Wazo mbadala: Aheri ya RUSHWA kuliko POSHO. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo mbadala: Aheri ya RUSHWA kuliko POSHO.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Feb 5, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Suala la posho linakuja kwa kasi na kugonga hisia za Watanzania kila kukicha. Ukianzia kwa wabunge, wanaomba kura kwa wananchi ili wawe wawakilishi wao dhidi ya serikali. Vikao vya bungu ni sehemu ya kazi wanayotumwa na wapiga kura wao kwa mshahara halali wanaolipwa na serikali. Wakifika huko wanakaa na kudai posho kwa malaki. Wanasahau kuwa vikao vya bunge ni moja ya kazi zao. Watumishi wa uma nao wakikaa kwenye semina na vikao vya kikazi, wanadai posho! Wanasahau kuwa semina na vikao hivyo ni kwa faida yao. Sasa wanajeshi nao katika kazi za kujitolea kuisaidia jamii nao wanadai posho..Kwa wenzangu na mimi huku mitaani, mwananchi ambaye hana ajira, anaishi kwa kubangaiza anaambiwa achangie ujenzi wa madarasa ya shule. Hakuna kumwandikisha mtoto darasa la kwanza mpaka mzazi atoe mchango wa ujenzi wa madarasa. Afisa mtendaji haidhinishi barua ya mkulima kuomba kufungua akaunti benki mpaka atoe mchango wa ujenzi wa sekondari wakati mbunge wake anatumia posho kwa ajili ya kunywea heinken. Bora rushwa potelea mbali, unahonga lakini unapata unachohitaji. Imekuwa kama biashara, ukihitaji gari la kifahari au hata la kawaida unanunua kwa pesa linakuwa mali yako. Ni sawa na kuwa unahitaji kazi, unampa pesa bosi naye anakupa ajira. Uko katika haraka zako unakutana na askari wa usalama barabarani. Anakusimamisha, ili uwahi dili zako, unampa pesa kidogo naye anakuruhusu unawahi mambo yako. Hii yaweza kuwa biashara halali kuliko posho. Unafanya kazi ya kulijenga Taifa, unalipwa mshahara halali kulingana na kazi yako, unapelekwa semina kuongeza ufanisi wako, unaenda kuwasilisha yale uliyotumwa na wananchi walio kuchagua na mshahara unapewa. Lakini bado unadai posho! Kwa mtazamo wangu ni heri RUSHWA ina kamsaada kidogo kuliko POSHO zinazowakaba wananchi.
   
Loading...