Travis Kitengo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 489
- 1,200
Kwanza nitoe pongezi za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunda kikosi kazi kinachoshughulikia kero za wanufaika wa huduma ya maji,hapa namaanisha wateja waliounganishiwa huduma ya maji.Baadhi ya kero ni kama uhalali wa bili,miundombinu nk
Kikosi kazi hiki kinaundwa na baadhi ya maafisa wa mamlaka ya maji mji,Afisa wa TAKUKURU wilaya nk.Kwa halmashauri ya mji wa Bunda nimeona kiongozi wa kikosi kazi hiki ni askari POLISI mmoja aliyejitambulisha kwa cheo cha Inspekta(Jina kapuni)
Nini hasa msingi wa kuandika hili andiko?
Kikosi kazi hiki kimefanya ziara kwa baadhi ya Taasisi mfano katika mashule nk.
Katika kituo X kilichopo ndani ya halmashauri ya mji alianza mchangiaji wa kwanza ambapo alitoa kero zake za kiufundi zinazomkabili ambazo zilijibiwa kwa ufasaha kabisa na maafisa wa idara ya maji.Baada ya hapo alifuatia mtoa kero wa pili ambapo yeye alijikita kwenye hoja kuhusu uwepo wa kundi linalohujumu miundombinu ya maji maeneo ya mjini na hasa ung'oaji wa mabomba na koki za maji hali ambayo hupekekea maji mengi kupotea na hivyo mteja na serikali kupata hasara kila mwaka.Mtoa kero alienda mbali zaidi kwa kudai kuwafahamu baadhi ya wahusika wa hujuma hizo na aliahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa kikosi kazi hicho kama kitahitajika kuwanasa wahalifu hao!
Dharau,kejeli na vitisho vya Askari kiongozi wa kikosi kazi kuhusu mtoa kero husika.
Kwa kuwa swala au kero hii ilikuwa inahusu makosa ya jinai na uhalifu ilikuwa ni moja kwa moja ijibiwe na askari husika ambaye ndiye kiongozi wa kikosi kazi husika,askari huyo alitumia muda mwingi kukanusha mambo yaliyoongelewa na mtoa kero,yaani badala ya kuandika kero husika na hata kupongeza mchangiaji ili zije zifanyiwe kazi,askari husika aligeuka kuwa advocate wa watuhumiwa kwenye issue husika hali iliyowashangaza hata wajumbe wenzake na watumishi katika kituo husika.Mtoa kero kwa ujasiri alimuomba askari azichukue hizo kero ili kama akihitajika kutoa ushirikiano atakuwa tayari kufanya hivyo.Askari kwa aibu akaziandika kishingo upande.
Madhara au matokeo ya Dharau kwa askari husika kwenye kikao husika...
Wajumbe wengine hawakuona umuhimu wa kuendelea na utoaji wa kero/maoni baada ya kuona mwenzao akidhalilishwa na mtu ambaye anahisi kuwa na kofia ya Inspekta wa polisi ana mandate ya kufanya chochote kile akisahau miiko na maadili ya kazi ya polisi.Wengi walishauri kama askari huyo ataendelea kuwa kiongozi wa kikosi kazi hiki,matokeo ya kilichokusudiwa itakuwa ni kupoteza muda na kuwavunja moyo wanatimu wengine.Timu haitafanikiwa kufikia malengo waliyoyatarajia!
Wito na ushauri kuhusu huyu Inspekta wa Polisi
Tunamshauri Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Maji halmashauri ya mji wa Bunda kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Bunda pamoja na vyombo vingine vya kiuteuzi kuangalia uwezekano wa kutengua nafasi ya askari husika kama kiongozi wa kamati husika na kutafuta mtu mwingine mwadilifu .Kituo cha Polisi Bunda kina maafisa wengi tu wa Polisi wenye weledi wa kufanya kazi hii kiuelevu.Kuendelea kuwatumia watu wasio na weledi ni hujuma ya wazi dhidi ya Serikali na watu wake.
Pia askari husika atambue cheo ni dhamana.Cheo ni mali ya umma.Cheo ni kwa ajili ya kutumikia umma,cheo ni kama koti la kuazima Leo unalo kesho utalirudisha kwa mmiliki.Pia afanye kazi kwa weledi kwa kuzingatia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na apunguze kujiona Mungu mtu!Mahali panapohitaji hoja,ajibu kwa hoja badala ya vitisho kwa mtoa hoja!
Nakala
Waziri wa maji
Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Bunda,
Kamanda wa Polisi wilaya ya Bunda,
Mkurugenzi mamlaka ya maji wilaya ya Bunda ,