Weekend story! BEN 10

Weekend story! BEN 10

Kyle wa Ghost, jamaa na umalaya wote alonao anabambikiwa watoto. Itakuwa hazalishi
 
Maisha ya gerezani hayakunipenda hata kidogo. Afya yangu ilikuwa high maintanance. Mwili ushazoea protins zake expensive, vita!ins, nutrients, ngozi ishazoea treatments expensive kama laser, akili yenyewe ishazoea mambo tofauti. Nilinyauka nikawa kama mbibi.
Mwanzo ilikuwa all funs and games. Ukifanya sheria mda mrefu matokeo yake unaichukulia poa. Niliichukulia poa sheria nikaona mianya mingi. Japo hujuma nazo niliziona.
Jela unakutana na watu wengi sana ukizoea. Siokubaya kama mnavodhania. Nimekutana na wabeba unga huku, wafanyakazi wa ma bank, wezi wa maofisini. Na watu wa kitaa pia wapo.
Once i stopped being bitter na kuanza kuwa mwanasheria wao wa bure kwa wale wasiokuwa na wanasheria, i became popular. Nikaanza kupata chakula bora, lotion, nutrients zangu, cream zangu. Mimi tena lawyer wa nyampara wote. Everybody needed legal help and they had to pay up!
Nikaweza kumiliki simu 24/7 kila maoaha yanahitaji vibali vyake, na mimi nilifanikiwa kupata kibali cha jela. Roomate wangu alikuwa anaitwa Cookie kwa jina la huku. Nae alikuwa na kesi ya mauaji pia. Alimpiga shoka mumewe baada ya kugundua anambaka mwanae cookie aliezaa na baba mwingine. Kesi haikukaa vibaya sanaa. Japo ilikuwa first degree murder. Bado kulikuwa na matumaini. Mimi niliikutia hatua za mwisho.
Siku mimi natoka mahakamani na Sam na kuona ishu imenikalia vibaya ila nilijua nitamkomeshea sam wapiyule nguchiro. Napewa taarifa hukumu ya Cookie imetoka leo na kahukumiwa kunyongwa! Nilisikitika sanaaa! Sanaaa! Nikaona kama maisha yamemdhulumu vile. Mtoto kabakwa, mama ananyongwa! It was just not fair. Iliniuma wiki nzima. Nikawaza bonti yake ataishijena je wanae wataishije? Baba kambaka dada, mama kamuua na shoka, mama kanyongwa!
Ikabidi niwasiliane na ofisini kwangu wa appeal! Maana Cookie ashahamishwa gereza. Na mimi kwa ndani siwezi kumsaidia chochote. Na pia nikaona kweli sheria mda mwingine inakuwa kipofuuu na mimi naweza kunyongwa kimasihara masihara. Nikazidi kuogopaaa sanaaa.
Ikabidi nimtafute Mozah akayajenge na Sam! Najua Sam ana tamaa sanaa. Na bar ile ndo roho yake. Moza akasema bisi pe 100. Mimi nikaamua kumpa 100. Pesa zinatafutwa ila uhai ndo mara moja. Hakukubali! Akasema tu the minute mimi nikifungwa bar itakuwa yake automatically. Na inavoonesha nitafungwa mda mrefu sanaa which was also true.
Yule mwanamke akawa ananijiaaa badae anapoteaaa. Sijaju ni nani. Jela mle kuna waganga pia, wanapiga ramli. Unaagiza zana zako ambazo ni nazi, kitambaa chekundu, ungo, kuku wa sadaka. Wanakupigia ramli unayotaka. Kuna mmoja ana tv ya asili pia. Nilianza na ramli. Nikamwambia kuna tukio nililiona ila sura ya yule mtu imenipotea kila nikijaribu kuiletaaa ina goma! Pia nataka kumuona mtu alienipiga usogo siku ya tukio langu. Akafanya manyanga yake paleee akaniambianamuona mtu, mweusi, mwenye mwili, mrefu, mule mule kwenye kivuli changu. Akanieleza swala la kisrusha sanaa kwamba ni mtu mmoja. Sikuamini sanaa ila nilistukaaa.
Nikaamua nikamtazame kwenye Tv ya asili ni nani na je majibu ni yale yale. Nimeleta zana na kila kitu, akafanya manyanga paleee, ikaja picha ila iko blurred huoni sura kama kichwani mwangu. Nae akasema ni mtu mmoja kweli. Ila bado sikuwa nimemjua Nikakata tamaa. Kuna mtu anapagawaga na pepo nikamfata anipandishie majini yake yanambie ni nani. Nikamlipa ofcourse jela hata mapepo mtaji. Tena mkubwa. Yanatumika sanaa kutabiri matokeo ya mahakamani kesho. Pepo wakasema ni shoga ako wa damu. Anatembea na bwana wako, na ni mtu mmoja ndio yale yale nayojuaaa. Nikakata tamaa kabisaa.
