Kama hujawahi kufungwa omba Mungu sanaa, tena sanaaaa! Kemea pepo zote hiko kitu kisikutokee! Hata ukiachiwa huru psychologically na socially ujue tu bado ni mfungwa! Jamii hatakaa iwe na imani na wewe. Yule ashawahi kufungwa! Baaaaaaas! Game over!
Nimetoka jela najikuta konki konki konki mastaaa! Nikata kufikia dukani kwangu, nakuta wameweka betting! Nauliza naambiwa tulifeli kodi! Sasa mlikuwa hamuuzi au vipi? Ndo pesa hio hio tuendeshea maisha! Haya nguo zangu ziko wapi? Ziko nyumbani! Bado sikukata tamaa!
Nimefika nyumbani nakuta furniture zangu wananiambia kodi iliisha! Sikushangaa sana sahivi, maana nikiwa jela wananiambia mambo yote shwariiii! Nguo zimeharibika hazifaiii! Zimeingia ukungu, madoa! Niliztia tu kiberiti nijie moja nimefilisika!
Hapo nyumbani ni kwa baba mdogo! Watu nyomii! Afu nakaribia kujifungua! Account inasoma 00! Nikampigia Moza! Akaja nikamwambia shoga siwezi kuishi hapa nachanganyikiwa! Akanikaribisha kwake! Niliwaza sanaa! Maana ana bwana pale, ataelewaje mimi kuja kukaa na mtumbo! Ila bikaenda hivo hivo! Anaishi kwenye appartment nzuri sanaa! Hazifikii ya Linda ila pako standard!
Yule bwana alinikuta pale, akawa tu mkarimu sanaa! Ananiita Mama! Ananinunulia ice cream, ukwaju! Veru carring! Mpaka nikamuuliza Mozah huyu bwana mbona hutaki kumzalia? Mbona ana roho ya utu hivi? Akaniuliza kama umechoka kuishi hapa leta choko choko ya ngoswe tuachie ngoswe! Nikaomba msamaha! Akaniyafutia bima ya premium kubwa! Not for once alini judge au kuniona ex convict!
Nyumbani nilikuwa sipendi kwenda hata kukutana na watu wanaonijua sikipenda maana pole zilikuwa nyingi sana! Nikawa nashinda ndani tu! Mpaka ikafika kujifungua mtoto akawa mkubwa sanaa, nilikosa zoezi nikapigwa kisu, nashukuru nikarudi na mwanangu nyumbani kwa Mozah! Wakike Mungu alinjalia. Nilitamani kumuita jina la mama ila Linda jela alikuwa kama Mama yangu nikamuita Linda! Japo nilikemea sana tabia za Linda!
Mozah si mtunzaji wa mzazi kabisaaa! Akaniruhusu mama mkwe wangu aje anitunze hapo hapo. Baso namwa!bia tuwe makini wasituchoke. Nakomaa na mtoto asije kulia usiku akamkera yule baba kabisaaa! Tunajifungia chumbani mda wote, mimi na mwanangu na bibi. Mpaka tuitwe kusalimia na yule vwana kama yupo.
Baada ya mwezi nikamwambia mama mkwe nenda tu, tupungue nishaweza! Mpaka pampers namtegemea Moza na shemeji. Maziwa! Nepikila kitu. Nilisikitisha! Nimelea kwa shida shida mwanangu akiwa na miezi miwili Sam akaja kuniona,mimi na yeye hatuna ubaya, akanipa million 3 nilimuona kama mtu vilee! Sikuwahi kitegemea nilivokoga pesaningekuja kutetemekea million 3, nikaziwekakwenye account kimyaaa!
Najipa moyo Linda akitoka atakuwa vizuriii sana nitahamia kwa Linda kwa mda nikijipanga! Mwanangu akiwana miezi 6 Linda akatoka, tukafikia kwanza kwa Mozah maana appartment yake ilikuwa locked inadaiwa kodi kibaoo! Nikamshauri pumzika hata wiki akili itulie kwanza mwili urudi!
Balaa likaanza! Linda hajui kujibanaa! Kakuta Mozah kaenda nje ya nchi kufata mzigo, Linda anashinda kwenye pool na bikini siku nzima anakunywa! Na yule baba wakaelewana hatariii! Wanaume wepesi sanaa! Unaona kabisaa anamtakaaa Linda!
Nikamuwahi tuhame leo leo! Anashangaa why? Kwani nimefanya nini? Nikamwambia bado hujafanya ila utafanya! Mi siwezi kutemvea na mume wa Mozah una ichukuliaje ile company tu! Nokamwambia twende! Amenuna tunaenda wapi sasa? Nikamwambia hapa nina 3 m twende !
