We are already Cyborgs

Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,343
3,284
0ead0194ce84e5a732dc5a049f669f27.jpg

Habari ya mwisho wa juma wakuu.

Matumaini yangu mko buheri wa afya.

Leo wakati napitia parua-pepe kusoma makala toka mitandao niliyojiunga (subscribe) nikakutana na hii habari kuhusu kampuni mpya Elon Mask amefungua inaitwa Neurolink Corp.

Kwa wasio mjua Elon Mask huyu ni raia wa Marekani mmiliki wa kampuni ya magari ya umeme Tesla Motors pia ni mmiliki wa Space X. Ni billionaire asiyeishiwa ideas.

Kabla sijaelezea hii kampuni niseme tu binafsi navutiwa sana na mambo yanayoelezea future technology. Nikipata makala inayoelezea teknolojia yakusisimua kama hii ya Elon Mask najikunyata nasoma kwa makini.

Kwa mujibu wa bandiko la Wall Street Journal hii kampuni ya Neurolink inajihusisha na utengenezaji wa teknolojia inayofahamika kwa jina "neural lace".

Hii teknolojia ya neural lace inahusisha kuwekewa (implanting) brain electrodes ambapo siku moja wakuu itakuwa inawezekana kabisa ku-upload na ku-download mawazo ndani ya ubongo wako.

Kwa wanaofuatilia makala za technology hususan makala zinazoeleolezea nanotechnology watakuwa wanafahamu majaribio mengi tu yamefanywa kuona uwezekano zaidi kuweza kusoma na kuelewa mfumo tata wa ubongo.

We are already Cyborgs wakuu.

Hii idea kuhusu "neural lace technology" ilianzia kwenye riwaya ya jamaa anaitwa Ian Banks. Raia wa Scotland. Kwenye mfululizo wa riwaya zake alielezea jinsi humanoids wanavyojiwekea kifaa ambacho kimebeba teknologia ya neural lace. Kwa wasiofahamu humanoids kwenye biotech ni viumbe kama wale wanaoonekana kwenye Star Wars.

Ukipandikiziwa hii teknolojia ya neural lace kwenye ubongo wako basi hii teknolojia inakuwa (grow) kadiri ubongo wako unavyokuwa. Hii maana yake teknolojia ya neural lace inaungana na mfumo wa ubongo wako.

Hapa nilipo nafikiria ugunduzi wa kustaajabisha kama huu. Nafikiria jinsi wazo lilianza kama hadithi ya kusadikika tu, leo inaenda kuwa kweli. Hakika kauna linalomshinda mwanadamu anayewekeza katika utafiti. Muda tu ndiyo mwamuzi.

Basi nikiendelea, mwanadamu akipandikiziwa hii teknolojia inatoa nafasi kuonyesha vile ubongo unovyofanya kazi ambapo itakuwezesha vifaa vya kielekroniki ku-interface na ubongo wako.

Hii mfano wake kuielewa chukulia vile unavyoingia kwenye mtandao wa internet unaweza kusoma habari, ku-upload taarifa au pia kudownload habari fulani iwe katika mfumo wa pdf au Ms word.

Huo mfano ni sawa na hii neural lace technology. Mawazo kwenye ubongo wako mtu anaweza kuyasoma....au akiamuwa ana-upload informations kwenye ubongo wako. Pia inawezekana ku-download mawazo wako.

Charles Lieber, mtaalamu wa nanotechnology Harvard University pia mshiriki katika research inayoelezea hii technology ya neural lace wanachojaribu ni kutengeneza daraja kati ya electronic circuits na mfumo wa ubongo wa mwanadamu.

Wakuu uvumbuzi wa kustaajarisha kama hu watu wanaweza uliza sasa inasaidia nini hasahasa. Hii teknolojia itawafaa sana watafiti wanaohangaika kuwasaidia watu wenye Parkinson disease.

Upande mwingine hii teknolojia itakuwa ndiyo mwazo kuwezesha teknolojia ya cloning kwa binadamu. Nasema hivi kwa sababu kuna jamaa hapa JF alidai Jimmy Carter amefanyiwa cloning. Binafsi siamini hivyo. Sasa hivi tunao android na gynoid.

Kwa wasiofahamu cloning kwenye biotech ni namna ya kutengeneza DNA ambazo zitakuwa na taarifa zote za binadamu (mfano wewe hapo msomaji) halafu anatengenezwa binadamu mwingine anayefanana na wewe kwa kila kitu kutia ndani namna unavyofikiri.

Wakuu kwa wasiofahamu pia android na gynoid ni nini hii siyo operating system ya Samsung....hehehee hiii ni humanoid robot ambayo inatengenezwa kufanana na binadamu. Wakiume anaitwa android na wakike anaitwa gynoid.

Nikiona maendeleo makubwa namna hii katika technology kuanzia nanotechnology, biotechnology, bio-engeneering, synthetic biology na field nyingine nawaza sana kuhusu miaka michache ijayo. Je itawezekana hats kuzuia kifo? Labda kuzuia seli zinazotufanya tuzeeke? Au labda mtu akipata ajali na kufariki ataweza kufanyiwa cloning? Sisi tunaoishi nchi duni kiteknolojia tunafikiwa na hizi aina mpya za teknolojia? Je ndiyo itakuwa mtego kutotupa hizi teknolojia ili watutawale vizuri? Hebu fikiria mtu aliyepandikiziwa neural lace technology si atakuwa ni mtu mwenye super power? Kwamba mataifa yaliyoendelea kiteknolojia yatatumia watu hawa kuvumbua vitu zaidi? Na wakiingia jeshini si ndiyo itakuwa hatari zaidi? Hakuna atakayewashinda.

Kwa hakika teknolojia inafikia hatua ya kustaajabisha kabisa. Naamini binadamu watakuwa tunatembea na kupishana na androids na gydoids mitaani wenye uwezo wa kuwaza wenyewe bila msaada wa mtu ku-control computer. Hawa humanoid robots watakuwa wanauwelewa kuzidi binadamu. Watakuwa wanajitambua wenyewe, wanaweza hadi kutofautisha kati ya jambo baya na zuri. Pia nawaona hawa robots wakipata maarifa kuweza kutengeneza wenyewe mfumo fulani kuongoza masha yao.

Unawaza nini kuhusu future technology? Miaka ishirini mbele, miaka hamsini mbele?
 
49764cbc3cb7ed5aaac6ca9ff9e8db53.jpg
 
kudownload mawazo kwa msaada wa electronic devc kutoka kwa natural human being haito kaa ikae
 
Hii ni furaha kwa blackhats....naona kabisa wakitamani kuijaribu hii kitu ikoje.
 
Back
Top Bottom