Wazo: Program ya Kutafuta Vijana Wenye Vipaji vya Uongozi


Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined
May 9, 2012
Messages
7,913
Likes
2,483
Points
280
Azizi Mussa

Azizi Mussa

Verified Member
Joined May 9, 2012
7,913 2,483 280
wadau nawasalimuni.

Wazo.

  • Kuna vijana wengi wenye vipaji vya uongozi lakini kulingana na mazingira yanayowazunguka, hawajapata fursa ya kuonesha vipaji vyao na na kuvitumia pindi fursa zinapokuwepo.Hali hii inapelekea wakati fulani unakuta anahitajika mtu mwenye uwezo na maono ya kiuongozi kupewa jukumu la kuongoza taasisi,idara n.k, lakini unaweza kukuta kwa haraka haraka tu anapewa yule ambaye mara nyingi anaonekana akishinda nje ya ofisi husika kwa kuwa ndiye anayejulikana (hata kama hana uwezo)


  • Na fikiri ipo haja ya mtu au taasisi ikaanzisha program ya kutafuta hawa watu wenye vipaji na kisha watakapoonekana wanaweza kutumika kwa maslahi ya taifa,na taasisi mbali mbali.(haina maana kwamba viongozi wote watatoka kupitia utaratibu huo bali hii ni kama hamasa tu)


  • Wazo ni kwamba lianzishwe shindano ambalo litarushwa live kwenye kipindi maalum cha TV, ambapo washiriki watakuwa na muda wa kuwasilisha mada walizopanga/walizopangiwa na kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa majaji, muongoza kipindi, wasikilizaji watakaokuwepo live.n.k


  • Kuhusu mada/washiriki wanaweza kuchagua mada zao wenyewe au kuchaguliwa mada au vyote.Mada zinazoweza kuwasiliswa ni kama vile,Nafasi ya Tanzania katika Shirikisho la Africa Mashariki, Nafasi ya Tanzania katika Umoja wa Afrika, Ulimwengu wa Utandawazi na Uchumi wa Tanzania, Maaadili ya Uongozi na Siasa Tanzania katika miaka 100 ijayo, Demokrasia ya vyama vingi na Maendeleo Tanzania .n.k.


  • Miongoni mwa mambo yanayo weza kupimwa ni pamoja na uelewa wa jumla wa mshiriki, uwezo wa kujieleza, uwezo wa kufikiri haraka na kufanya maamuzi,uwezo wa kushawishi, kuthibiti hisia n.k.


  • washiriki wanaweza wakawa pengine vijana kati ya miaka 18-30.Ushiriki ni vyema ukawa bure kukwepa utapeli, ila washindi wakapewa zawadi kwa ajili ya hamasa.


  • Wazo hili linabakia kuwa huru kwa wadau,taasisi chama,au hata mtangazaji wa kipindi cha TV, kulifanyia kazi.


NB. itapendeza kama wanaowasilisha mada, watawekewa kanuni ya kutoa mawazo ya jumla juu ya misingi ya ujumla na wasiwe wanataja au kuwasilisha mada kwa mtuizamo wa vyama vya siasa (miongoni mwa masharti mengine).Hii italeta maana zaidi.

Ni wazo tu ambalo na wewe unaweza kuliboresha zaidi, na mwingine akaboresha zaidi na mwingine akachukua fursa.
 
mwanamke kazi

mwanamke kazi

Member
Joined
Sep 24, 2013
Messages
71
Likes
0
Points
13
mwanamke kazi

mwanamke kazi

Member
Joined Sep 24, 2013
71 0 13
mhhh! Tanzania hii hakuna kitu
 

Forum statistics

Threads 1,263,516
Members 485,918
Posts 30,154,766