Amar! My Story.
I always wanted to something with my life, bigger than life itself. Since i was aboy i always saw the bigger picture. I started stealing by the age of five. It just felt right. Kwenu naweza kuonekana gaidi, bandidu mtu mubayaaa, ila mimi ni mtu kama nyie na nina sababu zangu za msingi kabisaa. Nilipokuwa naiba mama alikuwa ananimbia Mungu hapendi, ni dhambi and so on.
Wanasema Baba ni Mungu wako wa 2 duniani, ndio Mungu unaemuona, na baba yangu alinikataaa kata kata. At first i just couldnt accept the fact that my dada doesnt want me. WHY was baically the main question. Nikasema labda mama limuuzi na alimkosea sanaaa. Kwa jitihada zangu nikiwa primary nilimchimba bibi, pasipo kutaka sababu kila siku ieandayo wa Mungu nilikuwa namuuliza baba yngu ni nani, bibi jibu lake likawa moja, baba ako firauniii mjkuu wangu, hastahili hata tone la akili yako, yule alikojoa mbegu tu, bibi yangu ni mzaramo mumsamehe bureee.
Siku bibi akachoka akasema twende ukamuone firauni ambae ni baba yako, labda ukiona firauni kiasi gani utapata akili ya kuangalia maisha yako, usikae kabisaa hata sekunde ukawza una baba,sijui aakusaidia ule mfano wa baba tu, wala baba huna paleeeee. Bibi akanikokota mpaka kwenye ofisi moja ya bank, akasema ngoja hapa. Baadae akatoka mbaba, nilivomuona tu nilimjua maana tumefanana sana akamuila Julius. Julius kutuona akawa kama kaona kitu cha kumchefuaaa na kumuondoa mood.
Bibi akamfata akamsalimia shikamoo. Bibi akajikausha, akamwambia mwanao alikuwa anakuulizia baba yake, sasa sijataka kukufanyia uchuro umekufa, japo matendo yako na mfu hayana tofauti kabisaaa, nimeleta maana sie tukikuteta ananuna anatuona wangu tu, hatukupendi, nimemlet akuone mwenyewe ulivo firauni, ila akae akijua hana baba wal mfano wa baba. Julius akakasirikaa, sikia wewe bibi nikwambie kwa mara ingine, mimi sio baba wa mtoto huyo, kaka na mama yake akuoneshe baba yake, ila mimi sio, mbona unataka kuniharibia ndoa yangu? Muulize mwanao vizuri, dogo mimi sio baba yako, wanakupotezaaa. Akaondoka.
Tangu siku hio sikuwahi kumuulizia baba yangu tenaaa. Sasa Mungu wangu naemuona ndo alinitenda hivo, put your self in my shoes, my second god wants nothing to do me, absolutely nothing, ist because i have done something to him, no, he just dont like me, it made me loose faith on my bigger father Sr. God. I just concluded i dont have any fatherim just on my own.
Growing up withou a father nad mather wasnt easy, mama aliolewa tena, and she too didnt want me, anasingizia mume wangu hatakiii kabisaa huyu mtoto tukae nae. Pale kwa bibi palikuwa pagumu manake bibi ana watoto wngine mama zangu adogo wana watoto ao, wamezaa pale pale kwa bibi na wapo, so kila mtu anaangalia wanae mimi sina wa kuniangalia, bibi mzee mpaka aje anikumbuke jioni sanaa. Wale mama wadogo wananunua chips wanakula na wanao, au sikukuu wananunua nguo za watoto wao mi nabakia hivo hivo, labda bibi akiona vipi ndo afanye manuvaa. Kula chakula bila nyama ilikuwa kawaida manake mpaka kila mtu ampakulie mwanae nyama zimeishaaa. I jus grew up knowing i am on my own. Nikizubaaa napotea.
Mjomba wangu Mungu amuweke pema peponi, alinipeleka English Medium, akanimbia uncle mimi nikiwepo utasomaa mpaka ufike mwishoo, maka unambie uncle mi basi shule, nita fight usiku na mchana. Uncle alikuwa konda wa magari ya mikoani. Hakuwa na uwezo ilaalion umuhimu wa elimu. Ananimbia uncle wangu wewe kama mimi, ni kama tu yatima, wazazi wote hawakutaki, usiposoma huko mbele kugumu, utapoteaaa. Mi nitakusomesha uncle, kwanza baba yako mwenyewe japo hakutaki msomiyulee, darasa kaenda za kutosha, babu yako kwanza professor, shule itakukubali mi nakwambia.
