Raj kapool
JF-Expert Member
- Jun 29, 2018
- 1,630
- 2,771
TAFAKARI TABIA YAKO MBELE YA JAMII
Ng’ombe, akishatoa maziwa ya kulisha familia nzima, hurejea katika malisho yake taratibu. Lakini kuku, akishataga yai moja hupiga kelele ili kila mtu ajue. Je! Yai hilo alilotaga laweza kutosha hata kwa mlo wa mtu mmoja? Jibu ni hapana .
Katika maisha kuna watu wa aina mbili; kuna wale wanaofanana na Ng’ombe na wale wanaofanana na Kuku kwa tabia na mienendo yao.
Mtu afananaye na kuku akikusaidia jambo hata kama ni dogo sana atasema kila mahali ili watu wote wajue jambo hilo. Kama ni kazini au popote ulipo, atahakikisha anajisifu sana na kuisambaza habari yake ya kukusaidia kwa watu wengi. Dhamira kuu ikiwa kila mtu ajue msaada wake kwako!.
Kuna watu walisaidiwa na watu hawa wenye tabia ya kuku baadaye wakaishia kuumizwa mioyo yao baada ya kusambaa kwa habari hiyo. Msaada ukageuka fedheha kwao.
Mtu mwenye tabia ya kuku akitoa msaada hata kwenye kituo cha watoto yatima, au akisaidia maskini atatamani kila mmoja ajue na ndio hawa ambao hawawezi kutoa msaada bila jamii kutambua.
Kuna watu wenye tabia ya ng’ombe
Watu hawa wakikupa msaada wa mali au mawazo hata kama ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kumlipa fadhila, hawawezi kukusema kwa watu wengine au kujitapa kwa fadhila zao. Furaha yao ni kukuona unavuka salama na unafanikiwa kadri ya lengo lako lilivyo. Watu wa namna hii hupata thawabu kubwa kwa mwenyezi Mungu
Tamani kuwa na tabia kama hii ya kusaidia bila kujitafutia utukufu au kumfanya Bango la matangazo yule ambaye umempa msaada huo.
Hatulingani kwa vimo wala uwezo wa kupambana na maisha . Kila mmoja ana kamba yake kwa urefu ambao Mungu amemjalia . Kama kamba yako inakuruhusu kufika mbali, usisite kurudi nyuma kuwasaidia wale ambao hawafiki ulipo wewe au kuwasaidia kimaarifa kurefusha kamba zao katika upole na unyenyekevu.
Asanteni
kama ulipokea usisite kutoa tena