Wazo fikirishi kwa vijana wote wanaopenda kuweka picha za Utupu kwenye Mitandao ya Kijamii

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
WAZO FIKIRISHI KWA VIJANA WOTE WANAOPENDA KUWEKA PICHA ZA UTUPU KWENYE MITANDAO YA KIJAMII.


Mitandao ya kijamii kwa Mimi naona ina faida nyingi sana kwa vijana wengi endapo tutaweza kuitumia vizuri na kwa utashi wa hali ya juu.


Nasema hivi kwa sababu; vijana wanaweza kutumia ili; wajielimishe,wajikosoe,wawasilishe maoni yao,wawasiliane na ndugu pamoja na marafiki zao Duniani na kadharika.


Pia, faida nyingine ni kujiburudisha. Nitaeleza faida hii hasa kwa sisi vijana.


Mara nyingi tunaitumia vibaya hasa kuweka picha zetu kama tukiwa tuko watupu,yaani huna nguo yoyote. Mfano wangu umejikita kwa vijana japo na wazee baadhi wanayo hii tabia tu.


Tahadhari hii naitoa kwa vijana kwa sababu za msingi kabisa. Vijana ndiyo kundi kubwa linaloongoza kwa kutumia mitandao hii ya kijamii kuliko kundi lolote lile.


Nitatoa mifano mitatu hapa chini ninayofikiria ni ya msingi kwangu na vijana wote kama mtanielewa.


1. Kuna vijana wengine mna NDOTO za kuwa viongozi wakubwa,na mtakuwa viongozi kweli. Je,hatuoni kuwa baadae itatukosesha heshima kwa watu wetu tutakaowaongoza?. Tunatakiwa kujua wazi kabisa ukishatupia picha hata baada ya sekunde kadhaa ujue tayari imesambaa Duniani kote. Weka picha za kawaida tu, angalau hata ukiwa unajiachia uwe beach basi na watu waone kweli huyu alikuwa beach,japo na huko siyo utoe kila kitu ubaki u.......!!!!Tutafakari ili baadae isije tukaanza kusema ningejua!!!


2. Lazima utakuja kuwa Mzazi au Mlezi wa familia. Watoto wako wataziona hizo picha maana zitakuwepo kwenye mitandao ya kijamii. Kwa hiyo basi fanya mbwembwe zote kama kijana lakini usichojoe Nguo zote na ukatupia maana ujue kesho kutwa utakuwa Mzazi na watoto wako watakushangaa.


Wewe weka picha hata kama umejiachia kiasi chake lakini si kuwa mtupu kabisa. Baadae madhara ni makubwa kuliko sasa.


Kujiachia kama kijana lazima ujiachie lakini kuwa makini sana ukiwa unajiachia hasa kwenye kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii.


Usidhubutu kwa namna yoyote kuweka picha ukiwa hujavaa chochote na ukajipa moyo kuwa nitadelete,hapo ujue unajidanganya tu. Tutafakari sana tukiwa tunajiachia vijana.


3. Je,ukioa au ukaolewa na baadae mwenzako au wewe ukaja/akaja kuziona hizo picha kwenye mitandao ya kijamii itakuwaje?. Atajua kuwa hukuwa mtu mwenye hekima hata kidogo japo anaweza kukuvumilia kama kubadilika kwa hali ya hewa tunavyovumilia.


Tutafakari sana haya mambo,leo inaweza ikawa kawaida ukifanya lakini likija kukutokea ndipo utajua namaanisha nini hapa. Tutafakari sana tukiwa tunakula bata!!.
 
Back
Top Bottom