo nakupunguzia moto. Haya kunywaa! Roda akaulizaa, nini hiki mbona kama kina mandishi ya kiarabu? Bi Khadija akadakia dawa hio mwali wangu, we kunywa. Roda akasitaaa. Bi Zaina akamchokaa, akambwatukia kunywaaaaaaaaa, sio kuuliza uliza nini, mbona shahawa hukuuliza hiki nini ulizinawa za kutosha. Kwa woga Roda akanywa gubu gubuuuuuuu, akashusha kikombe kitupu huku Bi Zaina na Khadija wananenaaa. Mbele ya bi Zaina Roda akapata nafuu fasta fasta, wakaenda kutoa nyuzi (1990S Nyuzi za kupotea mwilini bado kabisaaa hata kunukia bongo) Akawa kapona kabisaa, anakaa vizuri na kutembea vizuri, Ikafika 40 ya mtoto.

Wakafanya Aqiqa au Aqueeqa kibongo bongo Akika. Miasha magumu ila bibi mtu akauza mazao yake ikapatikana hela ya Kondoo kwa shughuli hio. Wakaalika watu wa jirani, basi shughuli ikafanyika. Sasa wakaja mama na wadogo zake Rhoda, Bi Khadija akawapakulia chakula, mama Rhoda akawaambia msile hiki chakula tofauti na dini yetu. Roda akmwambia mama mbona mimi nimekula hakijanidhuru, Bi Khadija kahangaika kufanya shughuli hiii sanaa msipo kula atajisikia vibayaa, Bi Khadija akasema kama hawali haina neno, nitaenda kuwaombea wali kw bi Zaina, ujue dini muhimu hata sie ingekuwa shunguli yenu mngepiga nguruwe sie tusingekulaa. Mama Rhoda akamwambia usihangaike mzazi mwenzangu washakula wote hawa.

Baada mama mtu anambana Rhoda, sasa fanya urudi uje uendelee na shule, mtoto waachie, kama hutaki nipe mie nikuleleee ila shule muhimu. Halidi atakupa nini? Ndo maisha gani hayaaa? Mimi nimekusamehe na sitokukatia tamaa sababu nimekuzaa, unaninyanyasa sanaa mzazi wako kunivua nguo mji mzima, nadanganya uko Nairobi secondary. Anyway rudi nyumbani uende shule. Rhoda akamkatisha, mama kina Halidi wanataka walete posa! Mama Rhoda akapiga nini? Rodha akarudia wanataka walete mshenga! " Mxiuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! kweli hapo kwako Roda nilitoa tu uchafu tumboni, yaani nikajua umejitafakari, umejutia nafsi yako, umejifunza, na umekomaa ndo kwanza unapata sifaaaaa! Mwana hizaya mkubwa wewe" "Mama mimi na halidi tunapendana sanaa" "Atakupa nini Halidi hajaenda shulee, familia yao ndo hii hovyo hovyoooo! Ukijisikia siku au ukijitambua rudi nyumbani" Wakaendela na sherehe bila kusemeshanaaaa. Mtoto akapewa jina la Khadija na mjomba muislamu waliemuomba sababu mama mtu alisha slimu ila familia yake ndo bado, mjomba ndo alichinja kondoo yule na kufanya ibada yote kwa niaba ya upande wa mwanamke sababu ndoa bado na yule mtoto wa nje ya ndoa, mjomba alivomaliza tu hakushiriki akaondoka kimya kimyaaa kama dini inavoelekeza.

Jioni Halidi anamwambia Rhoda, hii 40 nilikuwa naiona mbali, kicheki mlivofananaaa. Yanga wangu huyooo! Rhoda yupo acha mambo yako, anaitwa Khadija. Wakawa wanachekaa, wanapendanaa hatariii. Halidi akamwambia nimepata mshenga, nataka aende kwenu kukuposa, sasa mama atasumbua sanaa, ndo maana nimemwambia aongee na mjomba wako, huende akamshawishi binamu yake akubali posa tufunge ndoa. Rhoda akamwambia tuombe heriiii.

