WCB watembelewa na Waziri wa mambo ya ndani

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762
Katika kile kinachoonekana viongozi wa serikali kuvutiwa na jinsi Diamond na lebel yake WCB wanavyoibadilisha tasnia ya muziki wa Tanzania kuwa fursa ya kibiashara na kazi rasmi, Mh. Waziri wa wizara mambo ya ndani, Mwigulu Lameck Nchemba ametembelea ofisi za WCB na kukutana na baadhi ya wafanyakazi na wasanii wa label hiyo ili kuwapa moyo na kuwahakikishia kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakisha kazi zao zinalindwa kwa mujibu wa sheria. Pia kawaambia kuwa serikali haitasita kuwapa msaada pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.

Binafsi nimeona ni jambo jema hasa ukizingitia wameshatembelea viongozi na mawaziri kadhaa. Rai yangu kwa wasanii wengine kuiga mfano wa WCB katika kuwa na ofisi maalumu na kuzipa thamani kazi zao.

wcb1.jpg

wcb2.jpg

wcb3.jpg

wcb4.jpg
 
Wanasiasa wetu wana mambo sana...
Diamond siyo artist peke yake, bali ni mwajiri aliyeajiri vijana zaidi ya hamsini, na katika vijana hao wapo wenye watoto, wake na wengine ndio tegemeo katika familia zao. Anawalipia mafao hao vijana, na zaidi analipa kodi zaidi ya milioni 40 kwa mwaka. Sasa nijuze ni kijana gani msanii ambaye anafanya kazi zaidi ya Diamond? Ukifikiria hapo, basi utaelewa kwa nini wanasiasa na viongozi wanakwenda kutembelea WCB kila mara. Wana mambo mengi ya kujifunza kutoka WCB ili wakaweze kushare hayo mambo na vijana wengine wanaohangaika kujikwamua kimaisha. Ukiwa kiongozi, na ukawa na nia ya kusaidia wasaniii au jamii fulani, basi ni lazima ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa na ujifunze kutoka kwa waliofeli ili kusudi upate njia sahihi ya kuwasaidia wanaokwama.
 
Ben na majibu ya miili 7 kule Ruvu yamepatikana???
Yaani viongozi wa Afrika na hasa Tz. ni waajabu sana kufanya inappropriate duties and repsponsibilities with every thn is politics.
 
Ulitaka afanye nini ili ujue ana kazi ya kufanya? WCB wanachangia pato la taifa kiasi gani kwa mwaka ukilinganisha na pato unalochangia wewe? Unajua WCB imeajiri vijana wangapi wenye familia zinazowategemea?
kwa hiyo kazi ya waziri ni hiyo au kuna watumishi wa kitengo chake.na swala la Uchumi labda jamaa kaenda kukopa.

swissme
 
Back
Top Bottom