Wazo huru: Yanga/Azam ziwakimbize Waarabu Saa 8 mchana

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
Kiukweli ili kuwapiga nyingi inabidi wawapeleke Taifa saa8 mchana, hakuna njia nyingine ya kuwang'oa zaidi ya kuwakimbiza saa8 mchana pale taifa na Chamanzi.
Ifikie wakati na sisi tuanze hujuma na hii ya saa8 mchana inawahusu waarabu.

Hili ata kwa Azam na watunisia linawahusu. Kwa uchache japo mabao matatu kwa bila nyumbani ni mtaji.
Sioni njia nyingine ya kuwatoa waarabu zaidi ya hiyo, ikumbukwe pia hawa jamaa hutumia muda mwingi kujiangusha na kujikuta game ikiisha kwa dk60 tuu!!

Lakini sasa kwa viongozi wetu sijui kama itawezekana, maana watataka kuitumia mechi hiyo kupiga pesa za viingilio.
 
Sasa hivi kina jeri wanawaza mapato ya mlangoni tu wewe utaona kama watapota sidhani kam wana mikakati
 
mnawapeleka mtwara uko kiwanja cha ndanda uko nangwanda sijaona, wakitoka salama lazima wahadithie kwao.
hakika hii ndo fitina pekee inayopumua.... Kama walivokua wanafanya enyimba wakitaka matokeo... Wanakupeleka bush na mvua wanaileta
 
Duh!kuna uwanja huo niliisha wahi kuchezea yaani golikipa na golikipa hawaonani inabidi centrehalf amwambie nyanda tumeisha wapa moja huko kipa anaanza kushangilia.Kifupi haiwezekani kwani caf wana viwango vyao na msimamizi wa mchezo huja kukagua uwanja.
 
Hii hujuma kwa azamu sawa, ILA KWA VYURA FC HAPANA AISEEE, NYIE SI MNAJIITA WA KIMATAIFA SASA VP TENA MBONA MNAANZA KUWAOGOPA WAKIMATAIFA WENZENU?????

KAMA VP TUUZIENI SISI HIYO MECHI TUICHEZE MUDA WOWOTE TUWANYESHE WAKIMATAIFA WALIVYO!

MKILETA UKAIDI MPIGWEEEEEE HATA 5 SAWA TUUU!
 
Azama wameanza kujifunza fitna na tumewaona walipowachezesha bidvest saa tisa alasiri! jamaa muda wote walikua wanakimbilia maji nje ya uwanja mara tu mpira unaposimama.

Kwa upande wa Yanga, hawa hawana chochote wanachokiwaza zaidi ya mapato ya uwanjani.Mimi ni shabiki wao ila hawanishawishi tangu 1935! wanaishi kwa kutegemea tu mapato ya uwanjani! eti sisi wa mikoani tuwasikilize kupitia tbc taifa! bora watolewe tu ili hao viongozi wa timu waanze kuumiza vichwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato.

Azam ya mwaka 2011 na vilabu vyetu vya yanga na simba vya miaka ya 1930's ni sawa na umbali wa Dar to Kigoma.
 
watu wengine jiografia ya dunia hawaijui, waarabu kuwachezesha saa 7 mchana si utachemsha wewe, wao wamezoea
 
Hii hujuma kwa azamu sawa, ILA KWA VYURA FC HAPANA AISEEE, NYIE SI MNAJIITA WA KIMATAIFA SASA VP TENA MBONA MNAANZA KUWAOGOPA WAKIMATAIFA WENZENU?????

KAMA VP TUUZIENI SISI HIYO MECHI TUICHEZE MUDA WOWOTE TUWANYESHE WAKIMATAIFA WALIVYO!

MKILETA UKAIDI MPIGWEEEEEE HATA 5 SAWA TUUU!
5 kama mlizocharazwa na Creativo Desportivo le Club Libolo au Haras el Hadood?

Sisi ni wa kimataifa ndio, si sawa na Sokoni FC
SAM_0447.jpg

Kweli watu wenye akili chanya hili laweza kuwa jengo la klabu? Hapa mchezaji anafanyiwa majaribio wapi hapa sokoni?

07.JPG


Weka heshima unaongea na nani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom