Wazo mbadala la kuijenga Tanzania mpya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo mbadala la kuijenga Tanzania mpya.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by amba.nkya, Feb 1, 2012.

 1. amba.nkya

  amba.nkya JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 431
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Heshima mbele WanaJF…
  Kwa muda mrefu sana watanzania wengi wanazidi kuwa masikini na wachache kuwa matajiri ilhali rasilimali zipo bwerere kila pembe ya nchi hii, na hivyo, kuwepo kwa Gap kubwa kati ya matabaka hayo huku masikini wakizidi kuteseka kwenye nchi yenye neema. Ukiangalia kwa jicho la karibu utaona hao matajiri wachache waliowengi ni wanasiasa kwa maana ya watawala kupitia chama tawala (CCM) ambao ndiyo wenye maamuzi na hizo rasilimali na pamoja na wafanyabiashara waliokaribu na wanasiasa hao.

  Sasa nini kifanyike?
  Kwa vile nchi hii inaendeshwa kisiasa, vijana wa Tanzania kwa uwengi na uwezo wao zaidi kuliko rika nyingine, pia ndio wenye hatima ya kuijenga Tanzania mpya kwa sasa ukizingatia kuwa ni wahanga wakubwa kutokana na kukosa haki za msingi za maendeleo ikiwa ni pamoja na kunyimwa fursa hususan elimu ya juu, kuwezeshwa kiuchumi (mitaji, ajira, rasilimali n.k). Hivyo, vijana wana wajibu wa kuhakikisha nchi ya Tanzania inajengwa upya kwa kushiriki kikamilifu katika kupambana kwa nguvu zote na udhalimu unaofanywa na wanasiasa (watawala) bila woga wala kukata tamaa.

  Mikakati
  1. Vijana kwa uwingi, uwelewa na uwezo wao wanapashwa kushiriki kikamilifu kwenye mchakato na uundwaji wa Katiba mpya.
  2. Vijana wengi wenye weredi katika nyanja mbalimbali washiriki kikamilifu kwenye siasa. Hii ni pamoja na kujiunga kwa wingi kwenye chama cha siasa chenye mwelekeo, nia dhabiti na ya dhati ya kulikomboa taifa hili. Mfano, CHADEMA ndicho chama mbadala kwa wakati huu.
  3. Kila kijana mahali alipo awe na ushawishi wa kuhamasisha wakazi wengi wa eneo husika wajiunge na chama hicho mbadala na kufungua matawi mengi iwe mjini hadi vijijini na kuwashirikisha viongozi wa chama hicho mbadala kwenye eneo husika.
  4. Vijana wengi kushiriki kikamilifu ktk chaguzi mbambali za vyama vya siasa kwa ngazi zote na kuhakikisha kura zinalindwa ipasavyo ili kuthibiti uchakachuaji wa matokeo ili kushinda chaguzi hizo.
  5. Wazazi wajitahidi kujinyima kwa kupeleka watoto shuleni bila kujali hali hali halisi kiuchumi ili kuwawezesha watoto wapate elimu ktk ngazi mbalimbali iwe ufundi sanifu, elimu ya juu na taaluma nyingine kama kilimo, ujasiriamali na hatimaye tuwe na taifa la vijana wenye uelewa mkubwa kwenye taifa hili na vijana ambao wanawezakujiajiri wenyewe na kuinua taifa letu kiuchumi na kupata maendeleo kwa ujumla.
  Ingawa kuna changamoto nyingi, ni imani yangu kuwa tukithubutu kuanza na wazo hili; tutaweza, tutasonga mbele na kuijenga Tanzania mpya.

  Nawasilisha…..
   
Loading...