Wazo la leo

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
Miezi mitatu na nusu sasa inatosha kukupa picha ya muelekeo wa maisha yako kwa mwaka huu wa 2017.

Hakuna siri wala huitaji nabii kukutabilia December mwaka huu itakuwaje, kama hautafanya kitu kuubadilisha huu mwelekeo.

Kama kweli unataka mabadiliko mwezi wa kumi na mbili fanya kitu sasa hivi kubadilisha huu mwelekeo.

Newtown law of motion inasema kila kitu kitaendelea kukaa kwenye muelekeo huo huo na kubaki kwenye mwendo huo huo, mpaka nguvu nyingine ya tofauti itakapo kuja kuingilia kati.

Kama hufanyi chochote cha tofauti kuhusu hayo madeni yako uliyonayo sasa hivi, usitegemee kufikia mwezi wa kumi na mbali kutatokea muujiza ukayafuta hayo madeni.

Kama hufanyi kitu cha tofauti sasa hivi kuhusu hali yako ya kifedha, kama kujiwekea akiba kidogo au kujiongezea ufahamu kidogo utakao kusaidia kuongeza kipato chako, usitegemee muujiza kwamba mambo yatabadilika ikifika mwezi wa kumi na mbili.

Yaani hiyo hali yako ya sasa hivi na ukiacha mambo yaendelee kama yalivyo huo ndiyo utakuwa mwelekeo wako kwa miezi yote ya mwaka iliyobaki.
 
Back
Top Bottom