Wazo: Tuchangie na kuunganisha nguvu kuiangusha CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo: Tuchangie na kuunganisha nguvu kuiangusha CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jews4ever, Aug 13, 2009.

 1. J

  Jews4ever Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele wakuu!
  Nathamini sana michango yenu katika jamii ya Tanzania.


  Wadugu,uchaguzi unakaribia,imekua ni mazoea kama sio utamaduni,
  kuona jukumu la kupiga kura linachangiwa kwa kiasi kikubwa na
  wenzetu wanaoishi vijijini huku sisi tuliopata nafasi ya kuona mwanga wa elimu na dunia kwa ujumla tukitoa maoni ya nani hafai,anaboa,n.k


  1.Sisi tuliopo ughaibuni, mnaonaje tukianzisha kampeni maalumu ya kitaifa
  na kimataifa kutafuta fedha za msaada kama michango, ili tuwezeshe wasio na fedha za kutosha wajumuike nawe mwenye uwezo mzuri kifedha kurudi nyumbani kwaajili ya kupiga kura ya ushindi?


  2.Kuepuka gharama hizo, ni kupata fursa ya kupiga kura tukiwa nje ya nchi,
  je kwa miezi iliyobaki tunawezafanikisha jambo hili?


  Tazama uzuri wa nchi unaoishi sasa, ni matunda ya mkakati mzuri waliojiwekea waasisi wa mataifa hayo,yamkini hatua zao za mwazo kabisa ktk mapambano zilikuwa katika level inayofanana na pendekezo kama hili.

  Ni lini basi tutatoka katika uongozi huu wa mafisadi,wezi,wenye chuki,usiopenda wala kuthamini nchi na watu wake?

  Chukua hatua, pamoja tunaweza.

  Pole kwa waliokwazika!

  Naomba kutoa hoja.

   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hii siyo breaking news!
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Na wewe ni mmoja ya wale wanaona tatizo ni CCM..!!

  Kabla ya kuangalia kuiangusha CCM kitaifa....Hebu anza na kazi rahisi kwanza ya kuiangusha CCM kwenye familia yako yote iliyopo Tanzania; wasiipigie kura CCM.

  Ukifanikiwa utakuwa umefanikiwa lengo lako kwa kiasi kikubwa sana.

  Kila la kheri.
   
 4. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Mhh,mwaka huu tutapata mawazo mengi kweli jamani....
   
 5. M

  MC JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wazo zuri, lakini haliwezi tekelezeka kwa stail unayoshauri wewe! badala ya kuongelea kuchangishana pesa ni bora tuhamasishe watu wajiandikishe na washawishi ndugu, jamaa na marafiki kujiandikisha,

  Kisha watu waelezwe Umuhim wa kupiga kura, na kwa walio Nje wawe na stragegic plan ambayo uchaguzi ujao utawakuta TZ (of course not possible for all, but at least...)
   
 6. S

  Shamu JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza jiulize: Ukiiondoa CCM madarakani unataka chama gani kiongoze nchi na nani awe Rais? Pili: Wapinzani unaotaka wewe waongoze nchi ni Wajamaa. Vyama vyote vya upinzani bongo vina kampeni za Ujamaa. Wanaamini Serikali inaweza kutatua matatizo ya Wananchi wote wa WTZ. Sasa jiulize, unataka UJAMAA urudi bongo? No way.
  What we need is Conservative way. Government efficient, less government, less tax, and let the market solve the problem.
   
 7. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2009
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Una wazo zuri la kutaka mabadiliko, ila siamini kwamba kuiondoa tu CCM madarakani ndo njia ya kujihakikishia maendeleo, kwani upinzani kuna watu gani wa kuingoza nchi kutoka upinzani? Watu wenye uwezo wa kuiongoza jamii ya watanzania mmekwenda ugaibuni na hamtaki kurudi. Hali ya vijijini ni mbaya kuliko mnavyofikiria nyie kuna umasikini mkubwa sana wa kipato na wa taarifa! umasikini wa taarifa ndo unotumaliza watanzania wananchi wanangia kwenye uchaguzi wakiwa hawana taarifa sahihi ni nani anafaa kuchaguliwa watu mliosoma mmeasi hataki kwenda kuwaonyeshe njia watu wa vijijini mmekaa mijini na ugaibuni kuendesha magari ya kifahari na kujirusha halafu watu wa vijijini wakichagua viongozi wabovu mmawalaumu. Ninyi wasomi wa tanzania mmefanana na na yule mtu alipewa chakula chote cha familia ale ili awe na nguvu aende kijiji cha mbali kuleta chakula yeye alipofika huko akalowea akawasaliti ndugu zake! Wasomi twendeni kwenye vijiji tukaelimishe watu tusibaki kulaumu CCM, CCM siyo tatizo tatizo ni watu! Changisha hizo fedha mje bongo tufanye outreach ya nguvu kabla ya uchaguzi tunaweza kubadili hali iliyopo sasa!
   
 8. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duh, hii imetulia sana, mimi naomba niwe mshika pesa!!!
   
 9. F

  Fungu la kukosa Member

  #9
  Aug 16, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa nakupongeza ewe Mtanzania mwenzangu uliye ughaibuni kama mimi kwa maoni yako mazuri ya kutaka tuiangushe CCM na kukipa ushindi chama ambacho kitakuwa tayari kutuletea maendeleo hapo bongo kama haya tuyaonayo huku ughaibuni(majuu- ulaya na America). Hiyo, inawezekana kabisa kama tutaungana na wenzetu wapenda maendeleo waliopo huko nyumbani Bongo.Lakini wasi wasi wangu ni Chama kipi cha kukichagua dhidi ya CCM? Vyama vyote vilivyopo kwa mtazamo wangu ni kama CCC:B. Vipo kwa ajili ya kupata ruzuku na si kwa ajili ya upinzani wa kweli. Kama kweli vyama vya upinzani Bongo vipo makini kuiondoa CCM madarakani, mbona haijatokea hata chaguzi moja vyama hivyo kuwa na agenda ya kuunganisha nguvu zao dhidi ya CCM. Kila chama cha simama kivyake na hivyo kupoteza maana halisi ya upinzani. Ni vizuri tukijifunza kutoka kwa wenzetu wa Kenya na Zimbabwe, kwa mtazamo wangu katika nchi hizo kuna afadhali kidogo ya kuwepo kwa mshikamano wa kisiasa miongoni mwa wapinzani ukilinganisha na Bongo.Labda Mungu ashushe Malaika toka mbinguni kuindoa CCM na siyo akina Lipumba,Mbowe wala Mtikila. Hata kama watachukuwa nchi, kitu cha kwanza watachfanya ni kujilimbikizia mali kama wafanyavyo Mafisadi wa CCM, kisha ndipo wa waangalie walala hoi,kwa kuwanadia sera za kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Wabongo ni wa Bongo tu.
   
Loading...