Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,858
Waafrika tunataka kuanzisha ugomvi wa mawe wakati tunaishi kwenye nyumba ya vioo.Wazungu wakitujibu na kusema ukweli tutakuwa wapole na kujiona sisi si kitu.
Kwa mfano,ukimuuliza Mugabe ndege iliyomfikisha Addis Ababa imetengenezwa na Waafrika au Wazungu atakuwa na jibu gani?
Tujiuluze tu hata lugha zetu za kiafrika sisi wenyewe tunazithamini?Mbona karibu kila mahali barani Afrika ni kingereza na kifaransa tu?Wakitubeza kwa kushindwa hata kuthamini lugha zetu tutawajibu nini?Hata hiyo speech Mugabe kaitoa kwa lugha gani?
Nchi ya kiafrika ikikumbwa na njaa,huwa hatusubiri wazungu watusaidie?
Janga la Ebola huko Afrika Magharibi ni kina nani walitoa fedha kusaidia kukabiliana na tatizo hilo?
Viongozi wa kiafrika wakiiba hela katika nchi zao huficha katika nchi nyingine za kiafrika au huficha katika nchi za Ulaya?Wazungu wakilisema hili na kutudharau watakuwa wametuonea?
Jamani,yako mengi sana ya aibu kuhusu sisi wa Afrika na ndio maana wanatudharau hivyo ni bora kwanza tukajirekebisha kabla ya kujitia kimbelembele.
Tulichofanikiwa Waafrika ni kutoa wacheza soka tu kwenda Ulaya ila mambo mengine yote yametushinda ikiwa ni pamoja na hata kujitawala wenyewe kwa wenyewe.Hata DEMOKRASIA TU IMETUSHINDA!
Ngozi nyeusi ni shida kwani hata hizi dini zetu bado zimetoka kwa hao wazungu na hata video za Yesu zinaonyesha Yesu si mtu mweusi.
Alafu hata wapigania uhuru wa nchi za kiafrika walisomea nchi gani na kwa msaada wa watu gani zaidi ya hao wazungu?
Mugabe na vingozi wengine wa Kiafrika mpaka leo hii wanatibiwa na kufia Afrika au Ulaya?
Waafrika tunatafuta usawa kwasababu za kibinadamu tu lakini sio kwasababu za kuwa na viwango(standards)-hivi ndivyo mimi ninavyoamini na nitaendelea kuamini hivyo mpaka siku naingia kaburini.
Tujisahihishe kwa mengi kabla ya kuanza kubwabwaja na kutafuta usawa.
NB:Nyie mnaonishambulia nijibuni swali hili dogo tu: Hivi siku yenu ya kuzaliwa au ya watoto wenu ikifika na mkakusanyika pale sebuleni, ule wimbo maarufu wa siku ya kuzaliwa (birthday),huwa ni wa lugha gani?Wa lugha yetu uko wapi?