We Are Not Too Late!!!

Ntakasi

JF-Expert Member
Oct 21, 2013
1,427
1,195
Wapendwa,Marafiki,Wadau.......
I Greet You!
As We Approach 2014 And Leave Behind 2013:::::kila mtu ana story yake.....nzuri na mbaya......Tukiwa tunaangalia 2014,kila mtu ana malengo yake......mipango yake......na maombi yake.
Nimeingia humu this year but i've been browsing as a visitor for almost three years now.....(many non-members still do that)
Within few months of being'Active'..nimejifunza mengi.....katika kujifunza huko nimegundua pia vingi.....lakini naomba niweke miongoni mwa vile ambavyo ni HASARA kwetu kama 'Jamii'
-UDINI
Kuanzia mdogo,nimekuwa katika jamii ya kikristo na kiislam...na sijawahi kuexperience 'Udini'kama nilivyoexperience humu......huku nje,(kwa eneo ninaloishi)pilau ya Idd na X-mass huwa tunakula pamoja...lakini humu ndani,naamini laiti kama ingekuwa ni 'Jumuiya' Halisi...basi tungekuwa na Vita Ya Ajabu....wasiwasi wangu ni kuwa baadhi ya members'wenye udini'..wannaweza kuwa Sumu katika kata zetu huku nje....Inasikitisha kwa kweli!..kuna akili za kuziacha kama zilivyo s ili TOFAUTIi isomeke....Ila si zile za UDINI...... Tupendane....Tunaweza tukatenda mema yoooote ila tukasahau 'Upendo Kwa Wote'...kitu ambacho huvuruga hata mema yetu tuliyofanya..,..Huvuruga hata nia zetu njema sababu tuna chuki na kundi fulani.......
Mungu Anajiinuaa sababu ANAISHI NASI SOTE......Hakuna haja ya kutukana mitume,vitabu au nabii wa dini nyingine ili kutetea ya kwako....Mungu asingemtaka mkristo au muislam basi wasingekuwepo....Asingemtaka mhindu or whoever basi wasingekuwepo.......Anayesali amesimama au ameinama lakini as long as moyo wake unatafuta mema kwa MUUMBA basi si sababu ya kuhukumiana....
Wengi siku hizi machafuko yanapotokea tunakimbilia kusema 'Dunia Imeisha'..ni sentensi ya kipumbavu mno.....sababu tunaacha kuchukua hatua muhimu sababu tu tunaamini inabidi iwe hivyo.....Ok,Kama Mungu bado analrta maelfu ya vizazi....vizazi hivyo vitakuwa na story ipi nzuri juu yetu?
Nguvu za chuki tungezihamishia kwenye kujenga 'Jamii Nzuri' tungeepukana na Mengi....
Nguvu ya chuki ihamie kwenye nguvu ya kupinga chuki....Naaam!Tuache Siasa Za dini......Wivu wa kijinga Na Majungu tunayoita 'harakati'.....Ilihali tupo hai basi Mema Yanaweekana kushinda ubaya...Mimi na Wewe ni sehemu ya mabadiliko...kwa pamoja tuhubiri upendo na mazuri....
Merry X-mass&Happy New Year!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom