Waziri Zanzibar atoa siku 14 walioharibu mikarafuu yake kujisalimisha, vinginevyo atasoma Albadir

Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,381
4,355
1.jpg

Waziri wa Zanzibar asiye na wizara maalum ambaye aliharibiwa mikarafuu yake, ametoa siku 14 tu, walioharibu mazao yake wajisalimishe la sivyo anawasomea albadiri na atakusanya waganga wote duniani!

Chanzo: ITV

========
Waziri asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mhe. Said Soud,amewapa siku kumi na nne walioharibu shamba lake kujitokeza.

Waziri huyo amesema kuwa watu hao wasipojitokeza atakusanya waganga wote nchini ili kuwasomea albadir. Akaongeza kuwa yeyote atakayejitokeza hatampeleka polisi.

Siku chache zilizopita,watu wasiojulikana wamevamia na kuharibu shamba la Waziri huyo. Hata leo,imeripotiwa ITV kuwa watu wasiojulikana huko Pemba wamevamia na kukata mikarafuu tisa kati ya kumi ya mkazi mmoja wa hukohuko Pemba.
 
Waziri asiye na Wizara Maalum wa Zanzibar Said Soud Said ameapa kuwasomea Albadir watu wote waliofyeka shamba lake usiku wa kuamkia june 14 mwaka huu .

Source ITV Habari saa 2.00 17.6.2016

Katika hujuma hizo zilizotokea katika shamba lililoko Mgelema Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake , jumla ya mikarafuu 29 , minazi 16 pamoja na mashina 250 ya muhogo yamengo’lewa na baadhi ya mengine kufyekwa na kitu chenye ncha kali .

Katika tukio hilo mikarafuu michanga 15 imeng’olewa na kutupwa ndani ya shamba , na mengine 14 iliyokuwa tayari kuzaa imekatwa na kuachwa ndani ya shamba .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi , Said Soud Said alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo vya kuhujumu mazao makuuya uchumi wa nchi .

Aidha alieleza kwamba , baadhi ya wananchi wanalichukulia suala la siasa kama ni chuki au fitina , na kuwashangaa wanaoendesha humuma hizo kwani haziwezi kusaidia kutatua changamoto za kisiasa .
 
Waziri asiye na Wizara Maalum wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mhe. Said Soud,amewapa siku kumi na nne walioharibu shamba lake kujitokeza.

Waziri huyo amesema kuwa watu hao wasipojitokeza atakusanya waganga wote nchini ili kuwasomea albadir. Akaongeza kuwa yeyote atakayejitokeza hatampeleka polisi.

Siku chache zilizopita,watu wasiojulikana wamevamia na kuharibu shamba la Waziri huyo. Hata leo,imeripotiwa ITV kuwa watu wasiojulikana huko Pemba wamevamia na kukata mikarafuu tisa kati ya kumi ya mkazi mmoja wa hukohuko Pemba.
 
Waziri asie na wizara maarum serikali ya mapinduzi zanzibar ametangaza siku kumi na nne kwa wale waliokata mikarafuu yake wajisalimishe vinginevyo ataita waganga wote tanzania nzima na kusoma alubadili
 
teh teh teh

Huyo atakuwa wa CCM tu huyo..
 
Waziri wa Zanzibar asiye na wizara maalum ambaye aliharibiwa mikarafuu yake, ametoa siku 14 tu, walioharibu mazao yake wajisalimishe la sivyo anawasomea albadiri na atakusanya waganga wote duniani! Source ITV

Wewe unayewashangaa viongozi wa ccm ndiyo unaonekana mkali,kwa ccm hii iliyoparaganyika maono na utashi,hayo ni mambo ya kawaida sana.Sioni tofauti ya tamko hilo na lile la kujenga uwanja wa kumbukumbu ya push-ups.
 
Usinichanganye! Mi sijataja mambo ya ccm wala chama chochote, nimenukuu alichosema waziri, we vipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom