DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,986
- 3,151
Kwanza kabisa ningependa kuunga mkono hoja ya kuwa na chombo mahususi cha kitaifa cha vijana kwa ajili ya kuweza kuongelea mabo mbalimbali yahusiyo vijana na kuishinikiza serikali nini kifanyike kwa ajili ya vijana, hoja ambayo kama sijakosea Mh. Mnyika alisema atapeleka hoja binfsi bungeni.
Tatizo la ajira limekuwa ni tatizo kubwa sana siku hadi siku hasa kwa vijana kwani ndo nguvu kazi kubwa ya taifa lakini pia ndo idadi iliyokubwa ukilinganisha na wazee. kuna sababu ni nyingi sana zinazochangia kukua kwa tatizo hili, ila binafsi nisingependa kuzieleza lengo langu hasa ni kuhusiana na hizi interview ambazo mwombakazi anatakiwa afanye kama njia ya kumpima uwezo wake na mambo mengine mengi.
Kwa mawazo yangu mimi ni bora serikali kupitia wizara ya kazi ingetunga sheria inayodhibiti makampuni, mashirika au wajiri mbalimbali wawe ndiyo wawajibikaji wakubwa pamoja na mambo mengine waweze kugharamia gharama za mwombaji anapoitwa kufanya interview, kwa nini iwe hivyo?
1. Kwa kiwango kikubwa watanzania tumepoteza uadilifu hivyo unakuta kampuni linaita waombaji lakini kumbe kuna watu wao ambao tayari wamewaweka kwenye hizo nafasi, kwa hiyo mtoto wa maskini anapoteza hata kasent kadogo alikokuwanako.
2. Mtoto wa maskini huyu (na hapa lazima ifahamike kwamba kunawatu wanajua neno umaskini lakini hawajui umaskini tulionao watanzania wengi) hana uwezo wa kuweza kugharamia gharama hizo kwani katoka shule juzi, nyumbani ni shida tupu, kasoma kwa shida hivyo kushindwa kuhudhuria hata kama yeye anauwezo hata zaidi ya waliohudhuria.
3. Mifano tunayo kwa vijana wengi hapa nchini kupitia sisi wenyeywe au ndugu zetu wa karibu jinsi ambavyo kijana wa kitanzania hasa mtoto wa maskini anavyonyanyaswa anapoomba ajira, kwa mfano utakuta kampuni imeita watu 20 kwenye interview lakini wanataka watu 2 tu (japo pia kunafaida za kuita waombaji wengi), bila kujali mazingira yao ya kiuchumi, madharani mtu anatoka mbeya kwenda Dar. ametafuta nauli kwa shida sana na dar hana ndugu hebu niambie gharama yake na mtu ni jobless halafu wapo ishirini, hivyo basi kama kampuni husika lingelikuwa linagharamia lisingeita watu 20 kwa kutaka watu 2.
4. Ni vyema pia serikali ikaweka utaaratibu wa kuhakikisha kuwa makampuni/ mashirika hayawasumbui waomba kazi hawa kwenda sehemu moja tu ya mbali kwa ajili ya interview, kwa mfano, ajira nyingi nchi hii interview zake zinafanyikia Dar. hata kama kituo cha kazi kipo Geita, ni kwa nini wasifanye hata kwa kanda ilikuwapunguzia mzigo wa gharama waombaji?
Huu ni mtazamo wangu tu, kwani inatokea mara nyingi tu Tanzania, watu wanaitwa interview kumbe kunawatu wamekwisha ambiwa hadi tarehe ya kuanza kazi, watu wanaitwa 1000 wanatakiwa 100, na interview zenyewe zaidi ya moja, kwa kiasi kikubwa mtoto wa kitanzania wa kawaida inakuwa ni kuzidi kutiana umaskini tu, ni bora pesa yake ndogo angeinvest sehemu nyingine kwani ukihudhuria interview Dar 3 na unatoka bukoba na kazi zenyewe ukakosa huo ni mtaji tosha!