Akaja mlokole akaniambia wewe mkristo kwanini unatumia huduma za pepo. Nikamwmabia a hatua nilipo natumia hata za shetani lenyewe. Akaniambia njoo kwa Yesukuna majibu yalio nyooka. Akaniambia unataka kuona nini? Nikamwambia siku ya tukio langu ku a mtu alinipiga nataka kumuona huyo. Pia nilifumania nataka kumuona na yule aliekuwa na bwana wangu.
Akaniambia huku hamna njia direct ila ipo. Toa sadaka kubwa sanaa. Usinipe mimi,toa hata kwa wagonjwa humu mahututi ikipokelewa mbinguni utaoneshwa. Sikuamini sanaa, ila nikajianda kutoa hiosadaka kubwa. Aliniambia nistoe mpaka nimwambie tufanye yetu.
Nikamwambia hii sadaka ni expensive, mionzi imeisha ocean road nawaagizia India wagonjwa wa hapa jela mionzi ya mwaka mzima. Nishaongea na Dr. Magereza hapo kaniambia hairuhusiwi ilahatuwezikuwaacha wenzetu wafe. Akanipaprocedure tufanye magereza wamepata mfadhili ifikishwe ocean road wakachomwe. Na ni zaidi ya milkion 167! Sio sadaka ya kitoto yaani salama yakobora nione na nione picha in HD, High Definition.
Akasema hivo ni vya Mungu kukupa si juu yake. Akafunga siku 3, siku ya 4 akanipandisha kwenye madhabahu yake huko chumbani kwake, akaniombea sanaa na kumsihi Mungu anisikilizena kama sina usafi wowote basi asikilize sadaka nayowatolea viumbe wake wanaojaribiwa na dunia. Aliomba sanaa mpaka akalia. Alinena kwa lugha zote. Nikafanya huomuamala kwa internent banking mionzi ikaja. Rank yangu ikapanda sana jela. Sanaa. Nikawa naheshimika mpaka na maaskari. Sipangiwi kazi.
Mkuu wa magereza akanihamishia VIP kwa kina Kyle. Ananiuliza napenda kukaa na nani. Ofcourse lazima nikae na Kyle. Akashangaa sanaa! Maisha yamegeuka mimi star wa jela zaidi yake. Mpaka naitwa kupiga storyna mkuu wa gereza. Chumba chetukama hoteli! Tu atoa oda tutakula nini kwa hisani yangu lakini. Guenda ile sadaka sikufanikiwa kuona nilichotaka ila ilinibadilishia maisha.
Kesi yangu ishasogea sanaaa, Bikamfukuza lawyer wangu wa kampuni yangu na kumuajiri lawyer wa Kyle,maana hata pepo zishaanza kusema Kyle ataachiwa huru. Ila bado mambo yalinikalia vibaya sanaaa!
Kyle alikuwa kaokoka, na ombi lakelilikuwa asijifungulie jela. Mimba ishapita miezi 9 akaambiwa awekewe uchungu akagoma mpaka hukumu yake ipite. Na hukumu yake ilikuwa siku 3 zijazo. Nilimuombea atoke,ila pia nilizidi kuogopa kubakia mwenywe maana bishamzoea kwa company.
Hukumu ya Kyle ilisomwa na siku hiosiku nzima naharishaaa. Moja haikaimbili haisimami. Mchana mkuu wa gereza akaja kunambia Linda, mshkaji wako kashinda kesi. Mashtaka 4 hajakutwa na hatia! Kakutwa na hatia ya domestic violance na kujeruhi. Kapigwa fine milion 4! Kalipa zotesasa ni mtu huruuu!
Nilifurahi kwa upande wake! Ila kwa upande wangu bado kulikuwa kweusiii. Hukumu yangu inakaribia na hukumu ya kifo naiona nje nje. Nilijuta kutokuzaa mapema! Nilijuuta! Siachi hata katoto jomoniii. Kyle akaja kuniona na mwanae alibahatika wa kike. Akaniambia namuita Linda for you. Moyoni nikaona nanyongwa wazi wazi.
Ikafika siku ya mimi kutoa utetezi wangu wa mwisho, sikujutetea sana as a lawyer nilishajua sina kesi. Nikawaza tu maisha ndo nishayapoteza. Kyle alikuwepo na mwanae. Baba yangu alikuwepo. Na watu wengi walikuwepo. Nikawaza nikihukumiwa mpaka process ya appeal ianze sio leo. Na na appeal nini. Nilikataa tamaa kabisaa.
