Shagiguku
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 407
- 133
Mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani, napenda nikufahamishe kwamba, ukiwa mkoani mwanza ukaingia katika kituo cha polisi cha kati (mwanza central police) kisha ukapanda ngazi na kuingia katika ofisi ya UHASIBU basi humo utakutana na watu wengi sana wanakwenda kulipa malipo mbalimbali.
Na humo ndani ya ofisi hiyo utakuta kuna meza tatu, basi wewe fika katika meza yoyote kati ya hizo ukiomba kulipia kitu chochote kwa mfano: road licence, kadi iliyopotea, kitambulisho kilichopotea, lincence ya udureva, liseni ya ukaguzi wa magari nk, nk. Baada ya kuelezwa fedha halali unayotakiwa kulipia ili upatiwe ile risti yetu ya njano tunayoitambua kwamba ni ya serikali, basi hapo ndo utasikia mmoja wa wahasibu hao (hasa atakayekuwa akikushughulikia suala lako) akikuambia uongezepo TSH. 5,000/= eti ya maji ya kunywa kwa vile mle ndani ya ofisi wamesweti sana hakuna hewa ya kutosha, tena anakwambia wazi wazi bila aibu wala woga wowote ule akisisitiza kwamba kama siyo hivo basi urudi ukapange foleni (ambayo kwa kweli ni ndefu tu).
Sasa mheshimiwa waziri hii rushwa inafanyika hadi ndani ya ofisi nyeti kama hii, je hao maturafiki huko barabarani watatubakisha kweli!!?
Na kama ni suala la kusweti ndani ya ofisi ya serikali basi tunawaomba muwawekee feni au kiyoyozi ili wasiwe wanasweti ili wasiendelee kutuomba sisi wateja TSH. 5,000/= ya maji ya kunywa.
Napenda kuwasilisha.
Nakala kwa:
1. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi mh. Nchimbi, J. - kwa taarifa.
2. Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Saidi Mwema. - kwa taarifa.
3. Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza. - kwa ufuatiliaji.
4. Mkuu wa kituo cha polisi cha kati mwanza. - sijui wewe kwa kitu gani maana walarushwa uko nao ofisini kwako...!!
5. Idara ya uhasibu jeshi la polisi kituo cha kati mwanza. - tumekwisha wafahamu hivo mkae mkao wa kushughulikiwa.
6. Great Thinkers wote kwa taarifa.
7. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania - Jakaya Mrisho kikwete - ukipenda fanya kusafisha hili jeshi usipopenda waache ili waendelee kutukaanga sisi wapiga kura tuliokuweka madarakani.....!!