Mkuu Mndengereko usikate tamaa ya kujifunza lugha, hivi ni vijimambo tu vya kupashana joto, ukijaribu, ukakosea, ukakosolewa, ndio unapata fursa ya kujifunza, hii si lugha yetu ila ni lazima kuijua maana ndio lugha ya biashara. Hata mimi niliyekukosoa sio kwamba nakijua kimombo ila tu nimeweza kuona makosa kwenye lugha yako, hata mimi hukosolewa sana tu. Hebu angalia hapa chini:
"no you don't my friend (unless) if you have take a lesson"
Hapa ulitakiwa uandike 'no you don't unless you take a lesson' "if" haikutakiwa kuwapo kwa sababu imeshawakilishwa na 'unless'.
Pili ukisha weka 'have' lazima useme "taken" hence 'you have taken' not 'you have take'
has 6 course and each (courses) it has at least of 5 lessons
Hali kadhalika hapa ukishasema 'courses' usiseme tena 'it' kwa sababu 'it' imeshawakilisha 'course', so ungesema 'the course has' na sio 'the course it has'
Pili kama umeamua courses (wingi) basi lazima iwe 'have' badala ya 'has' yani ingekuwa 'the courses have at least five lessons.
usikonde mwana pamoja sana.