Mamdogo kama wanga wacha watake ile chance apewe watoto wao, uncle akakomaa nyie akili hamna, mmezaa na wabeba mizigo, sijui ma dj hao watoto akili watatoa wapi. Si baba zao wapo wawalipie. Shule kiukweli nilikuwa nakuwa wa 1 kila siku, not that i ws bright, ilikuwa ukiwa wa 1 ada ulipi, sasa ikawa inanilazimu niwe wa 1 ili uncle kumpunguzia mzigo, mara chache nilikuwa nikiwa wa 2 uncle ananipa moyo,ila mwenywe najistukia asije kunichokaaa. Wakati uncle yupo kidogo hela ya shule , uniform, sikosi kabisaa, hata wenzangu haakujua home pagumu wala nini, mpaka school bus ananilipia fresh.
Darasa la 4, uncle alipata ajali, gari yao ikapindukaaa akakatika mguu, akaugua sanaa, akawa tu yupo home hana issue, amelost, ananimbia uncle Mungu hakupendaaa, uncle wako nimelost. Miasha yakawa magumu sanaaa. Nauli ikawa ishu. Na uncle alikuwa kama ndo anasimamia show pale kwa bibi, sasa alivokuwa alosto, mguu ana, anashinda kijiweni anavuta tu bangi, kulaviroba na kuangalia porno, maisha yaliyumba sanaaa, sanaaa. Kuna wiki sikwenda shule wiki nzima nauli hamna.Bibi akakereka akaniambia beba begi lako, we si una mama, twende huko huko.
Tumefika kwa maza, ushuani, maza anaishi nyumba nzima,kuna geti, tiles, kama hotel, akaniambia mi naenda, akija mama yako, mwambie bibi kasema kachokaaa na yeye anapumzikaaa ukae huku huku. Nikawa nimekaa nje barazani. Badae akaja mtoto na school bus kama darsa la 1 ananiuliza who are you? nakajibu. Kananiambia njoo ndani. Nikasita. Baadae namwambia dada, you are very bad kwanini humpi kaka chakulaaa. Dada wa kazi akaniletea nje.
Mama kuja dada kamuwahi nje, bibi kamleta mtoto anasema mwanao, kachoka yeye, mama kuja mbio kuniuliza imekuwaje? Basi ndo kuchukua hela ndani kunipa usiku huo huo kaniitia taxi nirudi kwa bibi, akanipa namba hela ikiisha tuma sms humu nitamtumia bibi akupe. Hapa hutakiwi kukutwa na mume wangu, itakuwa sooo. Ndo ikawa nafuuu, natuma tu sms huku hela imeisha. Hela ya ada, wakati ada silipi nampa uncle naona namsaidia kumbe ndo anazidi kunywea viroba tu.
Nikiwa darasa la 6, akiwa kalewa akagongwa na gari na kufariki dunia hapo hapo. I never felt alone in this worldkama siku hio. Japo uncle maisha yalikuwa yashamla Tigo kimtindo ila uwepo wake ulikuwa wa maana sana, he was the father that i didnt have. Sema sasa ndo bad father. Kuna siku nilipigwa shule, akanipa kisu, wakikupiga tena choma wote visuuu, choma usiwaze, dunia hii ukilegea unapotea. Uncle anakaa vijiweni na mimi naka nae, sasa story za kutukuza umalaya, wanawake, pombe na wizi zilinikolea sanasanaaa. Nikawa na uncle kitu kimoja. Bibi anapiga yowe unamuharibu huyo mtoto, uncle anamjubu mnataka ashinde na nyie wanwake awe shoga? Huyu anatakiwa akae na sisi wanaume awe dume la mbegu. Hahahaaaa.
Kijiweni wenywe walianza kunikubali kuwa dogooo, hatariiii. Sasa na mimi kutaka sifa nazidisha sasa, kuwa mkoraa mkora kweliii. Wakifanya matukio mi ndo mchora ramaniiii,na hivi nacheki muvi,nasoma vitabu watanipatia wapi. By the time niko darasa la 5 nikaanza kusimamia show kwa bibi, bibi anajua hela napewa na mama, kumbe nipo kwenye michongo ya wizi huko, ukabaji, uporaji.
Uzuri ncle aliniruhusu kutumia pombe tu, vilevi vingine alinikataza kabisaaa. Baada ya uncle kufariki kijiweni wakanichenjia wewe dogo bwana Uncle wako alikuwa anakutakia mambo makubwaa, alikuwa na mipango mikubwa na wewe sanaa. Alitaka usome darasa uwe boss kitambi meneja. Sasa sababu alikuwa mtu wetu sanaaa, tumona tumsaidie kutimiza matkwa yake ya mwisho. Ambayo ni kukusaidia wewe usome ufike mbali. Uhuni, wizi, ulevi marufukuuu. Tukikukamamta ni kichapo tuuu. Vijiwe marufukuuu. Hata uende kijiw cha mbagala ujue hatutajua tutajua na tutakuchenjia. Hapa hutakiwi kabisaaaa. Unachoruhusiwa ni kuwa malya tani yako, tembea na mtaa mzima, temba na mama zako, bibi zako huo ndo uanaume. Ila wizi, uhuni utaishia jela afuuncle wako alivokuwa mkorofi yule atajia ndotoni na mibakoraaa, atatucharazajeee sasa na hivi mzimu, anaweza hata akawaanatucharaza mchana kweupee. Hahaaaaaaaa! Bora mizimu mingine inangoja giza ndo ifanye yao, yule hata asubuhi akikumbuka ufirauni tulioufanya anatembeza bakora tu. Haahaaaaa!
Sikukaa tena kijiweni ila sio kwamba wizi nilicha, wizi kama kawaida. Niliacha kuwa front maana wale washkaji za uncle waliniwekea rada, wakanichimba mkwara ukiiba tunakupeleka wenyewe polisi, ikabidi nikae kwenye sekta ya udalali wa mali zilizoibiwa. Na hivi shule niko na wakishua, hela ilikuwa wazi. Mali ikiibiwa napewa kwa siri ili wale wanga wasijue, nami nawaonesha wanafunzi wenzangu wanawaambia uncle zao, na wengine mambo yanakuwa level.
Kuna siku ililetwa simu, nikataka kuipasisha kwa uncle wa rafiki yangu, kumbe huyo uncle anamjua alie ibiwa ile simu bwanaa. Wkaja huyu uncle wake na dogo. Nikawaambia kama vipi nyie nedeni polisi. Uncle akasema siis hatuendi polisi ila tunataka mgao ikiuzwa. Mi kuinunua siwezi maana mwenyewe ataniona nayo, ila ikiuzwa nipozwee. Nikamwambia hayo ndo maneno ya nyie watoto wa kiume kuongeaaaa, sio kushobokaa. Ikiuzwa utapata mgao. Ikauzwa nikawapooza soo likapitwa.
Siku nikaletewa simu imepigwa psota huko, kuikagua simu ya baba yangu wa kambo. Na kilichonijulisha yule dogo mtoto wa mama alikuwa screen saver. Nikaipitisha ukaguzi, kumbe baba firauni tu na yeye ana wanawake kibao, nikatami zile meseji nizitue kwa mama, anu nimpelekeesimu nzima, nikawaza tu dogo yule damu yangu ujue, afu kalelewa kimayai mayai, afu mtoto wa kike, kitaa hatodumu siku 2. Nikamee tu maana nikajua nikikiwasha tu kule dogo atajikuta kwa bibi na bi mkubwa mtu wa kuolewa tena tu. Na simu nikaiuza hela nzuri tu.
