Wazungu hawajawahi kutuacha salama

CARIFONIA

JF-Expert Member
Aug 17, 2013
518
901
Habari zenu jamani, bila kuwachosha sana ngoja niende moja kwa moja kwenye hoja yangu.

Kuna msemo mmoja wa kiswahili usemao usimtukane mamba kabla ujavuka mto, kitu ninachokiona kwa sasa ni kama hawa jamaa walienda maabara kui-upgrade hii kitu inaitwa corona.

Afrika tulijipiga kifua sana kuhusu huu ugonjwa kwamba autakua na madhara makubwa kwetu, kitu nachokiona kwa sasa ni kama huu ugonjwa unarudi kwa kasi ya tsunami sasa sijui ndio second wave, Kenya, Madagascar, South Africa, Zambia hali ni tete.

Naomba tu Watanzania tusijiachie sana kihivyo kwani mabeberu hayajafurai kwa sisi kuwa salama nadhani walikua wanajipanga kuja kutuonyesha corona bado ipo.
 
Kwa wanaofuatilia kwa ukaribu haya mambo wala hawawezi kushangaa haya mambo kwa sababu for months now, wamekuwa wakizungumzia suala la second wave! Na hili la second wave lilitabiriwa baada ya watu kuanza kufanya masihara!

Kuna Msukule mmoja wa Lumumba hapa juzi tu hapa akahoji eti kama huu ugonjwa upo kihivyo, mbona hujaleta athari US baada ya maandamano... yaani anasema haya huku akiwa hafahamu it's a matter of time kabla baadhi ya states hazijaanza ku-implement tena lockdown baada ya maambukizi kuanza ku-shoot upya!
 
Chige,
Halafu kama kule kwao mambo kama yameaza kukaa sawa wakati picha huku kwetu ndio kama linaanza upya.
 
halafu kama kule kwao mambo kama yameaza kukaa sawa wakati picha huku kwetu ndio kama linaanza upya

Mkuu, unaongea nini? Jana mpaka saa tano na nusu za usiku wameshakufa 700 na kidogo huko marekanj, ikifuatiwa na mexico, india na brazil. Kwenye bara letu afrika ya kusini ndio wanakufa zaidi, ikifuatiwa na egypt japo kwao imepungua kidogo.

Corona ipo na itaendelea kuwepo, na watu wanakufa, so twendelee kujihadhari zaidi, japo wengi wamepuuza masharti.
 
Halafu kama kule kwao mambo kama yameaza kukaa sawa wakati picha huku kwetu ndio kama linaanza upya
Ulaya mambo yameanza kukaa sawa lakini US mambo yamegeuka!! Na nani atashangaa US mambo kugeuka wakati rais mwenyewe amejawa kiburi huku wafuasi wake wakipinga kwa nguvu zote suala la uvaaji wa barakoa!

American Arrogance inawaponza!!
 
Back
Top Bottom