Wazungu wameichoka CCM, Wasituletee ya Libya

Kiukweli kwa hali tunayokwenda nayo watu wa usalama wakae sana chonjo.Hali ya Zanzibar kwa mwendo tunaoenda nao tukienda kwa kulazimishana tuko hatarini.Dunia ya sasa ya wasomi haiingii akilini uchaguzi ufutwe na utangazwe mwingine ,na huku mwenye kufuta hana mamlaka ya kufanya hivyo na bado mkahubiri demokrasia.Kama walivyoshauri wanadiplomasia wazoefu ubabe hauwezi kusadia hata kidogo,katika suala la Zanzibar.Tufikie hatua tuone ni muhimu tutumie busara zetu,amani hii tuliyonayo kwa swala la Zanzibar iko mashakani.Hatutakuwa wajinga kama tukijishusha kwa mustakhabari wetu.Mazingira na Jiografia ya Zanzibar,tamaduni na itikadi ya eneo lote la bahari ya hindi si ishara nzuri kwa baadaye kama hakuna muafaka.

Kumbuka ikiwa huu uchaguzi wenye mizengwe ukifanyika,CUF watakuwa ni kama mbogo aliyejeruhiwa.CUF wana wafuasi wenye itikadi,uelewa na maono tofauti na bahati mbaya hata jicho kimataifa linaonekana kuwaunga mkono kwa kiasi kikubwa.Upo uwezekano mkubwa utawala wa Shein kwa miaka mitano ukawa mgumu,upo pia uwezekano Zanzibar ikiwa kituo cha uasi.Suluhisho hapa ni dogo kama chembe ya haladali-MUAFAKA,wenye tija na pengine wenye kushirikisha vyama vyote.Tuache ubabe,majuto ni mjukuu.
 
Wazungu wakikuchoka, na wakaamua kukupa live basi ujue kweli wanamaanisha, waulize Libya, Tunisia, Misri, sudan, afaghanstan, Osama, n.k
hawa watu ni mabingwa wa kutumia kosa dogo sana kupenyeza fujo kubwa ili kumuondoa yoyote waliyemchoka

Nchi hizo za kiarabu ulizotaja walitumia diaspora kama vibaraka wao wa kuleta hayo mapinduzi Libya,misri,tunisia nk Waliotumika kwenye zile vita ni wale raia waliokuwa nje ya nchi.Waliwaanda huko kwao wakawapa uraia baadaye wakashinikiza nchi hizo ziwe na uraia wa nchi mbili wakarudi nchi hizo na kombati na maguruneti wakaanza vurugu na mapinduzi.Tanzania pia kulikuwa na mchakato huo wa kutaka kuwepo uraia wa nchi mbili lengo ni kuwa na madiaspora ambayo yangetumiwa kwa maslahi yao kuja kuleta za kuleta kama walivyoyatumia hayo ma-diaspora nchi hizo za kiarabu.

Uzuri pamoja na propaganda zote za vibaraka wa ndani ya serikali,bunge na nje, Serikali ilikataa na wabunge wakalipiga chini kuwa uraia wa nchi mbili OUT hatutaki.

Ulinzi wa Tanzania ni wa kila Mtanzania Sio TISS peke yake.Kila mtanzania ajione kama TISS kuilinda na kuitetea nchi yake dhidi ya kila njama ya siri na wazi iwe ya wazungu au vibaraka wa wazungu walioko vyama vya upinzani,CCM,serikalini au POPOTE.
 

Nimeisikiliza hotuba ya Mugabe, hakulitaja jina la Kikwete na maana halisi si hiyo hapo juu ya kile Mugabe alichozungumza. Hata hivyo, kuna tofauti ya CCM na nchi tajwa hapo juu. CCM wanabadilisha uongozi wakati katika nchi tajwa hapo juu, viongozi ni wale wale.
 
We utakuwa aidha umerogwa au UKAWA.
 
mkuu hao raia walipata wapi silaha nzitonzito zile
 

kwa iyo Mkuu ina maana kuwa viongozi wanaotawala wafanye wanachotaka hata kujiingiza katika mambo yanayovuruga amani kwa kutegemea vyombo vya Usalama??? KAMA NI IVYO NAONA NI KUJIINGIZA KATIKA MATATIZO YASIYO YA LAZIMA
 
Hivi tiss watawafanya nn wazungu kwa mfano? Unachekesha kweli
 
HUKUSIKIA JINA LA KIKWETE??????????????
 
Kuna watu tena wengi na hasa wale 'inner circles' wa ccm wanaamini kabisa na kwa kwa dhati kuwa Tanzania ni nchi ya amani na haitakaa ivurugike. Hata pale unapowaeleza kuwa amani ya Tanzania ni misingi kidogo ya haki aliyoianzisha Mwalimu na ili iendelee kusimama inahitaji kuendelezwa hawaamini hata hilo!
Kumbukumbu zinaonyesha kwamba miaka ya sabini na themanini nchi kama Zaire, Ivory Coast zilikuwa 'ulaya ndogo' na kilichozivuruga ni viongozi wake kuelemewa na shibe. Hata hapa ukiangalia video clips nyingi za wanasiasa hasa kutoka chama tawala juu ya suala la amani na Zanzibar unagundua ni shibe iliyopitiliza na ndio maana wengi wanamwaza JPM bila huku wakisahau kidogo kuwa naye ni 'mwenzao'.
 
Bora aliyelogwa na anaona ccm hawafai kuliko wewe ambae hujalogwa na unaona ccm inafaa kwani ni tatizo la akili na ufahamu mdogo!
Barikiwa mkuu kwa jina la Yesu Mungu alie hai kana CCM haifai njoo hapa uhamiaji ulizia haa mym ninatoa passport buree kwenda Kongo,Syria,Libya,Sudan Kusini na Afrika ya kati buree kabisa na nauli nakupa ukapumzike na kero za CCM ili Lowasa akiwa rais urudi.
 
Mbona north Korea wamweza kufight kiasi na propaganda za western na sasa wanawashikiria RAIA wamarekani wa3 na wamekiri makosa yao kwa nini ishindikane TZ.
 
Duh, elimu elimu elimu, hivi unategemea itapigwa ccm pekee? Nilidhan walio jf wako vizuri upstairs kumbeee sivyo
Mkuu tupo tunaojiekewa wasikutishe hao vijana wa miaka ya 95+kichwani horobo shule hawakutaka wanafanya kazi ngumu mshahara mdogo afu wana wanawake wazee hasira zao zote wanamaluzia mitandaoni na vitecno vyao vya bure.
 
Pamoja na kuwa kila mtu ameichoka CCM kwa kkiwango kikubwa lakini hayo unayoyataka yatokee ni ya hatari zaidi....amani ikipotea yatakuwa ni majuto makuu siyo tu kwako bali mpaka kwa vizazi vyako......bado tuna nafasi ya kurekebisha mambo katika nchi katika njia ya amani kuliko kuanzisha fujo ambazo madhara yake ni makubwa kuliko unavyodhani......

Kwa kiasi kikubwa sana raia wa Libya wapo kwenye majuto makuu hata yale madogo waliyokuwa wakiyadharau sasa hayapatikani....ni muendelezo wa mauaji na kila aina ya unyama...
 
Asante sana
 
Ni ujumbe mzito sana mkuu, majuto ni mjukuu na ninge huja baadaye sana. Mungu ibariki Tanzania
 
Mkuu tupo tunaojiekewa wasikutishe hao vijana wa miaka ya 95+kichwani horobo shule hawakutaka wanafanya kazi ngumu mshahara mdogo afu wana wanawake wazee hasira zao zote wanamaluzia mitandaoni na vitecno vyao vya bure.
[emoji1] [emoji1] haya mkuu, hawa vijana wamezidi kuchukulia poa kila kitu
 
Mbona north Korea wamweza kufight kiasi na propaganda za western na sasa wanawashikiria RAIA wamarekani wa3 na wamekiri makosa yao kwa nini ishindikane TZ.
Back ground ya Noth Korea huwezi kuifananisha na Tanzania hata kidogo wakati wa economic criss ya 1990 waliopitia North Korea baada ya USSR kusambaratika ilibidi watafute alternative ways ya kupata pesa kwa ajili ya kuendesha nchi yao na pesa wanazopata ni nyingi zinatokana na illegal means kama producing and smuggling drugs, smuggling Elephant ivory, selling weapons and nuclear tech middle east ,operating casinos in China unofficial nakadhalika ,sasa sisi ambao uchumi wetu unategemea pombe na sigara ,madini tu kuchimba hatuwezi mpaka na udongo unasafirishwa Ulaya na Marekani unategemea nini ????
Tunawakwepa vipi WB na IMF ??
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…