Wazungu wanavyohamasisha matendo ya kishoga kupitia kwenye series za Tv

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
Siku hizi imekuwa ni jambo la kawaida kukuta season inakuwa na kipande cha maigizo ya watu wa jinsi moja wakifanya matendo yanayoashiria kuwa ni ngono ya jinsi moja,mara nyingi waigizaji wengi huwa wanaigiza hasa vipande vya mapenzi ya mashoga na hata wakati mwigine hufikia hatua ya kuonyesha kabisa jinsi wanavyofanya mfano tazama season ya spartcus ,game of throne na nyingie nyingi.

Hii imekuwa ni jambo la kawaida na ajabu ni kwamba haijawai hata siku mojs serikali za Afrika achilia mbali ya Tanzania kukemea au kukataza tamthilia zenye maudhui hayo kuonekana tanzania.

Jambo hili linaenda sambamba na ukuaji wa mitandao ya kijamii na ueneaji wa intanet nchini.

ambapo walianza na season za kizungu na sasa wamehami kwenye season za kikorea na kihindi

Athari zake huenda ni pamoja na ile hali ya uoga waliokuwa nao vijana juu ya masuala haya kuanza kupungua na hata kufikia hivi sasa kuanza kuzoeleka ambapo vijana wa kiume wanajikuta wakifanya mapenzi bila kuogopa ile hali ya kufanana kimaumbile.

Uroboti huu ambao unasambazwa kwa kasi kubwa na tamthilia hizo madhara yake sahii yataanza kuja kujitokeza miaka 5 hadi 10 ijayo ambapo serekali za kiafrika zitajikuta zinashindwa kuzuia mienendo ya vijana wake na kujikuta wakikubali ushoga rasmi.

Je wewe ambaye uliwahi kutazama season yenye vipande hivyo vya ushoga unamchango gani katika hili?
 
Ndio mkuu, sanaa ya uigizaji inatumika sana kuinfluence tamaduni. Mambo kama ushoga yanakua influenced humo. Pia uhamasishaji wa tabia fulani ambazo zinalenga kuuza bidhaa za makampuni makubwa. Mfn unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara katika filamu unachangia biashara hizo kukua as u kniw matendo ya celebrities yanaigwa kwenye jamii.
 
Habari sana. Japokuwa sijawahi kushuhudia hayo maigizo. Ila najua kumekuwa na mpango mahusi ya dunia kuibadilisha kiutamaduni na kuishi maisha ya Sidoma na Gomora. Ila watu tumefungwa macho. Katika kusaini mambo ya haki fulani fulani kuna vipengele ambavyo hivyo vitu vinalazimisha kuwepo kwake na watu tunashabikia sana bila kujua madhara yake kwa vizazi vijavyo.
 
ushoga ni hulka ya mtu sio hiko unachosema
Sentesi fupi iliyobeba maana kubwaaa ......hili ndo jibu

Shoga ni tabiaa ya mtu hamna anayeshawishiwa kufanya kama hana hisiaa na hulka za ushogaa sp guys achen mambo ya kufikirikaa na imani za kale....wanaume mnakuwa waoga mpka kuangaliaa series eti kisa mnaogopa mtakuwa mashogaa khaaa!i wonder
 
Siku hizi imekuwa ni jambo la kawaida kukuta season inakuwa na kipande cha maigizo ya watu wa jinsi moja wakifanya matendo yanayoashiria kuwa ni ngono ya jinsi moja,mara nyingi waigizaji wengi huwa wanaigiza hasa vipande vya mapenzi ya mashoga na hata wakati mwigine hufikia hatua ya kuonyesha kabisa jinsi wanavyofanya mfano tazama season ya spartcus ,game of throne na nyingie nyingi.

Hii imekuwa ni jambo la kawaida na ajabu ni kwamba haijawai hata siku mojs serikali za Afrika achilia mbali ya Tanzania kukemea au kukataza tamthilia zenye maudhui hayo kuonekana tanzania.

Jambo hili linaenda sambamba na ukuaji wa mitandao ya kijamii na ueneaji wa intanet nchini.

ambapo walianza na season za kizungu na sasa wamehami kwenye season za kikorea na kihindi

Athari zake huenda ni pamoja na ile hali ya uoga waliokuwa nao vijana juu ya masuala haya kuanza kupungua na hata kufikia hivi sasa kuanza kuzoeleka ambapo vijana wa kiume wanajikuta wakifanya mapenzi bila kuogopa ile hali ya kufanana kimaumbile.

