Wazungu wanatuhitaji kuliko tunavyowahitaji hakuna katika karne hii

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Katika karne hii AFRICA ni mdau mhimu wa nchi za ulaya na Marekani kuliko karne zilizopita, tunatambua kuwa rasilimali nyingi wameshamaliza rasilimali nyingi zimebaki katika bara la afrika.

Wazungu wanatuhitaji kuliko tunavyoahitaji kwa sasa. Nchi za Afrika zipunguze misaada kutoka ng'ambo kwani zitaweza kujisimamia wakati wa kujadili mikataba mbalimbali juu ya uwekezaji.
 
Tumechelewa sana kulitambua hili. Hivi sasa sehemu zote zenye neema ya rasilimali zimegeuka laana. Sehemu za migodi asilimia kubwa wameacha mashimo, sehemu za mafuta wameacha balaa la vita na mafuta yameharibu uoto wa asili kwa kumwagwa kwenye vyanzo vya maji. Mbuga za wanyama tumebakiwa na hadithi tu kwa sehemu kubwa. Wanyama wengi wako kwenye tishio la kutoweka ama wametoweka kabisa. Na sehemu kubwa ya rasilimali zetu tumewamilikisha kwa miaka 99.
Hivi Tanzania kwa mfano tuwakatae leo wazungu tutatumia rasilimali zetu kwa miaka mingapi?
 
Yah, tusimame tu tujiamini na twende nao sawa 50/50 mezani ili kukomboa walivyotuibia. Kila bargain ni hivyo hivyo alafu tuone kama hatujaheshimiana
 
Kila inapofikia kujadili kuhusu rasilimali za afrika, huwa nina stuck ghafla, nakosa points. Maana, kila ninachofikiri ni sahihi, huwa napata contradictions za kufa mtu.

Tatizo kubwa zaidi huwa ni wapi pa kuanzia.
 
Pa kuanzia ni wananchi tukubari kufunga mkanda tujenge uchumi wetu, km kwa mwezi tumeweza kukusanya trilion 1 sawa na pesa tulizonyimwa na mkoloni US. Fikiria mpaka sasa tunaagiza vijiti vya mishikaki na njiti za meno kutoka china pamoja misitu tuliyonayo. Wazungu wanahitaji uranium na gas kwa wingi, sisi tunavyo. Ukipokea msaada utashindwa ku bargain mikataba.
 
Kila inapofikia kujadili kuhusu rasilimali za afrika, huwa nina stuck ghafla, nakosa points. Maana, kila ninachofikiri ni sahihi, huwa napata contradictions za kufa mtu.

Tatizo kubwa zaidi huwa ni wapi pa kuanzia.

Tatizo kubwa ni woga wetu kuwa hatuwezi kujitegemea. lazima tujipange tukubari kujitesa kwa muda kidogo huku serikali ikisimamia mambo muhimu sana km afaya na elimu harafu mengine yatakuja baada ya kuweka mazingira vizuri.
 
Back
Top Bottom