Website Ubalozi aibu tupu

Tumsifu Samwel

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2007
Posts
1,408
Reaction score
163
Je ulijua kuwa ndombolo na zouk ni traditinal music ya Tanzania? je ulijua sprgheti ni chakula asili cha Tanzania? Ubalozi wetu Ukitaka ujue kama ndombolo ni muziki wa asili wa Kitanzania na spargheti ni chakula cha asili cha Watanzania nenda tovuti ya Ubalozi wetu USA. http://www.tanzaniaembassy-us.org/tzepeo.html Ni mewaandikia wakajibu watanijibu mpaka leo jiii sa unadai hivyo nenda kacheki......ukicheka unanilipa

Kichekesho kingine website ya ubalozi wa Marekani Dar es salaam ina lugha ya kiswahili na kiingereza website ya ubalozi wetu Washington ina lugha moja tu ya kiingereza,ina maana ipo kwajili ya Wamarekani tu au?... website ya Ubalozi wa Marekani Tanzania http://tanzania.usembassy.gov/
 
Other native beverages are specific to certain regions and tribes. These are; Mnazi/ Tembo (Coastal region), Mbege ( Kilimanjaro region ), Wanzuki, Gongo. There also various beers, wines and spirits produced in Tanzania. These include Kilimanjaro beer, Safarai beer, Serengeti beer,Konyagi, Banana Wine and many more.

Uwiiiii!! yani jamaa wameweka ilicit brew in the list of traditional beverages??? are these people sewrious???
 
Hizi tambi na makaroti mengi namana hiyo ndo traditional food?
Walikosa unga wa mahindi? si wangeweka hata nguna la maana hapo na bamia kiaina?
 
tehe tehe....traditional food...kitimoto na kisusio!!!

nachea mwenyewe tu hapa.
 
Hizi tambi na makaroti mengi namana hiyo ndo traditional food?
Walikosa unga wa mahindi? si wangeweka hata nguna la maana hapo na bamia kiaina?

They are crazyyyyyyy.... watanzania tunatia aibuuuu.. vyakula asili tanzania viko kibao, wangeandika hata matoke au makande, lol.. ndombolo ni mziki wa bantu ba congo.. aibuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!
 
Hivi tambi ni traditional food ya wapi? Wasaidieni, naona hawa jamaa walidesa kasa!!
 
Mimi sina uhakika kama kuna watu kule walishawahi kuishi Tanzania. Inawezekana ndio wale wanaopigwa juu kwa juu toka wamezaliwa na mazingira halisi hawayajui si afadhali basi wangeliweka bongo ya fleva kama hawana rhumba za kitanzania? kuna msondo,kuna achimenengule wa wa wa na kuna goma la ukae sikinde kuna boso kuna masika zole zole wa zole langa yaani masikhara kwelikweli. Naam kwanini waamue kwamba muziki wa kikongo ndio asili yetu hawa jamaa hawana mtu wa utamaduni nini au ndio mazabe yenyewe digrii feki na akili feki!
 
Ndugu si unajua hii Nji inavyo endeshwa? ndio maana wakenya wanatuona wajinga wakutupwa hadi wanatangaza mlima wa Kilimanjaro huko kwao,sisi tuna baki kusema Ndombolo ni mziki wa asili ya Tanzania.... Hivi jamani kazi ya balozi si ni kuwakilisha nchi na kutanganza nchi?
 
kuna mahali wametaja majina ya wanamuziki......Judith wambura na Lady J Dee..kama watu wawili tofauti.
 
kuna mahali wametaja majina ya wanamuziki......Judith wambura na Lady J Dee..kama watu wawili tofauti.

Ni A.K.A , mkuu
 
Judith Daines Wambura Mbibo aka Lady Jaydee
Hawa ndio wawakilishi wetu ubalozini, nina wasiwasi iko siku mtu ataenda ubalozini na kuuliza mambo muhimu ya nchi na wakashindwa kumjibu maana hawa ni bure kabisa.
 
jamani kumbe gongo ni official???????????/ mi naanza sasa kusaka uwakala wa kuimport gongo uku majuuu............... uwiiiiiiiiiiiiiiiii................ aibuuuuuuuuu.............
 
jamani kumbe gongo ni official???????????/ mi naanza sasa kusaka uwakala wa kuimport gongo uku majuuu............... uwiiiiiiiiiiiiiiiii................ aibuuuuuuuuu.............

Ulikuwa ulijui hilo? mmh unajitafutia matatizo wewe!
 
Ugali wa muhogo na mboga ya mlenda hamna humo?
 
Nafikiri hayo maoni yako mwandiswhi ungeyapeleka kwa Waziri wa Mambo ya Nje pengine angeliona hilo na kulifanyia kazi kwa Web site zote za Balozi zetu Nje nia kujenga sio kuponda. ila kwa kuwa uliwaandikia wahusika wenyewe ndio maana hakuona umuhimu wa kurekebisha.
 
halafu hapo kwenye gongo kwa kuwa ni pombe haramu (inatengenezwa kienyeji) wasingeiweka ila wangeacha hiyo konyaji ambayo nayo ni gongo ya kisasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…