Uroboti huu ambao unasambazwa kwa kasi kubwa na tamthilia hizo madhara yake sahii yataanza kuja kujitokeza miaka 5 hadi 10 ijayo ambapo serekali za kiafrika zitajikuta zinashindwa kuzuia mienendo ya vijana wake na kujikuta wakikubali ushoga rasmi.

Je wewe ambaye uliwahi kutazama season yenye vipande hivyo vya ushoga unamchango gani katika hili?
siyo season pekee ata cartoon za watoto zina hayo mambo
 
Sentesi fupi iliyobeba maana kubwaaa ......hili ndo jibu

Shoga ni tabiaa ya mtu hamna anayeshawishiwa kufanya kama hana hisiaa na hulka za ushogaa sp guys achen mambo ya kufikirikaa na imani za kale....wanaume mnakuwa waoga mpka kuangaliaa series eti kisa mnaogopa mtakuwa mashogaa khaaa!i wonder
binafs nadhani mtoa mada ameelezea vizuri...kikubwa unachotakiwa kukitambua ni kwamba hao wanaotengeneza izo filamu hawalengi kukuhamasisha mtu mzima kam wew...wao wanadeal na kizazi kinachokuja, ebu fikiria watot wako wawe wanaangalia filam znazoshawish maswala ya ushoga unadhani watakua wanajfunza nn?!?!
usiseme tuu kwa wew kaa chini ufikirie na vizazi vnavokuwa muda huu hii hali inasikitisha sana...
 
Mtoto wa miaka 7-15 ataona jambo la kawaida kukung'utwa....ndo utakapoletewa posa mwanao wa kiume anaolewa
 
Kupambana na tabia mbovu ni jambo la kifamilia zaidi, hata serikali ikipiga marufuku haisaidii kitu kwani nyingi ya hizo series hazirushwi na TV za ndani bali watu wana download kwa internet na kuangalia kwenye simu/computer zao binafsi. Ni kama tu vile serikali kupiga marufuku bange lakini kila siku jani linasokotwa kama kawa, kama hautaki wanao wavute bange basi wape malezi bora kwenye ngazi ya familia
 
Upo sahihi mkuu. Hii ni campaign mahususi kabisa na wanamkakati wameamua kuitumia Hollywood kufanikisha azma yao.

Lengo lao hawataki wewe use shoga ila wanataka uzoee uone ni jambo la kawaida ili usiwakemee wala kuwashangaa wanaofanya.

Kizazi kijacho cha sisi wa Afrika kitafanya tu tr na bila woga na wala hakuna wa kuwakemea sababu wazazi wao tushaona ni jambo la kawaida na kulipinga ndio itakua ushamba.

Hali ni mbaya na hasa huko tuendako. Suluhisho ni kuwaweka wazo watoto na kuwaelimisha hasa kuitia mafunzo ya kidini yaweza kuwa ndio salama yetu.
 
Hivi kweny Series ya Arrow season ya mwisho yule dogo black mweny manywele alikuwa anafanya kazi Palmer technologies alikuwa punga eeeh?
 
ushoga ni hulka ya mtu sio hiko unachosema
Hulka ni nini? Ni tabia zinazojengwa kutokana na mazingira sambamba na mazoea. Endelea kuangalia hao mashoga wakifanywa until the day na ww utakapotamani kufany** ndo utajua kwa uhalisia kwamba hulka hujengwa na nini.
 
Niliona Hii Kitu Kwenye Series Zinazopendwa Duniani Kama
1. Da Vinc's Demons.
2. Empire
3. The Originals
4. G.O.T.
5. How To Get Away From Murder.

The List Goes On...
 
Hivi ni Seasons au ni TV Series..

by the way wazungu wanatumia kila njia na nguvu na akili nyingi sana kutuonyesha kuwa yale mambo ya ajabu ajabu kuwa ni ya kawaida na ndio matokeo yake sasa hivi TZ tuna vijana kama james delicious ..davitor and the likes
 
Back
Top Bottom