Wazungu bwana, wanajifanya wana huruma sana

Wazungu bwana, wanajifanya wana huruma sana

Huyo kazoea kwao Ulaya njiwa mpaka wanakudandia, homeboy ungewawinda


Alexander The Great
 
Nilibahatika kupata kazi sehemu ya shamba boy kwa mzungu,sasa lile eneo lilikuwa na vindege vingi sana,siku moja yaani ni siku Tisa kwanza nimepata kazi nikawa nimepika ugali na nilishapanga kuwa kunitapiga ndege,nilie ugali,nikawa na manati,kweli nikaanza kulenga vile vindege.

Nilikuwa na shabaha kila nikilenga sikosi,kumbe yule mzungu alikuwa ananichungulia dirishani, Mara akashuka akanigea elfu ishirini na tano,nikaona huenda amependezwa kuona nina shabaha sana.

Na Mimi kumuonyesha kuwa mimi ni hatari kesho yake ikawa kama jana mwendo wa kulenga ndege,jiwe ndege sikosi.

Mara naona walinzi wananifuata na kuniambia nitoke nje ya geti, mzungu hataki kuniona eti pamoja na kunipa hela ya kula Jana bado nimeendelea kuua ndege.

Sasa swali nauliza kwani ndege wale wa kwake hadi aumie,nimepanga kuweka mwanasheri amevunja mkataba na anilipe.
Waafrika hawana huruma hata kidogo. Kuna kijana mmoja alikuwa anawinda ndege mzungu mmoja akamwona akamwonea huruma kwa sababu ya umaskini wake yule mzungu akampa yule kijana 25,000 akifikiri yule kijana angeacha kuwinda wale ndege adimu. Chakushangaza yule kijana akataka kumfungulia yule mzungu kesi akidai anaingilia uhuru wake na anavunja mkataba!
 
Ni kweli ana huruma maana ningekuwa mimi ningechonga manati nikakulenga matakoni
 
Mzungu yupo sahihi!!

Kwa sababu umesema una shabaha yaani 'ukilenga hukosi' siku hao ndege ungemaliza kuwalenga wote basi hiyo manati ingetumika kumlenga mzungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom