real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,296
Anasema ''Mashine ya kutengeneza toothpick ni doa 28,000, dola 28,000 ni jukumu lako mtanzania kuwekeza, kuna watanzania wanaogiza mashine za toothpick, mfano mheshimiwa Lema ameagiza mashine ya toothpick anapeleka Kilimanjaro, watu wanahangaika, msikosoe tu,
Toothpick inatumia mabaki ya miti yasiyokuwa na kazi nyingine, na wala sio mbao, viwanda ni vita bwana Msigwa, toothpick mkitaka zisiagizwe nitazizuia zisiagizwe, TBS ni yangu, lakini na nyie muwekeze, watu wanapenda toothpick''
Mimi naona watanzania tusikae chini na kuiacha serikali pekee ndio ianzishe viwanda, bali wenyewe tujiongeze tupige hata kolabo kuanzisha viwanda vidogo vya usindikaji na hatimae tujenge uwezo hadi kuwekeza kwenye viwanda vikubwa, badala ya kuwekeza kwenye matanuzi na luxury na kukaa kuiombea serikali ifeli na kukesha kwenye social media kuchonga.