Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa awasimamisha na kuwastaafisha kazi watendaji watatu wa TCRA

Benz Petrol

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
504
195
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amewasimamisha na kuwastaafisha kwa manufaa ya Umma baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuhujumu kifaa cha mawasiliano. Waliosimamishwa ni:

1. Mkurugenzi idara ya sheria Elizabeth Nzagi ambaye amesimamishwa na kustaafishwa kazi
CbgydahWEAMJrLQ.jpg



2. Kaimu Mkurugenzii anayesimamia mitambo na kuchunguza mapato katika mitambo ya simu Mhandisii Sunday Richard
IMG_9056.jpg


3. Kaimu mkurugenzi idara ya sheria Bwana Modestus Ndunguru.
ngungu.jpg

Source: ITV habari

*UPDATES*

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa amewasimamisha na kuwastaafisha kwa manufaa ya Umma baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Taarifa hiyo ameitoa leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mara alipokutana na Waandishi wa Habari ambapo ameeleza kuwa, hatua hiyo imetokana na kutofungwa kwa kifaa kinachowezesha mtambo wa kufuatilia Mapato ya Simu (TTMS) hali iliyopelekea Mamlaka ya Mawasiliano na Mamlaka ya Kodi kushindwa kubaini mapato halisi ya makampuni ya simu na hivyo kushindwa kukokotoa kodi stahiki zinazotakiwa kulipwa na makampuni ya simu nchini na kuikosesha Serikali mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 400 pesa za kitanzania.

Akieleza kuhusu kazi za mtambo huo, Profesa Mbarawa amesema kuwa, mtambo ulitakiwa uwe na uwezo wa kufanya kazi ya kuhakiki ubora wa huduma za mawasiliano, kutoa Takwimu za mawasiliano yanayofanyika ndani na nje ya nchi, kutambua mapato na miamala ya fedha mtandao, kufuatilia na kugundua mawasiliano ya ulaghai, kutambua taarifa za laini ya simu na za kifaa cha mawasiliano pamoja na mapato ya simu za ndani.

''Kwa kushindwa kutoa ushauri wa Kisheria na kitaalamu, kwa uzembe au kwa manufaa yao binafsi, Mkurugezni wa Idara ya Sheria Bi. Elizabeth Nzagi na wasaidizi wao akiwemo Kaimu Mkurugenzi anayesimamia Mtambo wa Kuchunguza Mapato katika Mitandao ya Simu (TTMS) Injia Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Bw. Modestus Ndunguru wamesabbisha mtambo huo kufuatilia mapato ya simu kutoka nje ya nchi pekee na kutofungwa kifaa kinachowezehsa mtambo huo kufuatilia mapato ya simu za ndani,'' alisema Profesa Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kusitisha mara moja Mkataba wa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Bi. Elizabeth Nzagi ambapo pia ameigaiza Bodi hiyo kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Mkurugenzi anayesimamia Mfumo wa kuhakiki na kusimamia huduma za Mawasiliano (TTMS) Injinia Sunday Richard na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sheria Bw. Modestus Ndunguru ili kupisha uchunguzi dhidi ya uhusika wao katika kusababisha kutofungwa kwa kifaa kinachowezesha mtambo wa kufuatilia Mapato ya Simu (TTMS) ili kufuatilia mapato ya simu za ndani ya nchi.

Profesa Mbarawa pia ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt. Ally Simba kwa kutokuwa makini na utendaji wake mpaka kupelekea kutokea kwa hali hiyo na kuhakikisha kuwa tabia hiyo haijirudii tena.

"Namwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Dkt. Ally Simba kuhakikisha kuwa, ndani ya siku saba, Kampuni iliyofunga mtambo huo inafunga kifaa hicho kinachotambua mapato ya simu za ndani, naielekeza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina tangu mtambo ulipofungwa na utaratibu mzima uliotumika kuipata Kampuni iliyofanya kazi hiyo," aliongeza Profesa Mbarawa.

Mnamo tarehe 22 Machi mwaka 2013 Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliingia Mkataba na Kampuni ya Consortium of Societe Generale de Surbveillance SA (SGS) na Global Voice Group (GVG).
 
Umemsahau na mkurugenzi wa temesa nae katumbuliwa. Kiukweli huyu amecheleweshwa sana. Vivuko vingi vibovu, leo tumepanda mv magogoni likapotea na kuanza kuelekea kule upande wa bandarini, yani ni hatari tupu, hawa watu hela wanapata vivuko havitengenezwi.
 
Hapa kazi tu, TBA,AQRB tegeni miguu kwenye vitanda daktari anakuja majipu yatumbuliwe.
Majengo ni jipu na kodi zake.
 
Jipu kubwa wizara hiyo ni katibu mkuu upande was mawasiliano. Huyo jamaa magufuli alipaswa amtumbue badala ya kumteua. Time will tell. Huyo jamaa ni mwizi was hatari. Ni mla rushwa was hatari. Ni mtu was ten percent was hatari. Sijui raisi alifanya uchunguzi gani hadi kufikia kumteua huyo bwana. Angeuliza alipotoka angejibiwa na asingethubutu kumteua.
 
January Makamba ubongo ulikua paralyzed alivyokuwa akisimamia haya.
Mkuu Daudi,

Huyu Mbarawa si ndiye alikuwa Waziri wa Sayansi na Teknolojia na Makamba akiwa Naibu wake!

Haya yalosababisha hawa watendaji wa TCRA wastaafishwe yametokea leo ama ni wakati wake akiwa huko?

Hao jamaa wa tcra yaani zaidi ya TRA. Wana fedha balaa na wanajilipa salary za hatari. Wachunguzwe pia.
 
Hapa kazi tu, TBA,AQRB tegeni miguu kwenye vitanda daktari anakuja majipu yatumbuliwe.
Majengo ni jipu na kodi zake.
TBA wanajenga mjengo yasiyo na mvuto, ya kizamani sana. kwa mfano jengo lao jipya opp. na TEMESA Arusha, pia kuna lingine karbu na office za migration Arusha.

Ramani mbovu, please CAG ayachunguze tujue ukwel.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom