Wazo kwa Serikali: Pawepo "Vijana Taifa Bank"

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,339
Reaction score
1,493
Habari Tanzania !
Napenda niwe mshauri wenu kwa hawa vijana.

Ikiwapendeza, anzisheni taasisi mpya kutoka moja kwa moja Wizara ya Fedha iitwe " VIJANA TAIFA BANK". Hii taasisi iwe maalumu kwa kuweka na kuwakopesha vijana waweze kuwekeza kwenye miradi na biashara mbalimbali hapa nchini na ikiwezekana hadi nchi za nje.

Hii taasisi ifungue matawi mpaka ngazi ya Kata hapa nchini; lengo ni kuweza kuwafikia Vijana wote wa Taifa hili kwa uharaka na uhakika.

Hizo pesa zenu za Halmashauri mnazozipotezaga huko; ziwekeni humo (Vijana Taifa Bank) fedha zote na nyinyi Wizara mtie hela humo za kutosha yaani hata Bajeti yenu kabla ya kuipeleka Bungeni itisheni kikao na viongozi wa Vijana Taifa wawape mapendekezo yao ndio mkawazungumzie huko Bungeni.

Hitimisho

Ikiwapendeza hiyo taasisi iendeshwe na Vijana toka Vyuo Vikuu tu. Lengo hawa vijana watumike kikamilifu hasa kulitumikia taifa.

Karibu.
 
Ni wazo zuri sana.
Vijana wenye elimu na weledi tunao.
Kilicho bakia ni utendaji wenye tija na ufanisi
 
Benki hata ingeitwa chipukizi bank kama taratibu zitabakia kama zilivyo haitasaidia.
 
Bank zilizopo hazifanyi kazi kwa kuakisi dhumuni lao la Usajiri na endeshaji ndio maana kwenye Ulimwengu wa Biashara za Kifedha Bank zetu zimeathiriwa sana na kupitwa na ukuaji wa mitandao ya simu hapa nchini; pia uwepo wa technology bandia ndio unazidi kuzivua nguo hizi Taasisi za kifedha hapa nchini.

Leo hii huduma na bidhaa ambazo Benks zinatoa ni kipengele.
 
Mtaji wa viongozi ni umasikini na ujinga wa Mtanzania
Hawako tayari Mtanganyika apate utajiri na elimu Bora.
Hiyo ni ndoto wala hawawezi kuwapa banks, mtapewa fulana na baiskel
 
Hiyo mikopo watapeana wenyewe kwa wenyewe na benki benki itajiendesha kwa hasara na itakufa.

Mabilioni ya Kikwete yalipigwa na wao wenyewe.
 
H
Habari Tanzania !
Napenda niwe mshauri wenu kwa hawa vijana.

Ikiwapendeza, anzisheni taasisi mpya kutoka moja kwa moja Wizara ya Fedha iitwe " VIJANA TAIFA BANK". Hii taasisi iwe maalumu kwa kuweka na kuwakopesha vijana waweze kuwekeza kwenye miradi na biashara mbalimbali hapa nchini na ikiwezekana hadi nchi za nje.

Hii taasisi ifungue matawi mpaka ngazi ya Kata hapa nchini; lengo ni kuweza kuwafikia Vijana wote wa Taifa hili kwa uharaka na uhakika.

Hizo pesa zenu za Halmashauri mnazozipotezaga huko; ziwekeni humo (Vijana Taifa Bank) fedha zote na nyinyi Wizara mtie hela humo za kutosha yaani hata Bajeti yenu kabla ya kuipeleka Bungeni itisheni kikao na viongozi wa Vijana Taifa wawape mapendekezo yao ndio mkawazungumzie huko Bungeni.

Hitimisho

Ikiwapendeza hiyo taasisi iendeshwe na Vijana toka Vyuo Vikuu tu. Lengo hawa vijana watumike kikamilifu hasa kulitumikia taifa.

Karibu.
Hongera kwa kutushirikisha wazo nzuri... hili wazo moja kwa moja liingie kwenye fail za wizara ya vijana.
 
Back
Top Bottom