Wazo: Magu anzisheni chama chenu CCM hutaiweza

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Huu ni wito tu yametokea Kenya na KANU sasa Botswana ni yaleyale yanataka kutokea na Zambia.

Njia rahisi kwa Magu na wanaomuunga mkono kama kweli anaamini ana nguvu za mabadiliko na ana support ya Watanzania ni kuanzisha Chama kingine cha siasa. Hii itakuwa rahisi kwasababu wote watakuwa na agenda na lengo moja.

Kwa sasa CCM sio moja kuna wengi walioajiriwa na kutajirika na chama, kuna ambao wanataka kuacha watoto zao huko, kuna wana urafiki na kibaya zaidi wote hawa wana nafasi kubwa ndani ya CCM.

Hivyo hawafukiziki kirahisi, ni wengi na wale wanao support sana kama Mwinyi, Mkapa, Msekwa, Msuya wataondoka na kukuacha na vijana wenye uchu wa madaraka ambao ni wakina Nape, Mwigulu, Bashe, Makamba, Jofa na Makamba.

Hivyo kama kweli unataka kuleta maendeleo hutaweza kubadilisha yote CCM anza upya tu. Kwasababu sasa hivi ukisema lolote baya kwa mzee yoyote ana uwezo wa kuleta matatizo kwenye chama maana ana wafuasi.

Tatizo lingine wafuasi wako sio wengi ndani ya CCM kuliko wafuasi wengine wote na vikundi vyote pamoja ndani ya CCM.
Huyo Dr kamshidwa Membe je atawaweza Makamba, Kinana, Membe, Nape .... na wengine wote.

Kwa vijana wa CCM nawashauri sana hamtakuwa na nafasi mpaka mahakama iwe na uhuru zaidi sio kama sasa serikali inaweza kubana vyama msi support ubanaji wa vyama maana kesho na kesho kutwa hata CCM inaweza kuwa na vyama viwili na mlinzi wenu atakuwa mahakama. Jiulizeni je CCM ikivunjika leo halafu usiruhusiwe kuingia na kuwa mwanachama utafanya nini kama sheria ndiyo hizi hivyo mwangalie mbali mahakama huru na yenye nguvu ni muhimu kwa strategy yenu
 
Angekuwa anaweza siasa hasa za ushindani hilo angeweza. Kuna hatari ya yeye kuanzisha chama cha kijeshi na sio chama cha siasa. Jaribu hata kuangalia toka yeye ameingia madarakani ccm imepata taswira ya kijeshi zaidi, toka chama cha ushawishi wa kisiasa hadi chama cha mabavu na kisichotaka ushindani wa kisiasa.

Kwenye box la kura ndio kabisa, huko hakuna ushindani bali hujuma za wazi kwa kutumia vyombo vya dola. Hata hao wanaccm wanaopinga mwenendo wa sasa ni baada ya kuona chama chao kinatolewa kutoka chama cha siasa kugeuzwa chama cha kijeshi. Na hakuna uhakika kwamba kweli anakubalika kisiasa, kwani mpaka sasa hataki vipimo vya kukubalika vifanye kazi zaidi ya wananchi kulishwa maneno kwamba wanamkubali, na taasisi za kimamlaka kutumika kulazimisha kwamba anakubalika.
 
Kwa nchi yetu kuanzisha chama kipya ukaeleweka na kukubalika miongoni mwa watanzania wa kawaida (ambao ndio wengi) si jambo jepesi. Rejea kuimarika kwa CHADEMA kumeichukua miongo mingapi!! Jamii kubwa ya watanzania hata hawafahamu masuala ya itikadi za vyama vyao bali utawaliwa na ushabiki wa kushinda na kushindwa kwa chama husika, hivyo umaarufu iliyonao CCM ukijiengua unaumia wewe mwenyewe, ndo maana pamoja na moto unaowaka ndani ya chama hatuoni hata mmoja wao anaeshawishika kuhama au kuanzisha chama. Kila mmoja yupo tayari kuungulia chamani ili ikitokea la kutokea fursa yaweza kupatikana kama zari la Bashe aliyeonekana kupingana na Mkuu katika masuala mengi tu.

Sana sana anachoweza kufanya JPM ni kuhakikisha anawa-harass wapinzani wake ndani ya chama ili wao ndio wampishe na kuanzisha ama kujiunga na vyama vingine. Kimsingi hadi sasa CCM mpya inaweza kupata uungwaji mkono dhidi ya CCM asilia kutokana na kundi hilo la pili kuendelea kuamini kuwa Tanzania ni ya kwao kuliko watanzania wengineo.
 
Nadhani tungetumia nguvu zaidi kuijadili Chadema kuliko CCM. Chadema iko wapi wakati huu ambao CCM inaonekana ina msuguano. Hiki chama kimekufa au bado kipo hai. Maana siasa za nchi zote zinaendeshwa na CCM.
 
Huu ndo muda mzuri zaidi kwa CCM kutibuana kwa maslahi mapana ya chama chao ukizingatia upinzani wenyewe unapumulia masikio.

Mazingira ya kufanya siasa ukiwa mpinzani yamefanywa yawe magumu maradufu tena hao wenye madudu ndo hawawezi kwenda huko.

Siku zote wasiokubaliana na kinachoendelea ndani ya chama chao na wakawa hawawezi kubadili kitu ndo huanzisha vyama vingine hata kama wao ndiyo wengi. Refer CUF.
 
Njia rahisi kwa Magu na wanaomuunga mkono kama kweli anaamini ana nguvu za mabadiliko na ana support ya Watanzania ni kuanzisha Chama kingine cha siasa.
Wewe ndie uliyepotea njia kabisa.
Magu ndie mwenye CCM yake unataka aondoke akaanzishe chama tena, cha nini?
CCM ni ya nani kama sio ya Magufuli!

Hao wengine wasiokubali afanyayo Magufuli ndio wanaotakiwa wakatafute chama kingine au waanzishe cha kwao kipya.
 
Angekuwa anaweza siasa hasa za ushindani hilo angeweza. Kuna hatari ya yeye kuanzisha chama cha kijeshi na sio chama cha siasa. Jaribu hata kuangalia toka yeye ameingia madarakani ccm imepata taswira ya kijeshi zaidi, toka chama cha ushawishi wa kisiasa hadi chama cha mabavu na kisichotaka ushindani wa kisiasa.
Mleta mada sijui kwaza nini. Magufuli sio mwanasiasa ataanzia wapi kuunda chama cha siasa na kukijenga, kukilea hadi kiimarike, kama hana njia za kulazimisha? Ataamrisha watu wajiunge na chama chake alichokianzisha kwa nguvu?
 
Wewe ndie uliyepotea njia kabisa.
Magu ndie mwenye CCM yake unataka aondoke akaanzishe chama tena, cha nini?
CCM ni ya nani kama sio ya Magufuli!

Hao wengine wasiokubali afanyayo Magufuli ndio wanaotakiwa wakatafute chama kingine au waanzishe cha kwao kipya.
Kama kweli ni yake tusingewaona hawa wote kwenye chama mpaka sasa. Angekuwa na uwezo wengi wasingekuwepo lakini anashidwa kuwafukuza. Ukisema chama ni cha kwake unajidanganya utaona kama atafanya kitu kwenye chama ni huko serikalini tu. Hawa jamaa bado wana nguvu sana ndani ya chama
 
Kwa nchi yetu kuanzisha chama kipya ukaeleweka na kukubalika miongoni mwa watanzania wa kawaida (ambao ndio wengi) si jambo jepesi. Rejea kuimarika kwa CHADEMA kumeichukua miongo mingapi!! Jamii kubwa ya watanzania hata hawafahamu masuala ya itikadi za vyama vyao bali utawaliwa na ushabiki wa kushinda na kushindwa kwa chama husika, hivyo umaarufu iliyonao CCM ukijiengua unaumia wewe mwenyewe, ndo maana pamoja na moto unaowaka ndani ya chama hatuoni hata mmoja wao anaeshawishika kuhama au kuanzisha chama. Kila mmoja yupo tayari kuungulia chamani ili ikitokea la kutokea fursa yaweza kupatikana kama zari la Bashe aliyeonekana kupingana na Mkuu katika masuala mengi tu.

Sana sana anachoweza kufanya JPM ni kuhakikisha anawa-harass wapinzani wake ndani ya chama ili wao ndio wampishe na kuanzisha ama kujiunga na vyama vingine. Kimsingi hadi sasa CCM mpya inaweza kupata uungwaji mkono dhidi ya CCM asilia kutokana na kundi hilo la pili kuendelea kuamini kuwa Tanzania ni ya kwao kuliko watanzania wengineo.
Unaypongea ni kweli lakini huyu ni Dr Magufuli jina pekee ni maarufu na imara kuliko CCM ya miaka 42
 
Harufu ya Mapinduzi kwa mbaaaaaliiiiiii, kama nawaona wale clean ndani ya Chama wakijazana Chadema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom