Waziri wa TAMISEMI kutia saini mradi wa DMDP wiki ijayo

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,123
7,709
kufuatia swali lililo ulizwa na Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mhe. Mtemvu leo tarehe 26/5, Naibu waziri alitoa majibu kuwa;
barabara zote katika halmashaur zote za Jiji la DSM zita jengwa/kukarabatiwa.

Halikadhalika Naibu waziri ameongeza kuwa Wiki ijayo Waziri wa Tamisemi Mhe. Kairuki atatia saini kuanza kwa mradi huo wa DMDP.

Jimbo la Kibamba haswa eneo la Gogoni kuelekea Hondogo katika shule za sekondari hondogo barabara hizi ni mbovu sana, hivo wananchi watawashangaa viongozi wao Mbunge na Diwani wao kama barabara hizo hazito kuwepo kwenye mradi wa ujenzi.

Jimbo la kibamba kwa ujumla limesahaulika sana kwenye mradi wa DMDP, hivyo ni muhimu sasa kutoa kipau mbele zaidi kwa Jimbo la kibamba na haswa barabara hizo nilizo zitaja, Gogoni kuelekea kwenye shule za sekondari Hondogo lakini pia kuelekea kwenye mashamba ya kilimo cha mbogamboga kwenye maeneo hayo ya Hondogo.

Pongezi kwa Mbunge wa Kibamba na Diwani wa Kata ya Kibamba kwa jitihada za kuondoa kero za wananchi.
 
Back
Top Bottom