Japo simu ndo ilikuwa biashara yangu kubwa ila dhahabu nazo zilikuwa dili zangu, saa, na mambo kama hayo ya wakabaji. Bibi niliwahi kumpa jikufu la gram 250, alnalipenda mpaka kesho, kufu lisipoonekana hakulaliki mule ndani kabisaaaaa. Mama zangu wadogo nilikuwa siwapendi natoa mswaki tu, hata waniagize nini sitoiii. Bibi akaniona mimi tegemezi eti mda mwingine watu wanataka hela anasema mngojeni Amar arudi, Amar mwenyewedarasa la 7 jamaniiii. Kuna muuza Unga lishoboka kutaka kuniingiza kwenye u pusha, habari zikafika kijiweni, Pusha alijuuta, alichomewa moto kijiwe chake, gheto na nyumba yao ya urithi. Akaambiwa hio rasha rasha tu ajaribu tena ndo atawajua wao kina nani. Pusha alihama mtaa kabisaa na hajawahi kuonekana tenaaa. Tangu hapo watu wakaanza kuniogopa kabisaaa.
Wanawake nilianza nao tangu na balehe, huenda kabl hata sijabalehe kwenye baba na mama nimefunua sanaa wadada. Kwanza nilikuwa na hela, afu kikristo kinapanda, na mtu wa swagga sanaa sasa nakosaje wanawake kwa mfano, uswaiz hali ilivo ngumu. Soda tu unamla mke wa mtu. Nasikitika sikupata mfano wa kuheshimu wanawake, au sijui nimerithi mzee wangu maana vya kurithi vinazidi, mama wadogo nao walikuwa chupi mkononi sanaa, ukipa chocho hili lazima umkute huyu na bwana huyu leo, yule kesho hawasomeki kabisaa.
Nimemaliza msingi nikaingia secondary Azania, Aza boy, sikutaka boarding kusudi biashara yangu si mnajua tena. Nimefanya umalaya sanaa form 1 mpaka basiii. Manake hela ninayo, miziki naijuaaa pombe nakunywa, pamba napiga, simu nabadili kama nguo, yani nilionekana wa kishua hatariiii.
Sijui ilikuwaje ila nilikuwa na mkono wa kupiga wanawake. Demu akinizingua nampa kichapo cha uhakika.Sasa nilikua moraaa. Before i know it mademu wote hawanitakiii, washanijua sio, kwanza kitombiii, afu natembeza u Francis Cheka wa hatariii kwa Mademu. I jsut didnt know how to treat women. Dont blame me, given nimekulia kijiweni what could you expect.
Ilifika mahala nikienda na emu kwa bibi, bibi anamwambia utapigwaaaa, utakungutwaaa, huyu mara huyu japo mjukuu wangu ila sio mtuuuu, mi nakwambia binti, bora uondoke usije tenaa, huyooo mbwa tuu. Deu anatoka relay hana hamu. Baadae namchenjia bibi ile ile namwambia kwanza wewe bibi utakuwa mwangaa wewe si bure, mtu gani umezeeka hufi, mchawi wewe nakwambia, nae ananipa vyangu ningekuwa mwanga si ningekula nyama tangu mdogo, wazazi wako wamekutupa hapa na kwashiakor, umekondeanaa, nakupangua mavi, na kupambana uwe mtu leo hii umeota vuzi unaniita mimi mwanga? Ndo malaya kama baba yako, Mi nakwambia hio damu yenu ya vampayaa sio baba wala mtoto. Tunapeana kavu na bibi naingi gheto. Dakika 10 nyingi,Amara baba yangu umelala, si unajua nakupenda sana mjukuuwangu, fanya mpango wa mboga basi. Ndo kesi imeishaaa. Nikileta demu mwingine kama kawaida yake lazima aniwangie tenaaa. Nammind namwambia bibi wakati unakitembeza umezaa watoto baba mbalimbali mbona nilikuwa sikuingiliii lakini kwenye mishe zako, mbona hivo bibi unakuwa hunipendi. Anajitetea mimi nimeolewa ndoa 5 nazote nimezaa, sina mwanaharamu hata mmoja. Wew unavofanya dini haitakiii. Japo msikiti umeuasi ila haitakiw tukuendekezeee, we umlaya fanyia mbali ukijaribu humu lazima nikuingilie kwenye anga zakooo na kukuharibiaaa. Mwisho nikaacha kupeleka mademu home nikaona isiwe tabu lodge si zipo.
ITAENDELEA SAA 6 USIKU HUU.