Wazo: Wajumbe wa kamati za makinikia wanastahili nishani ya kitaifa!

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,840
2,000
Hili ni wazo langu kuwa wajumbe wote wa kamati hizi mbili zilizoundwa kuchunguza wizi wa rasilimali zetu watunukiwe nishani ya kitaifa ili kuenzi uzalendo wao kwa nchi.

Wajumbe hawa wamejitunza kwa kutokukubali kulaghaiwa.

Wajumbe hawa wanerisk na wataendelea kurisk maisha yao kwa manufa ya Taifa.

Wajumbe hawa wameitendea haki ekimu yao na gharama zilizotumika kuwasomesha.
 
Mfukua Makaburi

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,042
2,000
Subiri kwanza tuone matunda/matokeo ya kazi zao, sio hizi nadharia walizotuletea za kumdai mtu milioni moja wakati yeye uwezo wake ni shilingi elfu moja.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,840
2,000
Subiri kwanza tuone matunda/matokeo ya kazi zao, sio hizi nadharia walizotuletea za kumdai mtu milioni moja wakati yeye uwezo wake ni shilingi elfu moja.
Nani aliyekwambia uwezo wake ni mdogo kuliko anachodaiwa?yaani kajipimia mwenyewe uwezo na unamuamini?
 
Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Kuna mwingine wanataka kumpongeza wakati ameshindwa kuelewa hata "win-win situation"
Anasema wamekubali kulipa pesa yetu yote!
Sijui nae apewe zawadi gani?
Kwani kihere here cha kupongezana cha nini wakati hata matunda bado?
[HASHTAG]#NasubiriNoahYangu[/HASHTAG]
 
Ngangari

Member
Sep 6, 2013
42
125
Subiri kwanza tuone matunda/matokeo ya kazi zao, sio hizi nadharia walizotuletea za kumdai mtu milioni moja wakati yeye uwezo wake ni shilingi elfu moja.
Tuvute subira tuone impact ya kazi yao, inaweza kuwa positive au negative kwenye uchumi wa nchi na uwekezaji kwenye sekta ya madini kwa ujumla. Muda ni mwalimu mkubwa. Baadhi ya watu wanahofu tunaweza kuwa kama zimbabwe miaka michache ijayo. Ikitoke, tuwanyanganye nishati? Twende kwa subira
 
Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
9,621
2,000
Hili ni wazo langu kuwa wajumbe wote wa kamati hizi mbili zilizoundwa kuchunguza wizi wa rasilimali zetu watunukiwe nishani ya kitaifa ili kuenzi uzalendo wao kwa nchi.

Wajumbe hawa wamejitunza kwa kutokukubali kulaghaiwa.

Wajumbe hawa wanerisk na wataendelea kurisk maisha yao kwa manufa ya Taifa.

Wajumbe hawa wameitendea haki ekimu yao na gharama zilizotumika kuwasomesha.
Sasa mbona hatupatiwi hizo nakala za taarifa nzima?
 
UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,724
2,000
Wakati wamecopy na kupest chunguzi zilizopota yaani kuanzia ya Mboma nk"in Lissu's voice"
 
Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,211
2,000
Jamani mbona hatuwaamini wataalamu wetu waliochunguza hili sakata? halafu watanzania wapumbavu sana, yaaan wanadhani kuwa eti kwa kuwa mtaji wa Barrick ulikuwa Trilioni mbili kuwekeza hapa nchini na sisi kuwadai hiyo zaidi ya Trilioni 100 eti ni maajabu ya dunia...! Mungu wangu? hivi mnajua uchumi ulivyo?

Barrick tayari walisharudisha gharama zao za mtaji zamani sana, na sasa wanakula tu faida zaidi, ukitaka kujua hili, fuatilia report zao za kugawana share kwa miaka kadhaa, utashangaa sana,

Unajua watanzania wameathiliwa na umasikini hadi kwenye ubongo, hivyo wakisikia hiyo Trilioni 100+ hawaamini kama kweli Barrick wanaweza kuwa wanadaiwa hicho kiasi, hii ni kwa sababu ya mentality ya umasikini tulionao, hivo kutokujiamini wakati wote.

Kuna kitu kitajitokeza ambacho hamtakaa muamini, naomba kila mtu atunze record hii.

ACACIA alikuwa anamdanganya BARRICK kwa taarifa mbalimbali alizokuwa akimpa huyo mbia mwenzake, usidhani kuwa BARRICK hajui nini kinachoendelea.

Ni kama vile Tanzania imemfumbua macho BARRICK na kumwambia angalau hapa na wewe unaibiwa na ACACIA.

wizi wa ACACIA ulibase katika, Underdeclaration ya idadi ya makontena ya makinikia kwa BARRICK na kwa Hapa TANZANIA.

Kiwango cha mapato yatokanayo na hayo makinikia kilikuwa kinafichwa kwa BARRICK na Tanzania.

Risiti za malipo ya kodi na vitu vingine kutoka ACCACIA kwenda serikalini ni tofauti na risiti kutoka ACACIA Kwenda BARRICK.

Tulieni, nimewafumbua tu macho ili kuwaandaa kisaikolojia wale wengine.
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,689
2,000
Kama ile kamati iliyowang'oa kina Kalamagi haikupewa hiyo nishani itakuwa hii ha mchanga wa pwani!!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom