Wazo: Tatizo la ajira na interview lukuki

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Kwanza kabisa ningependa kuunga mkono hoja ya kuwa na chombo mahususi cha kitaifa cha vijana kwa ajili ya kuweza kuongelea mabo mbalimbali yahusiyo vijana na kuishinikiza serikali nini kifanyike kwa ajili ya vijana, hoja ambayo kama sijakosea Mh. Mnyika alisema atapeleka hoja binfsi bungeni.

Tatizo la ajira limekuwa ni tatizo kubwa sana siku hadi siku hasa kwa vijana kwani ndo nguvu kazi kubwa ya taifa lakini pia ndo idadi iliyokubwa ukilinganisha na wazee. kuna sababu ni nyingi sana zinazochangia kukua kwa tatizo hili, ila binafsi nisingependa kuzieleza lengo langu hasa ni kuhusiana na hizi interview ambazo mwombakazi anatakiwa afanye kama njia ya kumpima uwezo wake na mambo mengine mengi.

Kwa mawazo yangu mimi ni bora serikali kupitia wizara ya kazi ingetunga sheria inayodhibiti makampuni, mashirika au wajiri mbalimbali wawe ndiyo wawajibikaji wakubwa pamoja na mambo mengine waweze kugharamia gharama za mwombaji anapoitwa kufanya interview, kwa nini iwe hivyo?

1. Kwa kiwango kikubwa watanzania tumepoteza uadilifu hivyo unakuta kampuni linaita waombaji lakini kumbe kuna watu wao ambao tayari wamewaweka kwenye hizo nafasi, kwa hiyo mtoto wa maskini anapoteza hata kasent kadogo alikokuwanako.

2. Mtoto wa maskini huyu (na hapa lazima ifahamike kwamba kunawatu wanajua neno umaskini lakini hawajui umaskini tulionao watanzania wengi) hana uwezo wa kuweza kugharamia gharama hizo kwani katoka shule juzi, nyumbani ni shida tupu, kasoma kwa shida hivyo kushindwa kuhudhuria hata kama yeye anauwezo hata zaidi ya waliohudhuria.

3. Mifano tunayo kwa vijana wengi hapa nchini kupitia sisi wenyeywe au ndugu zetu wa karibu jinsi ambavyo kijana wa kitanzania hasa mtoto wa maskini anavyonyanyaswa anapoomba ajira, kwa mfano utakuta kampuni imeita watu 20 kwenye interview lakini wanataka watu 2 tu (japo pia kunafaida za kuita waombaji wengi), bila kujali mazingira yao ya kiuchumi, madharani mtu anatoka mbeya kwenda Dar. ametafuta nauli kwa shida sana na dar hana ndugu hebu niambie gharama yake na mtu ni jobless halafu wapo ishirini, hivyo basi kama kampuni husika lingelikuwa linagharamia lisingeita watu 20 kwa kutaka watu 2.

4. Ni vyema pia serikali ikaweka utaaratibu wa kuhakikisha kuwa makampuni/ mashirika hayawasumbui waomba kazi hawa kwenda sehemu moja tu ya mbali kwa ajili ya interview, kwa mfano, ajira nyingi nchi hii interview zake zinafanyikia Dar. hata kama kituo cha kazi kipo Geita, ni kwa nini wasifanye hata kwa kanda ilikuwapunguzia mzigo wa gharama waombaji?

Huu ni mtazamo wangu tu, kwani inatokea mara nyingi tu Tanzania, watu wanaitwa interview kumbe kunawatu wamekwisha ambiwa hadi tarehe ya kuanza kazi, watu wanaitwa 1000 wanatakiwa 100, na interview zenyewe zaidi ya moja, kwa kiasi kikubwa mtoto wa kitanzania wa kawaida inakuwa ni kuzidi kutiana umaskini tu, ni bora pesa yake ndogo angeinvest sehemu nyingine kwani ukihudhuria interview Dar 3 na unatoka bukoba na kazi zenyewe ukakosa huo ni mtaji tosha!
 
Haswa inapokuwa wanawaleta tu kwa sababu wanatimiza utaratibu wanakuwa na waajiriwa wao tayari inauma kwa kweli
 
Hili nalo neno mkuu, lakini sio mahala pake. jaribu sehemu ya kazi au habari mchanganyiko
.
 
We acha ndugu yangu. Siku moja nikaona tangazo la ajira kule Tanzania Atomic Energy Commission. Wakaniita nilikipata. Uzuri ilifanyikia Arusha na mimi nilikuwa naishi huko.

Nilitoka tu kwenye ile ya kuandika. Kama mtihani wa Paper I chemistry A-level. Nimemaliza 2003 A-level na Undergrad. 2007, leo narudishiwa mtihani wa A-level. It was a disaster.

Nikajuta. Nikasema naachana na hizi kazi ngoja niendelee na dili za dar.

We acha ndugu yangu. Siku moja nikaona tangazo la ajira kule Tanzania Atomic Energy Commission. Wakaniita nilikipata. Uzuri ilifanyikia Arusha na mimi nilikuwa naishi huko.

Nilitoka tu kwenye ile ya kuandika. Kama mtihani wa Paper I chemistry A-level. A. nimemaliza 2003 na Undergrad. 2007, leo narudishiwa mtihani wa A-level. It was a disaster.

Nikajuta. Nikasema naachana na hizi kazi ngoja niendelee na dili za dar.

Tehe teheeeeeeee! pole sana umenikumbusha jamaa yangu aliomba kazi ya kufundisha private na yeye ni mwl. wa kiingereza wwakampatia mtihani wa form 6, halafu hadi leo kimya so huwa namtania matokeo ya necta bado au ndo ulipata zero!
 
Daktari Mwakabanje,hacha kulialia kwani dili za kutoa mimba wanafunzi siku hizi hazilipi? Ajira ni janga la dunia kwa sasa kwa mujibu wa ripoti ya ILO(2012) pigana kimpango wako,nenda kenya ukaone jinsi watu wanavyoshinda katika vimbweta vya bustani za jiji kutwa nzima.Daktari Mwakabanje hacha uoga wa maisha.
 
Nakusikitikia sana ndugu yangu kwani nashindwa kuelewa kuwa wewe ni mzima au and this is a second time to receive your foolish comments!

1. Mimi sio medical doctor kama unavyodhani hiyo ni username tu, lakini kubwa zaidi unataka kuhalalisha mauaji eti kisa tatizo la ajira au ugumu wa maisha kweli wewe unafikra za kuku!

2. Mimi sijalialia kama unavyosema, nimetoa mawazo yangu juu ya uendeshaji wa interview na mizengwe yake sasa kwa sababu uelewa mdogo basi unaropoka tu!

3. Acha kumeza data eti tatizo la ajira ni janga duniani kote, unalinganisha tatizo la ajira marekani na Tz? Na unalinganisha hatua wanazochukua wenzetu kukabiliana na tatizo na sisi, sisi kila kukicha tunauaviwanda, tunaacha wageniwanafanya hata kazi tunazoweza kuzifanya, wengine wanaingia bila vibali nk!

THINK BIG!
 
Sasa unaona hiyo dhambi ya kujiita dokta inavyokutafuna, kisa eti una kadigrii ka hair dressing&beauty management.Lazima utatubu tu,bwana mdogo.
 
Suala la ajira sio tatizo,tatizo ni sisi vijana,wahitimu na wadau/wasaka ajira kushindwa kujisimamia ama kuwa na ubunifu wa namna ya kutafuta ajira.

Cha kufanya ni kuomba nafasi ya kujitolea kwanza angalau w1ki 1 ukikubaliwa fanya kazi ile kwa bidii ili siku ulizoomba zikimalizika paonekane pengo. Na wakati huo huo unapokuwa unafanya kazi hiyo jaribu kuji-socialize (kuwa karibu na watu).

Ajira zipo tena nyingi sana kikubwa ni uhaminifu,watu tulio wengi tumekuwa si waaminifu hivyo kusababisha watoa ajira kuwaweka ndugu zao ili kama nafasi hizo haziwafai.
 
Sasa unaona hiyo dhambi ya kujiita dokta inavyokutafuna, kisa eti una kadigrii ka hair dressing&beauty management.Lazima utatubu tu,bwana mdogo.

Kuendelea kubishana na watu kama wewe ni kuchafua sifa za JF, nafikiri ungenisaidia zaidi kama ungechangia kwenye uzi huu kuliko kuanzisha taarabu humu!
 
Kwanza kabisa ningependa kuunga mkono hoja ya kuwa na chombo mahususi cha kitaifa cha vijana kwa ajili ya kuweza kuongelea mabo mbalimbali yahusiyo vijana na kuishinikiza serikali nini kifanyike kwa ajili ya vijana, hoja ambayo kama sijakosea Mh. Mnyika alisema atapeleka hoja binfsi bungeni.

Tatizo la ajira limekuwa ni tatizo kubwa sana siku hadi siku hasa kwa vijana kwani ndo nguvu kazi kubwa ya taifa lakini pia ndo idadi iliyokubwa ukilinganisha na wazee. kuna sababu ni nyingi sana zinazochangia kukua kwa tatizo hili, ila binafsi nisingependa kuzieleza lengo langu hasa ni kuhusiana na hizi interview ambazo mwombakazi anatakiwa afanye kama njia ya kumpima uwezo wake na mambo mengine mengi.

Kwa mawazo yangu mimi ni bora serikali kupitia wizara ya kazi ingetunga sheria inayodhibiti makampuni, mashirika au wajiri mbalimbali wawe ndiyo wawajibikaji wakubwa pamoja na mambo mengine waweze kugharamia gharama za mwombaji anapoitwa kufanya interview, kwa nini iwe hivyo?

1. Kwa kiwango kikubwa watanzania tumepoteza uadilifu hivyo unakuta kampuni linaita waombaji lakini kumbe kuna watu wao ambao tayari wamewaweka kwenye hizo nafasi, kwa hiyo mtoto wa maskini anapoteza hata kasent kadogo alikokuwanako.

2. Mtoto wa maskini huyu (na hapa lazima ifahamike kwamba kunawatu wanajua neno umaskini lakini hawajui umaskini tulionao watanzania wengi) hana uwezo wa kuweza kugharamia gharama hizo kwani katoka shule juzi, nyumbani ni shida tupu, kasoma kwa shida hivyo kushindwa kuhudhuria hata kama yeye anauwezo hata zaidi ya waliohudhuria.

3. Mifano tunayo kwa vijana wengi hapa nchini kupitia sisi wenyeywe au ndugu zetu wa karibu jinsi ambavyo kijana wa kitanzania hasa mtoto wa maskini anavyonyanyaswa anapoomba ajira, kwa mfano utakuta kampuni imeita watu 20 kwenye interview lakini wanataka watu 2 tu (japo pia kunafaida za kuita waombaji wengi), bila kujali mazingira yao ya kiuchumi, madharani mtu anatoka mbeya kwenda Dar. ametafuta nauli kwa shida sana na dar hana ndugu hebu niambie gharama yake na mtu ni jobless halafu wapo ishirini, hivyo basi kama kampuni husika lingelikuwa linagharamia lisingeita watu 20 kwa kutaka watu 2.

4. Ni vyema pia serikali ikaweka utaaratibu wa kuhakikisha kuwa makampuni/ mashirika hayawasumbui waomba kazi hawa kwenda sehemu moja tu ya mbali kwa ajili ya interview, kwa mfano, ajira nyingi nchi hii interview zake zinafanyikia Dar. hata kama kituo cha kazi kipo Geita, ni kwa nini wasifanye hata kwa kanda ilikuwapunguzia mzigo wa gharama waombaji?

Huu ni mtazamo wangu tu, kwani inatokea mara nyingi tu Tanzania, watu wanaitwa interview kumbe kunawatu wamekwisha ambiwa hadi tarehe ya kuanza kazi, watu wanaitwa 1000 wanatakiwa 100, na interview zenyewe zaidi ya moja, kwa kiasi kikubwa mtoto wa kitanzania wa kawaida inakuwa ni kuzidi kutiana umaskini tu, ni bora pesa yake ndogo angeinvest sehemu nyingine kwani ukihudhuria interview Dar 3 na unatoka bukoba na kazi zenyewe ukakosa huo ni mtaji tosha!

Dear Friends

These attached vacancies appeared on Daily News of 17 January 2013 and requires qualified candidates to apply within two weeks from the date of first advertisement. Thus the dead for interested is 31 January 2013
 
Attachments

Back
Top Bottom