Halidi akapata kazi ya kibarua cha kupaka rangi, ni fundi rangi wa kujifunza funza huyu, akawa anatoka majogooo anarudi machweoo. Bi Khadija pekupeku zake akamuuliza Rhoda ulikutana wapi na Halidi hadi mkaamua mzae?

Rhoda akasema mpirani, timu yetu ilikuwa inacheza na timu ya shule jirani, sasa mimi ndo nikawa mshangiliaji mkuuu. Kumbe Halidi ananitazama tu, alikuja na washkaji zake kucheki mechi. Basi tulivotoka mpirani njiani rafiki yangu ni mtu wa boss wake Halidi, Kuongozana Halidi akanisifia najua kushangilia so twende wote mechi ya yanga, nikamshangilie yanga wakishinda. Na shoga angu na boss wa Halidi wakakubali twende twende. Kosaaaa! Mei 21 nakumbuka 1989 matokeo yalikuwa bila bila Yanga 0 Simba 0.

Baadae baada ya mechi Halidi akawa down sanaa, nikawa namliwazaa. Akanishawishi tufanye mchezo mbaya, nikakubali sababu alikuwa na huzuni sanaa na hayo matokeo. Nilikuwa sijui chochote na mama alinikataza sanaa. Na nilimpenda Halidi. Basi ikawa ndo mtu wangu tena, jioni yupo mkiani, tunafanya fanya mpaka nikabeba, akipata hela mara cinema, mara disco, mara party kila siku shule ishanishinda kabla hata ya huyu mtot, mimba ile shule wakanitimua rasmi, ndo tupo hapa tunaongea. Laiti Yanga wangeshinda siku hio ningekuwa darasani sahizi! Hahahahaaa! Wakacheka na bi Khadija. Bi Khadija akamuona Roda bado mtoto tu.

Ikaja taarifa Posa waliotuma kwa kina Rhoda IMEKATALIWAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!

Itaendelea Kesho saa 4 ASUBUHI kama kawaida.
 
Mwe saa nne nshalala jamani......ila nitaisoma asubuh......

Karibu tena .......
 
Igweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!11

Wazima nyieee, sio kwamba jpili nili wachomesha mahindi makusudii ni kwamba kama gundu tu, ki laptop chaliiiiii! Mungu si athumani nimepata kipalm top ndo tutaenda nacho mdogo mdogo.

Story ya leo ni ngumuuu, kama kawaidaaa, sirudiii, si copy, nakuja kivingine kabisaaaa! Hii ya leo ya maisha yetu yale ya watu wa chiniii. (Mshaanza oohh Lara wa kishuaa, mbona story zote Masakiii, mngejuaa jirani yenu tandale ya migo migo kwa popo bawa pale unaingia kulia, sasa leo hakuna Masaki, Mikocheni wala Mbezi beach! Na utamu ule ule. ) Mashabiki wa Simba, nayo Simba imooo, tuseme 50 Yanga, 50 Simbaa. Hahahaaaa!

STAY TUNED SAA 4 KAMILI.
Kumbe ndio maana una akili....Yanga vichwa sana....malizia basi Yanga halafu kule mbele Man Utd
 
lara 1,

You can make money kwa stori zako....here is the simple idea Unaanzisha Cafe inaitwa
"Today Story Cafe"

Moja watu wanaweza kuja kusikiliza story zako....


Mbili sometimes unawapa watu nafasi kuongea story zao za mapenzi kwa wasiotaka kuonekana wanaweza vaa mask...wakasimulia stori zao na wakapata ushauri....



Its good Idea if you seat down and develop the idea...watu wanaumia wengine wanatafuta sehemu ya kuongea, kushare story zao kwa mafunzo na wengine kupata ushauri.....


Kiingilio unaweka elfu tano tuu kila weekend watu wanakuja utasaidia ata tuwe na muvi za kibongo za uhalisia...

This is what I have 4 u
 
Hapa story tu ushabiki wa simba na yanga tupa kule...... Story hutuleta pamoja kama lile tangazo flani ivi hawara alijikuta anaibuka mafichoni na kumkumbatia mwenye mke baada ya goli kufungwa ha haaaa......
 
Hahaha hivi WanaSimba ndo hampo, au mnaogopa kunyimwa story. Wanatuonea hukuuuuuuu........
 
Back
Top Bottom