Nikaanza kukufuru sasa Mungu sadaka ya million 167 umeikataa? Au niongeze nyingine? Au mimi ndo mdhambi kuliko watu wote duniani. Nilikufuru sanaaa! Sanaaa! Badala nianze toba ndo kwanza kama kufanya dhambi nafanya dhambi kamili.
Usiku nimelala nikaota ndoto, very clear hight definition! Tukio lile la fumanizi kama flash back! Ile sauti ya Oooh Sam! Ikajiclick kichwani mwangu ni SHOSTI WANGU WA MZUMBE. Kavisaa kabisaa 200%! Nikaota niko nimemshikia Sam baatola akaja ananyata akanipiga na kigoda usogoni nikaanguka nikazimia! Afu nikastukaaa!
Picha sasa likanijia kamili. Nikampigia Mozah usiku huo huo aniitie shoga aje jela. Shoga akajua sijui chochote ! Akaja! Nikamwambia tu najua ni yeye alikuwa na Sam na alinipiga na kigoda. Kumbukumbu imenijia. Aligopa sanaa maana there is no way ningemuona alivonipiga na kigoda! Nikamwambia pale kwangu kuna surveilance na kampuni ilio nazo iko marekani. Wameniletea footage! Kuna big boss bwana wangu ndo aliweka. Nikamwambia mpaka alivokuwa kavaaa!
Nikamwambia tu kukupoteza dakika! Ila nimechoka kukaa huku! Naomba uwe witness, ionekane ni homicide tu, utoe wewe ushahidi ilivokuwa tu! Nitapunguziwa mashtaka! In return nakupa share za bar yangu na Sam! Nikamwambia ukikataa huna bahati!
Namtia ndimu Sam asiwe akilini mwako, nilimuiba kwa shoga angu ndo ananifungisha maisha hapa unadhani wewe atakufanyaje? Muwahi wewe! Anakutumia kunifunga mimi akishafanikiwa huna bahati! Akawaza sanaaa! Akakubali!
Lawyer wangu akaomba kuongeza shahidi aliejitokeza! Baada ya ugomvi mkubwa Judge akasema sababu nikesi ya maisha ya mtu tumsikilize. Sam hakuamini shoga angu anasimama kizimbani upande wangu. Akajua sina bahati, najimalizia mwenyewe!
Akatoa ushahidi wote uliokosekana na kuifanya kesi sasa i make sense. Wlivomalizana juu yabar sijui. Ila legally nilimuuzia share zangu na akawa mmiliki halali kabisaa.
Siku ya hukumu kihoro nilikuwa nacho kikubwa. Ila nilijua Mungu kashaniona! Kosa la mauaji sikukutwa na hatia nalo, kosa la kutumia silaha vibaya nilikutwa na hatia nalo na nikahukumiwa kupokonywa silaha na jela mwaka mmoja au fine ya million 10! Kupanga njama za mauaji pia nilikutwa na hatia na hukumu ya jela miaka 3 bila fine. Ila sababu ya tukio la fumanizi mahakama itanipunguzia adhabu kutokana na tabia njema na matendo mema kwa jamii niliionesha nikiwa nangoja hukumu watauhesabu huu mwaka wa kesi kusikilizwa! Kwa hio nitabakisha miaka 2.
Nikarudushwa aegerea kwa connection za mkuu wa gereza. Hapo natembea nae namcontrol navotaka! Nikaanza kumwambia nimechoka siwezi kukaa miaka miwili nafanya mipango ya msamaha wa raisi. Akija usifanye makosa kuniweka kwenye list!
Nikafanya conection zangu wizarani! Nikawa nangojea siku ya uhuru kwa hali na mali! Ikafika! Muheshimiwa akaja. Usiku nilihakikisha naletewa list nijione kama nimo! Nishapaki vitu vyangu. Akapita muheshimiwa! Tukaitwa majina tuliosamehewa na mimi nimo! Akatutaka tukaqe reformed tusirudi tena pale. Tena akasema list naiweka hii mwakani nikimkuta mmoja wenu karudi huku atapata tabu sanaaa! Muheshimiwa akaondoka zake.
Tukamaliza ku sign na kutoka! NikamkutA kyle ananingoja nje! I was free again! I am free ndugu msomaji! Napiga miyowe i am freee! Kyle akasema dont be so happy Linda, life is not that free for X CONVICTS. Matatizo ndo kwanza yameanza.
ITAENDELEA!
hatari firee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom