Wazo: Yanga family day carnival "Mtoko wa kibingwa"

ndo vile

Member
Mar 11, 2023
25
12
YANGA FAMILY DAY CARNIVAL, MTOKO WA MABINGWA
Uendeshaji wa kisasa wa mpira wa miguu, haushii kwenye timu kusajili vizuri na kupata matokeo uwanjani. Matukio ya nje ya uwanja yanayofanywa na timu yamekuwa na manufaa na mvuto mkubwa sana kibiashara kwasababu wapenzi na mashabiki wa mpira wa zama hizi wamekuwa wafuatiliaji wazuri wa matukio ya timu zao nje ya uwanja, jambo ambalo limeleta fursa nyingi mpya za kibiashara na kuzifanya timu kupata mapato,kujitangaza na kuvuna mashabiki wapya.

Nchini Tanzania timu ya Yanga imekuwa na utamaduni wa kufanya matukio mbalimbali yenye mlengo wa kusaidia jamii na kurudisha tabasamu kwa makundi yenye uhitaji,timu ya Yanga imekuwa ikitoa misaada ya kibinadamu kwenye vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika kila mkoa wanapokwenda kucheza,pia imekuwa ikishiriki kwenye matukio ya uhamasishaji kama uhamasishaji wa uchangiaji wa damu,uhamisishaji wa usafi n.k.Utamaduni huu wa Yanga kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya nje ya uwanja yamesaidia kujenga taswira chanya ya timu kwa jamii,kuvuna mashabiki wapya,na kuongeza uhusiano mwema kati ya timu na mashabiki.

Katika miaka ya hivi karibuni timu ya Yanga imefanya uwekezaji mkubwa mkubwa sana kwa kusajili wachezaji wenye ubora pamoja na kuajiri benchi la ufundi lenye ubora jambo ambalo limesaidia kurejesha furaha ya wapenzi na mashabiki wa Yanga iliyokuwa imepotea,timu ya Yanga imefanikiwa kuvunja rekodi kwa kucheza zaidi ya mechi 40 za ligi ya nyumbani pasipo kupoteza mchezo wowote,pamoja na furaha walionayo mashabiki na wapenzi wa Yanga kwa sasa bado hakuna jukwaa maalumu la kuwakutanisha mashabiki na wapenzi wa Yanga wakiwa na familia zao nje ya uwanja ili waweze kusherekea mafanikio ya timu yao.

YANGA FAMILY DAY CARNIVAL MTOKO WA MABINGWA
Ni siku maalumu kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya Yanga wakiwa na familia zao kukutana na kusherekea kwa pamoja mafanikio ya timu yao,siku hii yenye kauli mbiu ya “MTOKO WA MABINGWA’itatoa fursa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya Yanga kukutana na viongozi,wachezaji na benchi la ufundi na kusherekea kwa pamoja mafanikio ya timu yao pia kubadilishana uzoefu na mawazo. Kwa kupitia siku hii mashabiki,wapenzi,viongozi,wachezaji na benchi la ufundi wa Yanga wakiwa na familia zao watapata wasaa wa kufahamiana,kuburudika,kupeana michongo huku wakisherekea mafanikio ya timu yao pendwa ya Yanga,pia siku hii ni muhimu kwa timu ya Yanga kupata mapato kwa kupitia viingilio na uuzaji wa jezi.

MATUKIO KATIKA YANGA FAMILY DAY CARNIVAL#MTOKO WA MABINGWA
Burudani za mziki kutoka kwa djs,live band,na wasanii wa kizazi kipya,
Michezo ya watoto,
Vinywaji na chakula,
Photo shoot, kupiga picha na wachezaji, viongozi na benchi la ufundi,
Celebrate appearance,

Big screen zitazokuwa zinaonyesha mechi mbalimbali za Yanga haswa tulizowafunga makolo,
Uuzwaji wa bidhaa zenye nembo ya Yanga,
Usajili wa mashabiki wa Yanga kidijitali.

FAIDA ZA YANGA FAMILY DAY CARNIVAL, MTOKO WA MABINGWA

Timu kupata mapato kupitia wadhamini,viingilio,na uuzwaji wa bidhaa zenye nembo ya Yanga.
Umoja na mshikamano kati ya mashabiki,viongozi na wachezaji kuongezeka mara dufu.
Kuongezeka kwa idadi ya mashabiki waliosajiliwa kidijitali.
Uwezekano wa kuvuna mashabiki wapya,haswa kundi la watoto.
Fursa kwa mashabiki kukutana kubadilishana uzoefu,mawazo na kupeana michongo.

NAWASALIMU KWA JINA LA YANGA NA MAKOMBE YAENDELEE
 
YANGA FAMILY DAY CARNIVAL,#MTOKO WA MABINGWA#
Uendeshaji wa kisasa wa mpira wa miguu,haushii kwenye timu kusajili vizuri na kupata matokeo uwanjani.Matukio ya nje ya uwanja yanayofanywa na timu yamekuwa na manufaa na mvuto mkubwa sana kibiashara kwasababu wapenzi na mashabiki wa mpira wa zama hizi wamekuwa wafuatiliaji wazuri wa matukio ya timu zao nje ya uwanja, jambo ambalo limeleta fursa nyingi mpya za kibiashara na kuzifanya timu kupata mapato,kujitangaza na kuvuna mashabiki wapya.
Nchini Tanzania timu ya Yanga imekuwa na utamaduni wa kufanya matukio mbalimbali yenye mlengo wa kusaidia jamii na kurudisha tabasamu kwa makundi yenye uhitaji,timu ya Yanga imekuwa ikitoa misaada ya kibinadamu kwenye vituo vya kulelea watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu katika kila mkoa wanapokwenda kucheza,pia imekuwa ikishiriki kwenye matukio ya uhamasishaji kama uhamasishaji wa uchangiaji wa damu,uhamisishaji wa usafi n.k.Utamaduni huu wa Yanga kushiriki kwenye matukio mbalimbali ya nje ya uwanja yamesaidia kujenga taswira chanya ya timu kwa jamii,kuvuna mashabiki wapya,na kuongeza uhusiano mwema kati ya timu na mashabiki.
Katika miaka ya hivi karibuni timu ya Yanga imefanya uwekezaji mkubwa mkubwa sana kwa kusajili wachezaji wenye ubora pamoja na kuajiri benchi la ufundi lenye ubora jambo ambalo limesaidia kurejesha furaha ya wapenzi na mashabiki wa Yanga iliyokuwa imepotea,timu ya Yanga imefanikiwa kuvunja rekodi kwa kucheza zaidi ya mechi 40 za ligi ya nyumbani pasipo kupoteza mchezo wowote,pamoja na furaha walionayo mashabiki na wapenzi wa Yanga kwa sasa bado hakuna jukwaa maalumu la kuwakutanisha mashabiki na wapenzi wa Yanga wakiwa na familia zao nje ya uwanja ili waweze kusherekea mafanikio ya timu yao.
YANGA FAMILY DAY CARNIVAL#MTOKO WA MABINGWA#
Ni siku maalumu kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya Yanga wakiwa na familia zao kukutana na kusherekea kwa pamoja mafanikio ya timu yao,siku hii yenye kauli mbiu ya “MTOKO WA MABINGWA’itatoa fursa kwa mashabiki na wapenzi wa timu ya Yanga kukutana na viongozi,wachezaji na benchi la ufundi na kusherekea kwa pamoja mafanikio ya timu yao pia kubadilishana uzoefu na mawazo. Kwa kupitia siku hii mashabiki,wapenzi,viongozi,wachezaji na benchi la ufundi wa Yanga wakiwa na familia zao watapata wasaa wa kufahamiana,kuburudika,kupeana michongo huku wakisherekea mafanikio ya timu yao pendwa ya Yanga,pia siku hii ni muhimu kwa timu ya Yanga kupata mapato kwa kupitia viingilio na uuzaji wa jezi.
MATUKIO KATIKA YANGA FAMILY DAY CARNIVAL#MTOKO WA MABINGWA#
Burudani za mziki kutoka kwa djs,live band,na wasanii wa kizazi kipya,
Michezo ya watoto,
Vinywaji na chakula,
Photo shoot,kupiga picha na wachezaji,viongozi na benchi la ufundi,
Celebrate appearance,
Big screen zitazokuwa zinaonyesha mechi mbalimbali za Yanga haswa tulizowafunga makolo,
Uuzwaji wa bidhaa zenye nembo ya Yanga,
Usajili wa mashabiki wa Yanga kidijitali.
FAIDA ZA YANGA FAMILY DAY CARNIVAL,#MTOKO WA MABINGWA#
Timu kupata mapato kupitia wadhamini,viingilio,na uuzwaji wa bidhaa zenye nembo ya Yanga.
Umoja na mshikamano kati ya mashabiki,viongozi na wachezaji kuongezeka mara dufu.
Kuongezeka kwa idadi ya mashabiki waliosajiliwa kidijitali.
Uwezekano wa kuvuna mashabiki wapya,haswa kundi la watoto.
Fursa kwa mashabiki kukutana kubadilishana uzoefu,mawazo na kupeana michongo.
NAWASALIMU KWA JINA LA YANGA NA MAKOMBE YAENDELEE
Lini hyo
 
Yanga hawana akili ya kuanzisha chochote wao wanasubiria simba aanzishe ili waige lakini kwanza wataanza kuponda lakini baadae wanaiga kweli kama una mtoto umzuie asiwe yanga maana akili zao wanazijua wenyewe.
 
Ndo maana mnaitwa makolo
 
Back
Top Bottom