Waziri Dkt. Stergomena Tax: Mfumo wa Taarifa kwa Wawekezaji ni fursa ya kutanua masoko ndani na nje nchi

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
298
513
20221201_072917.jpg

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji, mfumo umezinduliwa Novemba 30, 2022 jijini Dar es Salaam.SERIKALI imetaja vipaumbele katika uwekezaji ambavyo ni Kilimo, Usalama wa Chakula, Nishati (Nishati jadidifu), Elimu, Utalii na Miundombinu.

20221201_073130.jpg

Kwa Upande wa Naibu Waziri wa Uwezaji, Exaud Kigahe amesema kuwa Changamoto iliyokuwepo ni kukosa kwa taarifa za uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, amesema sasa mfumo huo utaonesha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa mataifa mengine duniani.

Kigahe amesema hakuna masharti yeyote katika uwekezaji ni kuwa na vifaa vya teknolojia ya kisasa ili kuweza kuingia katika Mfumo huo kwa kuweza kupata taarifa za sekta unayotaka kuwekeza au kufanya biashara.

"Serikali inapoendelea kutengeneza mazingira wezeshi kwa wawekezaji, Watanzania wachangamkie fursa hiyo kwani uwekezaji sio kwa watu wa nje ya nchi tuu bali ni ya Watanzania wote.

DSC_0026.JPG

Naibu Waziri wa Uwezaji, Exaud Kigahe akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo wa taarifa kwa wawekezeji.

=====

Waziri Dkt. Stergomena Tax: Mfumo wa Taarifa kwa Wawekezaji ni fursa ya kutanua masoko ndani na nje nchi

Baada ya uzinduzi wa Mfumo wa Taarifa kwa Wawekezaji uliozinduliwa Novemba 30, 2022, Dar es Salaam, Serikali imetaja vipaumbele katika uwekezaji ambavyo ni Kilimo, Usalama wa Chakula, Nishati (Nishati jadidifu), Elimu, Utalii na Miundombinu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa katika uzinduzi huo amesema Mfumo huo utawawezesha wawekezaji wa ndani na nje nchi kupata taarifa za fursa mbalimbali na masoko.

Aidha, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema amesema mfumo huo utaonesha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa mataifa mengine Duniani.

20221201_084848.jpg

Naye, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNDP, Christine Musisi amesema UNDP inashirikiana na Serikali kutengeneza mfumo wa taarifa za uwekezaji zitakazomwezesha mwekezaji kupata taarifa na fursa za uwekezaji zilizopo pamoja na masoko kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi ili kuleta maendeleo nchini.

Amesema: "Tanzania inafursa nyingi katika sekta ya Miundombinu, Utalii, Kilimo, Uhifadhi wa chakula, Elimu na Nishati.”
 
Back
Top Bottom