Nikatafuta nyumba Sinza tukapata kwa laki 5 ! Tukagawana vyumba viwilivya kulala mimi kimoja nilipanga niwekehouse girl! Yeye anasema mimi hapa sitokaa sanaa! Siwezi kabisaa!
Kurudikwe ye kampuni yake board of directors wakamfosi a resign sababu ni x convict ni reputation mbaya kwa law firm yao! Akagoma! Ukarokea mtafaruku mkubwa! Wakaacha wote na kwenda kufungua law firm yao wakaiba na wateja wote! Akabakia peke yake!
Mi nikahitolea nikawe secretary! Naenda na mwanangu ofisini! Hamna mtejaa hamnaaa! Kila akiwapigia watu washambadilikia wanamuona x convict! Alidataa! Mwenyewe nilidataaa! Pesa ya kula mpaka akadange ndo tule! Kudanga kwenyewe kwa mkuu wa magereza! Tulisikitisha!
Anamwambia ampangie appartment mshahara wenyewe wa serikali wapiii! Anaambulia laki 2 za kula basi. Maisha yalikuwa magumu sanaaa! Hatuna mbele wala nyuma! Akaniambia mtoto mkubwa huyo jiongeze! Siwezi kuwalisheni wewe na mwanao! Nikasema sawa! Sio uongo!
Nikamwambia mama mkwe awe anakuja kuniangalizia mtoto nimepata kazi ya usiku! Akakubali bibi wa watu hana noma! Navuja maziwa kudanga gani huku nanuka mtindi!? Nikaweka breast pads! Perfume kama yote! Nimepiga bwanga na crop top! Tumbo la uzazi halijarudi vizuribwanga lile nimelichomekeamo! Kwa nje nadai, ndani nyapu nyapu! Lace wig langu aliniazima Mozzah ndo nitolee! Chini raba za 10,000 kko! Tumejipodoaa!
Linda yeye msichana, kavaa bukta fupiii, na vesy na raba! Lace wig muhimu! Tukaenda 4040 Tabata !aana matajiri wooote wa dar, kahama, arusha na tz kwa ujumla ndo kiwanja chao kikubwa! Maboss wa wozara zote nyeti na sirikali pale ndo chocho lao! Tumeita uber mpaka pale! Mi siomzoefu! Njia nzima nilijilaani kuachana na Sam na kupanga kwenda kumuomba msamaha! He would never allow me to front like that!Never!
Tumeingia nimekaza roho! Linda ananiambia hapa tusijibweteke ni mwendo wa kwenda chooni mfululizo zitaanza kumiminika bia! Akainuka yeye kwenda uani, taratibuuu! Karudikaniambia nenda wewe! Nikashukuru nikabadiliahe pads za manyonyo kabla top haijachora ramani!
Narudi nakuta anakunywa Jackdaniels! Akaniambia nishalinasa lipapa! Tukaitwa hamieni huku! Tukamkuta kijana tu Maprosooo! Anashobokajena Linda sasa? Huku na huku anamwa!bia twemde casino ila natala kwenda na wewe peke yako! Nikadakia sawa! Wakaniacha! Chukua bodaboda fastaa kwa mwanangu! Nikamkuta kalilia nyonyobalaa!
Alirudi siku ya 3 akauliza vipi maendeleo nikamwambia bado sijapata! Ndo nafanya mazoezi hapa na diet! Wiki sidhani kama litaisha bila bila. Akasema jitahidi sana! Haya sio maisha! Kiukweli kazi nilikiwa sijaifanya serious na Ijumaa ikawa ndo hio! Akaniambia siondoki mpaka upate danga! Ikibidi kukuuza kwa mnada nitakuuza!
Nimeenda chooni narudi naletewa muhudumu unakunywa nini? Nikaagiza Hei ken kwanza Linda Jackdaniels! Baadae akja mnunuaji mwenyewe shombe shombe! Ananikodolea mimi tobaaa! Akauliza unaitwa nani? Linda akawahi anaitwa Amina! Akajaaa! Amina jina zuriii, jina la mama ake Mtume! Nikasema ndio! Akauliza Amina una miaka mingapi? Linda akawahi kunijibia 21! Nyie nyie mweeee! Mimi nina 21 mie huyuuuu? Akajaaa! Akasema inaonesha Amina muoga muoga! Linda anamwambia kwao haruhusiwi kutoka huyu! Mwarabu kadataaaa!
Linda anamuiliza unafanya kazi gani? Akasema mimi nina shelli! Ninazo nyingi Kibaha! Same, Nzega hivooo! Niko in oil and transportation! Linda akaaga akaenda VIP sasa na yeye kudanga! Natetemeka utumbo! Nasema leonafumuliwa marinda yooote! Mwarabu huyu wa mafuta si mtu mzuri.
Akaniambia twende hotelini, nikasema poa! Njiani nasali na ku swali kwa mpigoo! Akaanza kuniambia usiniogope mimi mtu mzuri, kwanza na mke wangu sema ana mtoto mchanga, ila ni mtu wa familia! Nimekuelewa hujakaa wazi sanaa, hujajiacha uchi umejistiro nikasema tutawezana!
Nikamwambia hata mimi na mtoto, sema maisha magumu ndo nimekuja kutafuta nepi na maziwa! Akasimamisha gari! Akaniambia Amina usitumie uongo wa mtoto, kama hujanielewa kuwa muwazi tu nakurudisha kwenu! Nikamwambia kwetu nimefukuzwa si nimezaa! Ikabidi nitambae na biti fasta fasta nishasahu intro! Akasema muongoo! Nikamwambia ona mwaziwa yananivuja sasa kwanini nikudanganye? Akasema kwa hio mwanao ana. Nyonya? Nikamwambia eeeh!
Akaniuliza ulisema u akaa Sinza ipi? Nikamuelekeza! Tukawa tunaenda kimya kimya tu! Mpaka nikafika! Akanipa 300,000 nunua chakula cha mtoto, kikiisha nipigie namba hii akanipa business card! Sitaki tena kukuona 4040 nikikufumaaa huna bahati! Haya kanyonyeshe! Dogo kama alijua anajiliza mda huo balaaa! Huuuiu! Nikawa nimepona!
Sikutoka siku 3 pesa si ipo! Ya 4 nikasema nipige ile namba haipatikani! Shubhamit! Linda ashaanza choko choko! Nikamwambia Linda bimeshakuwa mzoefu kila mtu aende kivyake la maana turudi na pesa asubuhi! Akakubali! Maana nilikuwa mzigo kweli!
Nikaamua kwenda La charz! Ili niwahi kumnyonyesha mwanangu! Jirani! Kufika tu jibaba la serikali hili hapa! Linanipa ahadi kibao! Mara nataka nikufile mimi huo mchezo naupenda sana! Nitakufanyia chxochoteeee unachotaka! Nikamwambia hilo ondoa shaka! Basi roho yake kwatu! Namwambia mambo ya mjini hayo! Nikahakikisha kalewa chakariiiii! Nikamwambia. Kaenda chooni nikasepa na I phone X!
Asubuhi namwambia Linda akagomba sanaaa! Tutarudi segerea! Hizi nuksiii! Ikawa inapigwa akapokea! Lenyewe linachimba mkwara! Linda akamwambia sasa tuma pesa namba hii hapa akamtajia nambabyake ya kudangia million 2, sema uko wapi tunakurudishia! Akase!a situmi! Akamqambia hizi video zako za kiboga utazikuta insta! Na copy kwa mkeo si huyu umemsave my wife? Akasema natuma! Akatuma, tukatoa tukampa boda boda ampelekee posta! Akanikataza kuwaibia wateja!
Nikawaza kuliko niwadange nisiowajua bora niwadange nao wajua! Nikaanza na Sam! Narudia tena msomaji sina ubaya nae! Nikapendeza na kwenda kwenye bar yake! Nikakaa nakunywa soda! Akaniona lazima anionee! Akaja kuniuliza kwema! Nikamwmabia kabisaa! Akauliza mtoto? Nikamwambia hajambo! Akasema leo umenikumbuka? Nikamwambia kila siku nakukumbuka! Akasema leo sana mpaka umekuja kunisalimia! Nikamwambia nimekuja ofisini hapa kudanga! Akastukaaa! Ila hakusema kitu! Akaniaga kwenda kwenye kusimamia!
Nikaanza kupata vichwa! Huku na huku nikampata dogo, nikamwambia nina miaka 18! Ananinunulia bia sio kitoto! Sam akaja kuniita! Nikaenda kumsikiliza! Anauliza is this serious? Namwambia ndio! Anasema sio unalte jokes! Nikamwambia haya jokes mi naondoka na dogo kule! Akasema how much is he gonna pay you? Nikamwambia 300,000! Akauliza na mimi itanifanyia bei gani? Nikamwambia 500,000 mashine yako kubwa sana! Akacheka tu! Anasema nikitoa hio pesa nakula mzigo serious! Namwambia ndio , sasa kwani usile? Anasisitiza usiku mzima usidhani nitakuonea huruma? Namwambia hata kifurushi cha wiki kipopesa yako tu! Akaniambia mpotezee dogo.
Nimekaa pale mpaka kafunga bar! Mngese anauzaaa! Wanahesabu mauzo kwa machine! Akanichukua mpaka kwake! Appartments za hatari! Sam maisha yalimpenda haswaaa! Ananiambia hii ni second home, home kwakw kuna mwanamke anaishi nae! Namwa!bia basi na mimi ndo niishi hapa! Ktoka kuwa njia kuu mpaka mchepuko! Anajibu we can arrange!
Sam simuogopiiiii! Katika watu nisio waogopa ni Sam! Kabisaa kabisaa! Nimevua nguo, nimeoga na kuvaa taulo! Nakunywa zangu pombe zake bila pressure! Anataka maongezi kwanza na hivi boss kasema! Nikamwmabia sawa! Unataka kuongea nini?
Kwanini hukunizalia mimi miaka kumi? Nikamuuliza ulisema unataka mtoto? Akasema Hans alisema? Sikumjibu! Namjibu nini sasa! Akakomaa! Nikamwambia Sam niulize maswali yote ila sio kuhusu Hans hata kama unalipia hio ni too much! Akasema maswali yangu yote kubusu Hans kama huwezi kujibu vaa uondoke! Nilimia rohooo! Nikajikaza uliza? Akaendelea pale pale Hans alisema? Nikamwambia ndio alisema! Tena alibembeleza mpaka akalia! Akaguna Mmmmhhh!
Akauliza ulimchoma kisukwanini? Nikamsimulia aliniwekea unga nikapita nao airport! Akasema hata mimi ningekuchoma kisu kama ungenifanyia hivo! Ni halali kabisaaa! Akauliza mimi na Hans nani mwanaume bora zaidi aliekukosah zaidi? Nikamwambia Sam mbona unataka kuninyima hio pesa lakini! ? Akasema jibu swali! Nikamjibu Wote wangese tu! Hamna mwwnye afadhali! Akachekaa kwa dharau! Akasema ungesema Hans hii pesa haki ya mama ungeikosaa! Ungepishana nayo mlangoni.
Nikamuuliza mbona huulizi nani anafanya vizuri zaidi kati yenu? Nani alijua kunifanya? Akaniangalia kwa jicho la tahadhari! Nikamwmavia Sam unajua nini jitombee afu jilipe hio laki tano! Nikavaa na kuondoka zangu. Nikakubali tu siku hio nimefanya kazi ya kanisaa.
Nafika home nakuta kitm tim watu wamejaa! Roho ikafanya paaah! Nikasogeaa nakuta zogo! Kumbe Linda kanywa sumu bwana kakimbizwa hospitali hoiii! Mapovu yamejaa chumbani, mlango umevunjwa! Kumbe mama mkwe alisikia anakoroma, na kukuruka ndo kumzungukia akamuona anatoa povu mdomoni. Kuita watu wakavunja mlango na kumkimbiza hospitali! Nilichokaa!
Kiukweli mwenyewe sumu nilikiwa naitamanii! Naitamani mnoo mnoo! Sema mjue nini mtoto nitamuacha vipi? Ndo kilichonipa nguvu ya kupambana! Nikaenda hospitali hali yake ilikuwa mbaya mno mno! Nikarudi nyumbani naweweseka mama mkwe akanipa barua alioikuta kwa Linda!
Imeandikwa kifupi tu!
"Kyle ndugu yangu utaniagia kwa wengine, nimeshindwa maisha haya, nimeshafeli maisha na huo ndo ukweli! And please dont blame this on you" Forever friends! Linda!
Niliumiaaa sanaaaaa! Tena sanaaa! Kilichoniuma zaidi this is me next kama nisipo jiongeza! Saa 8 hio nikambeba mtoto mgongoni nikapanda bodaboda mpaka Club D! Nikazuiwa kuingia.
Nikaanza kuita Ghooooooosttt! Wananitoa kwani natoka sasa? Watu wakajaa! Akaja Ghost! Kyle kumbe ni wewe? Hans hayupo hapa if this is about Hans! Nikamwambia its not about Hans nashida na wewe binafsi! Wakaniachia niingie ofisini kwake!
Amenikazia mijicho, Nikamwambia nipe huo huo unga nikupelekee nchi yoyote, bara lolote,mji wowote kiasi chochote kwa bei yoyote! Akaniuliza umetumwa nini? Nikamkazia sura! Wakaja kunisachi wire sinaaa! Mpaka breast pads wakazichana chana hamna wire!
Akaniambia mimi siuzi unga these days! Nikamwambia Ghost! Ghost! Ghost nimekuita mara 3, nimesema nipe huo unga nisafirishe! Nipo tayariii!
ITAENDELEA KESHO